Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jana (Tar 12/03/2013) kwa kauli moja ilipitisha bajeti ya Tshs. 156,439,616,904 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam.
Kati ya fedha hizo Tshs. 49,206,498,064 ni mapato ya ndani ya Manispaa, ambapo zaidi ya 50% ya bajeti imelenga kuhudumia miradi ya maendeleo zikiwemo barabara, maji, shule, hospitali, mikopo ya vijana na wanawake na masoko.
Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda alisema Manispaa yake imejipanga kuhakikisha inasimamia miradi hiyo ili ilete mabadiliko ya kuchumi katika Manispaa hiyo.
“Tumejizatiti kuisimamia vizuri miradi hii ili ilete tofauti katika Manispaa yetu ya Kinondoni.” Alisema.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika jana (Machi 12) katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu wake, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty akizungumza wakati wa Kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana (Machi 12). Katikati ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda na Naibu wake, Songoro Mnyonge.
Sehemu ya Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakifuatilia kwa makini wakati wa Kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana (Machi 12).