Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

WAKAZI ZAIDI YA 160,000 JIJINI MWANZA KUNUFAIKA KWA MRADI WA MAJI KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI(SBL)

$
0
0

Mke wa rais mama Salma Kikwete akisaidiana na Meneja miradi wa

SBL Nandi Mwiyombela wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji la Mwanza
Getrude Ngonyani kuashiria kuanza kutumika kwa kisima kwa ajili ya wakazi wa Mwanza.


 Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria
uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa ajili ya wakazi zaidi ya 160,000 waishio jijini Mwanza, kushoto kwake ni 
Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Pascal K. Mabiti na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Jaji Mark Bomani.
Meneja miradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL) Nandi Mwiyombela
akitoa maelezo kwa mke wa Rais mama Salma Kikwetejuu ya kisima
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti katika Hospitali ya
mkoa wa Mwanza - Sekou Toure.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akihutubia wakazi wa jiji la
Mwanza(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti katika eneo la  hospitali ya Sekou Toure ulifanyika Alhamisi ya wiki hii.
Meneja miradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela
katikati akisalimiana na mke wa rais mama Salma Kikwete mara baada
yakuwasili katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwaajili ya
uzinduzi wa kisima cha maji na pembeni yake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mwanza Patrick Kisaka.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>