Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akielezea huduma mpya ya Airtel yatosha yaani Simu kadi moja, taifa moja, bei moja inayomwezesha mteja wa Airtel kuwasiliana na mitandao yoyote nchi na kupata kifurushi cha muda wa maongezi, sms, na internet kwa bei nafuu hadi shiling 349/= pichani (katikati) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Meneja masoko Airtel Anethy Muga
Mkurugenzi mkuu wa Airtel bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel yatosha inayomwezesha mteja wa Airtel kupata dakika za muda wa maongezi,sms na kifurushi cha internet.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, huduma hii imebeba ujumbe wa simkadi moja, taifa moja, bei moja.
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, huduma hii imebeba ujumbe wa simkadi moja, taifa moja, bei moja.
========== ========== =========
Airtel yazindua gharama nafuu za kupiga simu mitandao mingine
* Airtel yadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja -
Wateja nchini kufaidika na kiwango cha chini cha hadi 75% kupiga simu
popote bila kikomo
* Piga simu muda wowote usiku and mchana
Dar Es Salaam Jumatano 20 Marchi 2012. Airtel Tanzania leo imezindua
huduma mpya ijulikanayo kama "AIRTEL YATOSHA" itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa kiwango nafuu cha hadi asilimia 75 bila kuwa na sababu kubadili simu laini kwa kuhofia gharama.
Huduma ya AIRTEL YATOSHA inadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei
moja inayoendeleza dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora na nafuu
ambapo wateja wa Airtel sasa watapata ofa ya kifurushi kitakacho wapa
muda wa maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet ambacho
kinaweza kutumika kwa siku au kwa wiki kulingana na mahitaji ya wateja
Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa huduma hiyo iliofanyika
katika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw
Sunil Colaso Alisema" Huduma ya Airtel YATOSHA ni maalum kwa kila
mtanzania, hii itawarahisishia watanzania wote kupata mawasilino
nafuu kwa kupiga bila kikomo kwenda mitandao mingine nchini.
Kupitia
kifurushi cha Airtel YATOSHA wateja wa Airtel watafurahia kiwango cha
chini cha hadi shilingi 349/=, hii inamaana kwamba mteja atapata
dakika 10 za kupiga simu kwenda mtandao wowote muda wowote, pia SMS
100 (ujumbe mfupi wa maneno) pamoja na kifurushi cha intenet cha 25MB
ofa itakayotumika masaa 24 kwa siku
Faida za AIRTEL YATOSHA kwa mteja zinadhihirisha dhamira yetu Airtel
ya kutoa huduma za mawasiliano bora na nafuu nchini. Airtel
tunazingatia kuwa wateja wetu wanamahitaji tofauti na ndio sababu
kubwa inayotufanya tuwe wabunifu kwa kuwapatia huduma zinazogusa kila
aina ya wateja na kuleta mabadiliko halisi kwa kuwapa wateja wetu nchi
nzima thamani ya pesa zao
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi,i Beatrice
Singano Mallya alisema " Airtel YATOSHA ni huduma inayopatikana kwa
SIKU au kwa WIKI hivyo mteja anapewa nafasi ya kuchagua anachokata.
Katika mpango wa WIKI mteja atatozwa shilingi 1,999 na kupata dakika
70, sms 700 na kifurushi cha interneti cha 175MB.
Kujiunga na huduma hii mteja anatakia kupiga *149*99# na kuunganisha
moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchangua kifurushi
anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na
kifurushi cha internet. Dakika za maongezi zitatumika kupiga simu
kwenda mtando wowote nchini kwa massa 24 na gharama za kupiga simu
zitatozwa kwa sekunde.
Kuhusu muda wa kujiunga na Airtel YATOSHA mteja anaweza kujiunga
wakati wowote kati ya 0500hrs to 2359hrs,
Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zenye
ubora na ubunifu nchini. Na hii ni njia nyingine ya kudhihirisha jinsi
Airtel inavyotoa huduma za mawasiliano yenye ubora na gharama za
ushindani kwa watanzania. Airtel itaendelea kuwa chachu ya maendeleo
kwa kutoa huduma bora zenye gharama nafuu.