Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

KAGASHEKI: TEKELEZENI WAJIBU KWA KUZINGATIA KANUNI NA TARATIBU

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza wajibu wa kutekeleza kazi kwa ubunifu na uadilifu huku wakizingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia utendaji kazi.

Balozi Kagasheki alitoa rai hiyo wakati akifungua rasmi mkutano wa 20 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jijini Dar es Salam.

Mhe. Waziri aliwataka wajumbe wa wajumbe wa baraza hilo kutambua kuwa Baraza ni chombo muhimu kwa ajili ya kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

“Tumieni vema nafasi mlizonazo kuhakikisha kuwa haki na wajibu wa Mwajiri na Mtumishi vinapewa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa kulinga maslahi ya pande zote mbili kwa manufaa ya Taifa zima.

“Moja ya changamoto mliyonayo kama Baraza hili ni kuhakikisha watumishi wanazingatia nidhamu na maadili katika utumishi wa umma. Ninafahamu mazingira ya kazi na hasa katika vituo vyetu si ya kuridhisha, lakini ni vyema tukahimiza watumishi kufuata kikamilifu Sheria, Kanuni na taratibu za utendaji wa kazi”, anasema Kagasheki.

Anasema wajumbe wakitekeleza wajibu wao kama Wajumbe wa Baraza, watarahisisha kazi ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Aidha, aliwataka katika utekelezaji wa majukumu yeao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano, utendaji kazi kama timu moja kwa uwazi na kuaminiana hususan katika maamuzi yanayohusu wengi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>