Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

DHANA YA UJIRANI MWEMA YAPUNGUZA MATUKIO YA UJANGILI KWENYE HIFADHI

$
0
0
Mahmoud Ahmad Monduli

IMEELEZWA kuwa Ujirani mwema katika hifadhi za taifa hapa Nchini imepelekea matukio ya ujangili kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na jamii kuwa makini kwa kutoa taarifa kwa wanaohusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu

Pia katika kuhakikisha zana ya ujirani mwema inafanikiwa katika jamii inazozunguka hifadhi hizo ni pamoja na kutoa elimu kuhusu uhifadhi na kujenga mahusiano mazuri.

Akizungumza hivi karibuni na jamii Mwansishi wa habari katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Mhifadhi msaidizi hifadhi ya Manyara idara ya ujirani mwema Bw.Goliath Mtawa alisema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali wanazokutananazo katika kutekeleza miradi husika, jamii imeonekana kuithamini miradi hiyo.

Bw.Mtawa alisema kuwa ili jamii ithamini miradi hiyo ni pamoja na kuchangia asilimia 30 ya pesa au nguvu kazi,mali gafi inayopatikana katika eneo husika na hifadhi kuchangia asilimia 70 ya mradi uliyoibuliwa.

“Jamii inapochangia kokoto,mchanga,nguvu kazi katika miradi huwafanya wao kuthamini miradi kwa kiasi kikubwa zaidi”alisema Bw.Mtawa.

Akielezea changamoto wanayokumbana nayo katika kutekeleza baadhi ya miradi ni pamoja na umaskini ndani ya jamii yenyewe hali inayopelekea kushindwa hata kuchangia katika miradi iliyoibuliwa na kupitishwa hivyo kuifanya miradi hiyo kutofanyika kwa wakati.

Alitaja baadhi ya miradi waliiyotekeleza kwa jamii kwa mwaka wa fedha 2011-12ni pamoja na kuweka mfumo wa umeme wa jua katika shule ya sekondari Silahamo Wilayani Karatu iliyogharimu shilingi Milioni 35,Josho la kuogeshea mifugo katika kijiji cha Moyamayoka Wilaya ya Babati Milioni 17 na laki tano

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>