Assalam akaykum
Nimeona nichukue nafasi hii nitoe mapendekezo maana sijaona mwananchi kuchangia mawazo kutokana na matatizo yaliyopita ya mitihani Tanzania sasa kwa upande wangu nina haya naomba sana tena sana niwekee japokuwa ni marefu kidogo lakini nahisi ni jambo muhimu:
Mfumo wa Elimu Ningependekeza ungekuwa hivi:
Kuwepo na Tuition Resources (iwepo Online au hata maktaba zetu) ambayo itakuwa na mgawanyiko wa mambo makuu matatu (3) nayo ni haya:
1. 1. Syllabuses (Silabas)
2. 2. Lecture Guides (Muongozo wa Kusoma na kusomesha)
3. 3. (a) Specimen question papers. (Sampuli ya Maswali) (b) Past Question papers and Answers.(Maswali na Majibu ya Mitihani iliyopita)
Mambo ya Nyongeza :
· Kama kutakuwa na mabadiliko yoyote kwa mtihani ujao uelezwe hapa.(MFANO Masuala mangapi yanatakiwa yajibiwe yameongezeka au kupungua)
· Kama kutakuwa na Mabadiliko au nyongeza ya Syllabus vile vile ioneshwe hapa.
· Ripoti ya Mtihani ambayo ieleze wapi wanafunzi walifanya uzuri na wapi bidii iongezwe na wapi walifanya vibaya.
· Vidokezo vya kusoma (Reading Tips)
· Listi ya Vitabu au website za kutafuta material zaidi (Reading lists)
· Kuwepo na Manual au Mkusanyiko wote wa masomo ambayo kama kutakuwa na mabadiliko yaelezwe kama nilivoorodhesha hapo juu wapatiwe wanafunzi kwa either bure au pesa kidogo walipie
· Kuwepo na reward kwa wanafunzi waliofanya vizuri na utambulisho mfano watolewe kwenye majarida maalum ya elimu ambayo yatasambazwa bure au hata kwa fee ndogo.
Ufafanuzi kidogo
1. Sylubuses : Zioneshe mgawanyiko wa masomo ambao mwanafunzi akitoka atatoka na ujuzi mfano somo la Biologia
1. Agriculture iwepo na core unit (masomo ya lazima) na optional zake asipandikizwe mwanafunzi mambo ya Anatomy au Biochemistry au biomechanics pamoja na masomo yanayohusu Agriculture, (information overload).
2. Lecture guides: ambayo itagawika kwa:
(a) Learning outcomes (Mwanafunzi aelezwe umuhimu wa hicho unachomsomesha
kwanza kabla hata ya kwenda kwenye mada.
(b)Indicative contents ( Ambazo zipo kwa number mfano Somo la Human Resources
1.1Definition, 1.2.Work related stress ,1.3 Equality) Hii itamsaidia mtu kukumbuka
ambapo akijibu suala la mtihani kuwa topic hii ni topic ya 1.3. au 2.4.au hata
akitafuta material online yatamuonesha kuwa soma topic no.1.3 au 3.4 n.k
(c)Examination tips (Muhimu sana unamueleza mwanafunzi atarajie swali la aina
gani katika topic hii na jibu la aina gani ajibu)
3. (a) Specimen Question papers ambazo zinakuwepo mwanzo wa mwaka kuonesha mwanafunzi atarajie masuala ya aina gani yatakuja katika mtihani sasa anajifanyia mara kwa mara kujibu maswali haya kwa kutumia resources mbali mbali na pia zioneshe marks ambazo atapata kwa kila suala atakalojibu .
(b)Maswali na majibu ya mtihani iliyopita,ni muhimu kwa kuwa unamjengea
mwanafunzi jinsi gani ya kujibu masuala au atarajie nini ,
Hitimisho
Wengi watasema mfumo wa maswali na majibu wanafunzi watakuwa hawasomi wata solve maswali tu,lakini sio kweli mfano yakiwepo maswali ya somo la Biologia tokea ya mwaka 2005 naamini kujibu mara kwa mara haya maswali yanakujengea confidence na ufahamu vile vile na mara nyingi elimu ni ile ile mambo madogo madogo tu yanaongezeka ambayo hata kwenye mitihani ya ulaya huwekwa kijiswali kidogo tu kimoja cha mark ndogo kutokana ni jambo jipya.
Mfumo huu pia unatumika U.K mfano maswali ya interview unatakiwa uyasome na sio uwende interview kichwa kichwa,
masuala ya driving lesson unakuwa na CD na vitabu ambayo kwenye mtihani wenyewe yanakuwa hayohayo
Masuala ya uraia unapewa kitabu unasomeshwa hivo hivo hata masuala ya shule .
Sasa tuchukue mfano wa Driving lesson unajiona unajibu tu maswali lakini utakapoanza kuendesha je halikujii swali ulosolve ukaona aha nilisolve hili swali kuwa round about nikae upande gani sasa je si ujuzi huu?
Haya ndio nionayo mimi ila kila mtu ana mawazo yake
Ahsanteni.
Dr.Abdul AE
University of Huddersfield