Ankal na bendi yake aliyoipa jina la Orchestre les Libeneke akiwa mazoezini na vijana wake kwenye kambi ambayo kwa sasa jina kapuni kwa kuhofia wadaku. Tayari bendi hiyo ina nyimbo nne huku ikifanyia kazi mbili zaidi, kabla ya kuingia studio kurekodi.
Akiongea na mwandishi wetu wa maswala ya burudani kwa njia ya simu, Ankal amesema ameamua kujiingiza katika muziki kwani umo ndani ya damu yake ambapo kaka yake mkubwa Ismail ni mmoja wa waanzilishi na wanamuziki wa awali wa Dar International ya Marijani Rajabu. Pia Ankal anasema anafanya sana mazoezi na Wananjenje na hivi sasa anakaribia kuhitimu kupiga drums.
Hakupenda kuweka bayana bendi itazinduliwa lini na wapi, ila alisisitiza ni kabla ya SabaSaba mwaka huu. Hivi sasa anatafutwa producer mkali wa kurekodi nyimbo zao pamoja na video. Huenda wakamtumia tiketi Producer mkali Miika Mwamba aliko huko Sweden aje ashurikiane na wakali wa nyumbani kufanya vituzzzz.
Ankal akiwa na kijana wake Omary Makuka ambaye naye alipigia Dar International. Kwa sasa wanakamilisha nyimbo mbili za mwishio kabla ya kuingia studio. Katika hizo sita mbili ni 'Remix' ya ngoma za
Marijani Rajabu 'Mayasa' na 'Rosa Nenda Shule'