Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam. (picha: Magreth Kinabo - MAELEZO)
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amewataka viongozi nchini kuienzi na kuithamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.
Kauli hiyo imetolewa na Mzee Kingunge Ngombare Mwiru ambaye alikuwa mgeni ramsi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Kitabu hicho kimeandikwa na Mathias Eugen na uzinduzi wake uliandaliwa na familia ya Kaluta wakishirikiana na baadhi ya wataalamu wa lugha hiyo kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA). Kitabu hicho kimekusanya kazi mbalimbali zilizofanywa na Hayati Kaluta wakati wa uhai wake.
Mzee Kingunge anawaasa Watanzania kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali, mfano Bungeni.
“Lugha ni chombo cha msingi kwa binadamu pia inatofautisha kati ya binadamu na viumbe vingine ambapo kupitia lugha ndipo tunapokuza uwezo wa kufikiri kwani huwezi kukuza uwezo wa kufikiri biala ya kuwa na lugha ya kueleweka,”alisema Kingunge na kuongeza: “Hatima ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio wanaweza kukipandisha au kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee Kingunge.
Hata hivyo, aliunga mkono lugha hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa changamoto kuwa yatupasa kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya msingi, sekondari hadi vyuo vikuu. Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake kuwa masomo mengine kama vile hesabati wanapata alama 90 hadi 95, lakini lugha hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo inaelekea ufundishaji wake ni tatizo.
“Kama kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimua ya Chuo Kikuu,”alisema, huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno ambayo si sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.
Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha hiyo Profesa Mugyabuso Mulokozi na Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuenzi fasihi za Watanzania.
Watu wengine mashuhuri waliohudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na Balozi Job Lusinde, Suleiman Hega na Hashim Mbita.