Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na Mwenyekiti wa kampuni ya Poly Technologies Inc ya China, Bw. Zhang Zhengao (katikati). Mwenyekiti huyo aliongozana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo ili kueleza nia yao ya kuwekeza katika ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea kutokana na gesi asilia katika mkoa wa Mtwara au Lindi.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Mwenyekiti wa kampuni ya Poly Technologies Inc ya China, Bw. Zhang Zhengao ramani ya bomba la gesi kutoka Mnazi Bay Mtwara hadi Dar es Salaam na kumfafanulia kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya gesi asilia.
Wajumbe wakimsikiliza rais wa kampuni ya Poly Technologies Inc ya China, Bw. Wang Lin (aliyenyoosha mkono) wakati wa kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa wizara.