Mtoto Simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma alilazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza kutokana na mtoto huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .
Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya .
Mtoto Simon Mlope alikubwa na ugonjwa huo wa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo inamsababishia mtoto huyo kuvuta pumzi kwa shida.
Mama wa mtoto Simon Mlope anayeitwa AMINA ALLY anawaomba watanzania kumsaidia mtoto wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari kuwa Simon anatakiwa kwenda nchini india kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2006 huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.
Majirani wa familia ya Simon nao wanasema kuwa mtoto huyo anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.
Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la MLOPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MLOPE atumie simu namba
0752732290
Mtoto Simon Mlope anavyoonekana hivi sasa kutokana na maradhi ya moyo yanayomsumbua.
Mtoto Simon Mlope akiwa na Mama yake Mzazi atambulikae kwa jina la Amina Ally.