Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

shilingi bilioni 18 kutumika katika uchimbaji wa visima

$
0
0
Na Frank John-Maelezo. 
 Jumla ya shilingi bilioni 18 zitatumika kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20  vya maji vitakavyokuwa na  uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 266 kwa siku katika maeneo ya Kimbiji wilaya ya Temeke na Mpera wilayani Mkuranga kuanza mwezi wa sita mwaka huu na kukamilika mwezi wa sita mwaka 2014.

Hayo yamesemwa leo na afisa mtendaji mkuu  wa mamlaka  ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)  Archard Mutalemwa wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kwa  kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea maeneo ya miradi ya visima hivyo.  

Mutalemwa alisema kwamba utafiti uliofanywa  umeonesha kuwa maji hayo ni safi na salama kwa matumizi ya binadamu na tayari mkandarasi kwa ajili ya kutekeleza wa mradi huo ameshapatikana . Pia mpango huo utahusisha maeneo kadhaa ikiwemo upanuzi wa kituo cha Ruvu juu ambao utaanza  Julai mwaka huu na kukamilika  Machi mwaka 2015.

“Tumeandaa mpango maalum wa kuhakikisha tunatatua  tatizo la maji safi linalowakabili wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga  bwawa la Kidunda kuanzia  Septemba mwaka huu na upanuzi wa mtandao wa mabomba utakaoanza mwakani na miradi yote hii itakamilika  mwaka 2015”, alisema Mutalemwa.
 
Aliitaja miradi mingine katika mpango huo kuwa ni upanuzi wa mfumo wa majitaka unaotarajiwa kuanza mwakani na kukamilika mwaka 2016 na  upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini.
 
Kwa upande wa mradi wa upanuzi wa Ruvu Chini ambao unagharamiwa na Serikali ya Marekani kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 57, Mutalewa alisema kuwa utaongeza uwezo wa upatikanaji wa maji lita milioni 270 kwa siku.
 
Naye Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Dk. Binilith Mahenge alisema kuwa shilingi bilioni 27 zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi watakaotakiwa  kupisha mradi huo na  aliwataka wananachi wa jiji la Dar es Salaam kuipa Serikali muda wa kufanya kazi hasa za kutatua tatizo la maji.
 
Tatizo la upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam limekuwa ni changamoto kubwa ambapo hadi sasa DAWASA ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 300 kwa siku huku mahitaji yakiwa ni lita milioni 450.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles