Wafanyabiashara wa kitimoto mjini Iringa wakionyesha milango yao iliyofungwa na mgambo leo kama njia ya kupinga uuzaji wa nyama ya nguruwe (kitimoto)
Hapa wakiamua kuchimba barabara kuzuia magari kupita eneo hilo
Maandamano ya kupinga marufuku ya uuzaji wa kitimoto leo
Na Francis Godwin
Wafanyabiashara wa kitimoto katika eneo la vibanda vya UVCCM mjini Iringa leo wamewatimua mgambo wa Manispaa ya Iringa ambao wamefika eneo hilo kufunga biashara zao kama njia ya kunusuru wananchi na ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12 jioni baada ya ofisa mifungo Manispaa ya Iringa akiwa na mgambo kufika eneo hilo kufunga biashara zote za kitimoto eneo hilo.
Wakizungumzia hatua hiyo wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanashangazwa na uamuzi huo wa uongozi wa afya Manispaa ya iringa kuwazuia wao kufanyabiashara hiyo wakati maeneo mbali mbali maarufu nyama hiyo ikiendelea kuuzwa kama kawaida .
Hivyo wameutaka uongozi wa Manispaa ya Iringa kusitisha mpango huo kwani unawatesa wananchi hao wajasiriamali wenye kipato cha chini ambao wanategemea biashara hiyo.
katika hatua nyingine wafanyabishara hao na wateja wao wamewatimua mgambo hao na ofisa mifugo huyo katika eneo hilo kwa madai muda waliokuwa wakifanya kazi ni muda ambao si wa kazi na kudai kuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa .