Pambano la masumbwi kutetea makanda wa mabara wa WBF(world boxing forum) wategemea kufanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga kwa kuwakutanisha Alan Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa mkanda huo aliouchukua nchini Malawi kwa kuzipiga na Jumanne Mohamed wa tanga ambae anavyo vigezo na sifa zote za kuugombania ubingwa huo.
Jumanne Mohamed ambae alipata nafasi ya kugombania ubingwa wa dunia nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na mnamibia nafasi hiyo imejirudia tena,safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini mwake.Muandaaji wa pambano hilo Ally Mwanzoa akizungumza na viongozi wa ngumi nchini pamoja na katibu mkuu wa ngumi za kulipwa Ibrahim kamwe amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan kamote autetee mkanda wake alioupata Blantaya nchini Malawi usije ukapoteza kwa kutokuutetea ubingwa wake huo, na kukaa na uongozi wa ngumi kwa kuangalia bondia gani anafaa na ikaamuliwa jumanne Mohamed anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi.mwanzoa aliendelea kwa kusema pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi kati jj ngotiko na haji juma wa Tanga katika pambano la raund kumi, na kutakuwepo na mapambno mengine mengi y a utangulizi.