Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

WATEJA WANAOTUMIA HUDUMA YA M-PESA SASA KUTUMIA ATM ZA DTB KUTOLEA FEDHA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati,(kushoto)akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi ya kutoa fedha kwenye mashine za kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote walipo nchini,huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dares Salaam pamoja nae ni Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,akitoa fedha kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kutoa fedha kupia mashine za kutoa fedha za DTB kupitia huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.
Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.wakifurahia mara baada ya kutoa fedha kwa mara ya kwanza kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kwa huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini.

Ukuaji wa teknolojia ya huduma maarufu ya kutuma, kupokea fedha pamoja na kufanya malipo ya huduma mbalimbali kwa njia ya simu za mkononi ya kampuni ya Vodacom ya M-pesa inazidi kupanuka na hivyo kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma hiyo kuzidi kuboresha maisha na kuyafanya kuwa rahisi zaidi.

Katika kufikia mafanikio hayo Benki ya Diamond Trust (DTB) leo imetangaza ubia wa kibiashara na kampuni ya Vodacom Tanzania ubia ambao unawawezesha wateja wa M-pesa kuwa na uwezo wa kutoa fedha kutoka katika akuanti za M-pesa kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM) za benki ya Diamond Trust.

Wakitangaza na kuzindua huduma hiyo jijini Dar es salaam Mkuu wa Kitengo za Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati, amesema hayo ni mafanikio mengine ya kibishara kwa benki hiyo ya DTB katika kupanua wigo wa huduma na namna benki hiyo inavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuleta urahisi kwa watanzania.

"DTB inayo Furaha kubwa kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiteknolojia hapa nchini. Hii ni huduma ya kwanza na ya aina yake ambayo hakuna shaka kwamba inaashiria uwezo wa DTB katika kuleta ufumbuzi wa namna bora ya kutumia teknolojia kurahisisha maisha."Amesema Bahati

"Tukishirikiana na Vodacom tunawawezesha wateja wa M-pesa walio karibu na benki zetu na hususan mtandao wa ATM kuwa na uhakika wa kutoa fedha kutoka akaunti zao za M-pesa saa ishirini na nne katika siku zote saba za wiki."

Bahati amesema jambo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini.

Hata hivyo hii ni frusa ya kipekee kwa wateja wa benki ya DTB ambao wamejiandikisha kwa ajili ya huduma ya M-Pesa hawana haja tena ya kutembelea matawi ya benki hiyo ili kuweza kuweka amana zao au kuhamisha fedha kwa biashara, marafiki na familia zao. Pia uzinduzi wa huduma hiyo utawezesha kujenga urahisi wa kuruhusu wasiotumia huduma ya benki kupata huduma za kifedha karibu nao.

Azma ya DTB ni kuzidi kuongeza kasi na maboresho ya utoaji wa huduma kwa wateja wake na washirika wake wengine kwa kuhakikisha inaendelea kupanua wigo wa huduma zake ikiwemo kuongeza ATMs, matawi na huduma nyinginezo kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kibenki nchi nzima.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa M- Biashara wa Vodacom Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa." Voogtz ameongeza kuwa ubia huo ni mwendelezo wa azma ya kampuni ya Vodacom kutumia fursa za teknolojia ya M-pesa kuzidi kuleta amsiha ya watu mikononi mwao kutumia simu za kiganjani.

"Wateja wa Vodacom M-pesa wanayo sababu nyingine ya kujivunia kuwa sehemu ya mtandao mpana wa huduma hii salama, rahisi na yenye kuaminika zaidi nchini wakiunganishwa na makampuni na hata tasisi zaidi ya 200 kufanya malipo ya huduma na manunuzi kwa urahisi na wepesi zaidi kupitia simu za viganjani."Aliongeza Voogtz

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>