Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kupambana na utumwa unaoendelea hivi sasa kila pembe ya dunia.
Professa Ali Mazrui, Mwanazuoni maarufu akisaidiwa kuketi kabla ya kuzungumza katika siku hii ya maadhimisho ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa .
Professa Mazrui akizungumza ambapo pamoja na mambo mengine alielezea histotia ya utumwa na biashara ya utumwa pamoja na harakati mbalimbali zilizopelekea kukomeshwa kwa biashara hiyo. pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa kuendelea kuwaenzi waathirika wa ukatili huo, alitaka pia kuenzi yale mema ambayo baadhi yake ni matokeo ya historia hiyo ya Utumwa, Professa Mazrui alikuwa mzungumzaji mkuu katika maadhimisho haya ambayo hufanyika Machi 25 ya kila mwaka.
BANGO lilombeba ujumba wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa, maadhimisho ambayo yalifikie kilele Marchi 25 hapa Umoja wa Mataifa.