|
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hab Mkwizu akifungua Mkutano wa siku mbili kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka utumishi wa umma. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili mbinu na mikakati ya kuboresha masilahi na tija kwa watumishi nchini na ulifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. |
|
Katibu wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi. Tamika Mwakahesya akitoa mada juu ya Muundo na Majukumu ya Bodi hiyo kwenye mkutano wa siku mbili wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika jijini Dares Salaam. |
|
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kushoto) akijadiliana jambo na wadau wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa Bodi hiyo wa siku mbili uliowahusisha Wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika hivi karibuni jijini Dares Salaam. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya, wakifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu -Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Lucy Matozi na Mkurungezi wa Rasimali watu –Bunge, Bibi. Kitolina Kippa |
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu wa tatu kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa mkutano wa siku mbili Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumushi wa Umma na wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika jijini Dares Salaam