Na Mwandishi Maalum
Imeelezwa kwamba ujumbe wa amani unaweza kuenezwa kwa njia nyepesi na rahisi kama ile ya kuwatumia vijana na watoto kutumia vipaji vyao kuchora michoro inayobeba ujumbe unaosisitiza umuhimu wa amani duniani.
Hayo yameelezwa na Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya miaka mitano ya “Jioni ya Amani”, ambapo Asasi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama CITYarts Pieces for Peace ilionesha kwa wageni waalikwa michoro mbalimbali iliyochorwa na watoto kutoka nchi 62 zikiwamo za Afrika.
Madhumuhi ya hafla hiyo ambayo Ubalozi ulikuwa mwenyeji yalilenga katika kuonesha ni kwa namna gani watoto wanavyoweza kuhuburi na kuienzi amani kupitia sanaa ya uchoraji na kwa njia hiyo pia kukuza vipaji vyao.
CITYarts Pieces for Peace ambayo makao yake yako New York, imekuwa ikitembelea nchi mbalimbali, na kuwahamasisha watoto na vijana kuchora iwe kwenye makaratasi, mabango au hata kuta kwa lengo moja tu la kueneza ujumbe wa amani.
Balozi Manongi amewashukuru waandaaji wa hafla hiyo kwa kubuni wazo hilo jema la kuwahamasisha watoto kutumia vipaji vyao vya uchoraji kuhubiri amani hasa kwa kuzingatia kwamba mara nyingi mawazo wanayotoa watoto yanakuwa hayajachakachuliwa.
Naye Mkurugenzi wa CITYartsPieces for Peace, Bi Tsip Ben-Haim pamoja na kuushukuru Ubalozi wa Tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa hafla hiyo, amesisitiza haja na umuhimu kwa jumuia ya kimataifa kuienzi amani kwa hali na mali.
Akasema kwamba uamuzi wa Asasi yake wa kuanzisha program hiyo ya kuwashirikisha watoto kupitia sanaa kueneza ujumbe wa amani, imekuwa na mafanikio sana na kwamba program hiyo imesambaa katika nchi nyingi.
Michoro wanayochora watoto na vijana hukusanywa na kuwekwa katika mabango ambayo waandaaji wa michoro hiyo husafiri nayo kila nchi wanayokwenda na kuionesha kwa watu wengine na kwa namna hiyo kueneza ujumbe wa amani kutoka taifa moja hadi taifa jingine.
watoto hawa Linda, Maria, Stephen na Alex nao walipata fursa ya kutoa ujumbe wao wa amani kwa njia ya michoro, michoro hapa wapo bize kila mmoja akichora ujumbe wake alioubuni mwenyewe.
Na utamduni wetu ulikuwapo, watanzania hawa, Eri Fungo na Amiri Koba hawakuwa nyuma kurindimisha midundo iliyosherehekesha hafala hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa CITYart akielezea madhumuni ya hafla hiyo na kubwa zaidi ushirikishwaji wa watoto katika kueneza ujumbe wa amani
Wageni
Balozi Tuvako Manongi akiwashukuru waandaji wa hafla hiyo pamoja na wageni waliofika, katika mazungumzo yake mafupi, Balozi alisititiza kwamba watoto na ambao mawazo yao hayajachakachuliwa.
Wageni waalikwa wakisoma ujumbe wa amani
Wageni waalikwa wakipata kitu kidogo walichangamkia sana Maandazi