Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko mabao 7-6.
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima akikabithi kombe captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko mabao 7-6
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda) kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akimtambulisha Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima ambaye wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.