Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

DUCE yazindua Diploma ya Juu ya Elimu

$
0
0
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kimeanzisha program mpya ya Diploma ya Juu ya Elimu iliyoanza chuoni hapo hivi karibuni. Programu hiyo inatolewa massa ya jioni na ina lenga kuwapa fursa watu ambao wangependa kujiendeleza katika taaluma ya ualimu lakini hawana muda wa kujiunga na masomo katika muda wa kawaida. 

Programu hii inatolewa kwa watu ambao wana shahada au stashahada katika fani nyingine nje ya ualimu lakini wangependa kujiunga na taaluma ya ualimu au tayari wanafundisha lakini hawakusomea ualimu. Progranu hii pia inawafaa watu wanaoendesha shule kama wamiliki au viongozi wa shule.
Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Dkt Kitila Mkumbo akitoa maelezo yanayohusiana na program mpya ya Diploma ya Juu ya Elimu inayosimamiwa na kitivo cha Elimu, kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Godliving Mtui.
Naibu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Godliving Mtui akikabidhi makabrasha mbalimbali kwa wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa program hiyo.
Wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa program hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>