Wakati ulimwengu ukiyumba kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, wajasirimali wanatafuta uchumi mbadala ambao wanaweza kuuamini kwa ajili ya kuhifadhi na kuzalisha pesa zao.
Ktk mazingira hayo kuna sababu nyingi za kuamini kwamba uchumi unaofuata sheria za ki-Islam unajiuza, na hilo limetokana na misingi yake ktk kukataa riba, kukataa kitu kinachijulikana kama ‘short selling na baadhi ya miamala ya kibiashara inayoendelea duniani.
Ni kwa sababu kama hizo ambapo ulimwengu uliingia ktk matatizo makubwa ya kiuchumi na kuwafanya wajasirimali kutafuta uchumi mbadala ambao unaongozwa kwa misingi madhubuti na kwa umakini wa hali ya juu imefahamika.
Kufuatia mazingira hayo kiongozi wa Dubai Sheikh Mohammad Bin Rashid Al Maktoum mapema mwaka huu ametangaza kwamba ana mpango wa kuifanya Dubai kuwa makao makuu ya uchumi unaofuata sheria za ki-Islam.
Kama hatua ya kulifanikisha hilo, Sheikh Mohammad alitangaza mkakati ya kuibadilisha Dubai kua makao makuu ya Sukuk (Islamic bonds) ambazo zitahamasisha mashirika na nchi mbalimbali kutoa Islamic bonds badala ya zile zile zisizokua za ki-Islam.
Ktk hatua nyingine ni kuundwa kwa jopo la kisheria la pamoja ambalo litashughulia na maswala ya viwango. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuata sheria za ki-Islam tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com