Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

UPDATES: JK ATEMBELEA TENA ENEO LA TUKIO, WANNE MBARONI, KAZI YA KUCHIMBA KIFUSI INAENDELEA

$
0
0

 Eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa sita mchana leo maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha. Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa jicho la wasiwasi.
 Rais Kikwete akiwa eneo la tukio tena leo, baada ya kutembelea jana,  akitoa maagizo kwa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kwamba kila aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji, msimamizi na mjenzi wahojiwe na wawajibishwe wakipatikana na kosa 
 Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa jana, Ijumaa, Machi 29, 2013, ametembelea jengo  lililoporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kwenye Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro mjini Dar es Salaam na amesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo hilo.

Rais Kikwete anawapa pole nyingi wafiwa, anawapa pole nyingi walioumia na wanaoendelea kupatiwa matibabu baada ya kubanwa katika kifusi, wakiwamo watoto wadogo ambao walikuwa wanacheza chini ya jengo hilo la ghorofa 16 wakati lilipoporomoka asubuhi ya jana huku likiendelea kujengwa.

Rais Kikwete amewapongeza na kuwashukuru wananchi wote walioshiriki na wanaendelea kushiriki katika zoezi la uokoaji pamoja na vyombo na taasisi za umma na Serikali zinazoshiriki katika zoezi na kazi hiyo ya uokoaji.

Amewataka waendelee na jitihada hizo ili kama kuna watu ambao bado wamebanwa kwenye kifusi waweze kuokolewa ili wapatiwe matibabu, na kama watakuwa wamepoteza maisha basi miili yao ipatikane na iweze kupewa mazishi ya heshima yanayostahili mwanadamu.

Wakati alipotembelea eneo la tukio hilo, Rais Kikwete ametoa maelekezo mahsusi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadik pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova.

Rais amewataka kuhakikisha kuwa Mjenzi wa jengo hilo, Mhandisi Mshauri aliyekuwa anasimamia ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam  ambaye alitoa kibali cha ujenzi na ndiye Mkaguzi wa ujenzi pamoja na mwenye Jengo wanapatikana haraka na kuwajibishwa ipasavyo.

Aidha, Rais Kikwete amezitaka taasisi za kitaaluma zinazohusina na shughuli za ujenzi – Wachoraji Majengo, Wakadiriaji Majengo, Wajenzi, Wakandarasi na Wahandisi nazo zichunguze tukio hilo kwa haraka na kwa karibu, ili zibaini yapi yalikuwa ni matatizo na zichukue hatua kwa mujibu madaraka na mamlaka ya taasisi hizo kwa sababu zinayo madaraka na mamlaka hayo.

Rais pia amesema kuwa wakati umefika kwa taasisi hizo sasa kujihusisha kwa karibu zaidi na matatizo yanayojitokeza katika shughuli za ujenzi kwa sababu kila yanapoporoka majengo inakuwa heshima mbaya kwa taasisi hizo. 

Hivyo ni muhimu kwa taasisi hizo kufanya uchunguzi wa kubaini nini chanzo cha kila tukio kuanzia na lile la jana – kama ilikuwa ni udhaifu katika uchoraji, kama ilikuwa ni udhaifu katika ukandarasi, kama ilikuwa udhaifu na Ushauri ili hatua stahiki zichukuliwe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>