Hali inavyojionyesha sasa ni kuwa filamu za kiswahili miaka michache ijayo zitakuja kuteka soko katika nchi nyingi duniani kuliko ilivyo sasa hivyo hakuna haja yoyote ya kutumia kiingereza katika filamu zetu sisi kama waafrika tunaopaswa kuendeleza na kukuza mila na tamaduni zetu ikiwemo lugha ya kiswahili ambayo ni lugha inayozungumzwa na mataifa mbalimbali.
Watengenezaji wa filamu nchini Denmark ni kama wanatupa ishara kuwa filamu za kiswahili ni lulu huko ulaya hivyo tufanye juu chini kuongeza ubora katika filamu zetu ili kuteka soko la dunia.
Tantine ambaye jina lake halisi ni Tatu Daniel Musa ni actress anayekubalika nchini Denmark akiwa tayari amecheza filamu chache tu huku filamu yake ya JABUKA ikiwa imemfanya akubalike vizuri kwa mashabiki. Filamu hiyo imetumia lugha ya kiswahili hivyo kuonyesha kuwa kiswahili kinatuunganisha watu wengi Afrika, ulaya na marekani.
Tantine muigizaji aliyejaaliwa mvuto wa aina yake ana asili ya Tanzania na Congo. SWP ilipomuuliza anavutiwa na kazi za actors gani katika nchi za africa mashariki alijibu kuwa anapenda kazi za Irene Uwoya and Wema Sepetu.
Actress huyu anayezungumza kiswahili, kidanish na kiingereza anasema kuwa filamu za kiswahili zinapendwa katika nchi za scandnavia lakini tatizo ni kuwa hazifiki huko hivyo wadau kukosa filamu hizo pengine ikiwa sababu kubwa kwa wao kuanza kutengeneza filamu kwa kiswahili ili kuwapa wadau kitu wanachotaka.
"Kwakweli filamu za kiswahili zina pendwa sana apa Scandinavia Kuna wadau wengi wanatamani movie za kiswahili ila wanakosa sehemu za kuzinunulia ili wazione".
Hilo linatokea hasa kutokana na nchi nyngi za scandinavia kuwa na ushirikiano wa karibu na nchi za africa mashariki na pia mara nyingi wanamuziki wa Tanzania wakialikwa kufanya show katika nchi hizo. Hata hivyo subtile ya kiingereza bado ni muhimu ili kuzidi kuwavutia wasiojua kiswahili ili kukuza soko zaidi.
Hili linatakiwa kuchukuliwa seriously kwa wasambazaji na watengenezaji wa filamu za kiswahili katika kusambaza filamu katika nchi ambazo kazi zao zinakubalika hii ndivyo inavyofanyika hata Hollywood na Bollywood kutoa kipaumbele na kufanya utafiti wa soko katika nchi wanazohisi kazi zao zinakubalika.
Serikali yetu nayo kupitia kwa rais Kikwete isikie kilio hiki cha wasanii wa filamu maana kama serikali ikiwa serious itakusanya mapato mengi sana kupitia filamu na wasanii kuwa na kipato kizuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Pichani ni muigizaji Tantine anayeishi Denmark