Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SIKU 3 WA MABADILIKO YA TABIANCHI JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, wakati akifungua mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Machi 21,2013 kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Fereji, wakionyesha moja vitabu vya Mabadiliko ya Tabianchi, baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabinchi, ulioanza leo Machi 21, 2013 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (kushoto) ni Makamu Katibu Mtendaji wa UNFCC, Richard Kinley.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mwakilishi wa Balozi wa Denmark, Hanne Fritzen,wakionyesha moja vitabu vya Mabadiliko ya Tabianchi, baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabinchi, ulioanza leo Machi 21, 2013 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Fereji.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwahutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>