Kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam juzi siku ya Ijumaa Kuu tarehe 29 Machi, 2013 mpaka sasa maiti za watu 30 zimepatikana.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, watu 17 waliweza kuokolewa, wanne kati yao bado wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wengine walitibiwa na kuruhusiwa.
Kazi ya kufukua eneo la ajali inaendelea na sasa inakaribia kufikia ukingoni.
.