Naibu Waziri Tamisemi(ELIMU) Ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ,Kassim Majaliwa Akipokea msaada wa mashuka 100 kwa Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto kwa ajili ya vituo vya Afya vya wilaya hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto akikabidhi mashuka 140 Diwani wa kata ya Singino/Kivinje,Jafari Arobaini shuka ambazo zitasambazwa katika vituo vya Afya vya wilaya hiyo.
Na Abdulaziz Video,Globu ya Jamii - Lindi
Imeelezwa kuwa Hospital ya Wilaya ya Kilwa/Kinyonga Mkoani Lindi Inakabiliwa na Upungufu Mkubwa wa Shuka kwa ajili ya Wagonjwa wanaolazwa katika Hospital hiyo pamoja na Vituo Vitano vya Afya Wilayani humo.
Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa Wilaya ya Kilwa Dr Mike Mabimbi baada ya kukabidhiwa mashuka 140 na Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto katika hafla fupi iliyofanyika katika hospital hiyo.
Amesema kwa sasa hospital yake yenye vitanda 90 kila kitanda kinatumia mashuka mawili tu kwa siku ambayo hayakidhi mahitaji kwa mgonjwa alielazwa ambae anapaswa kuwa na mashuka manne kwa siku Dr Mabimbi amesema kupatikana kwa mashuka hayo kutasaidia baadhi kusambazwa katika vituo vya Afya katika kata za Tingi,Nanjirinji,Pande,Njinjo na Masoko ili kupunguza tatizo hilo sugu kwa Wagonjwa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwamoto amesema msaada huo ni katika Juhudi za Mfuko wake kuhakikisha kuwa Wagonjwa wanaolazwa hospitalini wanapatiwa huduma Muhimu za Kijamii ikiwa ni pamoja na matibabu mazuri .
Aidha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekabidhi mashuka 100 kwa ajili ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi katika Hafla fupi zilizofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa na Hospital ya Wilaya ya Kilwa(KINYONGA)