Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

wanamuziki wa nyimbo za injili kutoka afrika kusini,Drc-Congo,rwanda na zambia wawasili jijini Dar tayari kwa tamasha la pasaka hapo kesho uwanja wa Taifa.

$
0
0
Pichani kati ni Mwanamuziki nguli wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Sipho Makhabane alipowasili usiku wa jana kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na baadhi ya wanamuziki wenzake (hawapo pichani),tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama.

Mwanamuziki nguli wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Sipho Makhabane akizungumza na Wanahabari wa vyombo mbalimbali mara alipowasili usiku wa jana kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na baadhi ya wanamuziki wenzake (hawapo pichani),tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31
Mwanamuziki Sipho Makhabane akibadilishana mawazo na Mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za Kiroho hapa nchini,Upendo Kilahiro,mara baada ya kuwasilia usiku wa jana kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Wanamuziki wa kiroho wa kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda wakizungumza na baadhi ya Wanahabari wa vyombo mbalimbali mara walipowasili mapema jana jioni kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka  litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31,ambapo pia watazindua albamu yao mpya itakayoitwa Mtegemee Yesu yenye nyimbo kama vile  Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.
Baadhi ya Wanamuziki wa nyimbo za kiroho wa kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda wakiwasili mapema jana jioni kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka  litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31
Mwanamuziki Ephraim Sekeleti wa Zambia ambaye  pia aliwasili jana kwa ajili ya kutumbuiza tamasha la Pasaka.Tamasha la Pasaka litafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijni Dar es Salaam kesho na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles