Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Tbl yakabidhi msaada wa magodoro vituo vya Afya mjini Moshi

$
0
0
Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii,Moshi.

WADHAMINI wakuu wa mbio za Kilimanjaro Marathon, kampuni ya Bia ya TBL, imekabidhi msaada wa magodoro na vyandarua kwa uongozi wa hosptali ya Huruma na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni kama sehemu ya maandalizi ya mbio za Kilimanjaro marathon zinatarajia kufanyika machi 3.

Misaada ya aina hiyo hufanywa kila mwaka na TBL wakati wa maandalizi a Mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurudisha faida iliyopatikana kwa wananchi kutokana na utumiaji wa bidhaa zake.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi, alisema kuwa TBL imeamua kufanya utaratibu huo ambao wamekuwa wakifanya kila mwaka na mwaka huu wameonelea ni vyema wakatoa msaada katika hospitali hizo.

Kilindi alisema kuwa msaada wa magodoro hayo 210 na vyandarua 200 ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisa jamii ya Tanzania inafurahi na kujivunia kilicho chao na kuongeza kuwa hicho wal;ichokitoa ni sehemu ya shukuruni kwa watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mara.

“Kama wadhamini wakuu wa mbio hizi, tumekuwa tukishiriki katika shughuli nyingi za kijamii na moja yao ni kutoa msaada katika mahospitali, leo tunatoa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa hospitali za Kiaseni ya Rau na Huruma ya Rombo, tunaamini katika hili tutakuwa tuimesaidia kwa kiasi fulani,” alisema Kilindi.

Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahimu Msengi akipokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa hospitali hizo aliipongeza TBL kwa kuamua kuijali jamii inayonunua na kutumia bidhaa zao na kuongeza kuwa msaada huo anaamini utakuwa wa manufaa makubwa kwa wagonjwa katika hospitali hizo.

“Moyo wa kutoa sio lazima uwe nacho, TBL wameonesha kuwa kazi yao sio kutengeneza bia tu, bali wanaweza kujali jamii na katika hili nawapongeza sana na ningependa mashirika na makampuni mengine nayo yangekuwa yanafanya hivi,” alisema Msengi.

Msengi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote na wamiliki wa makampuni kuiga mfano mzuri ulioonesha na TBl na kusisitiza umuhimu wa kutoa kwani jukumu la kuhudumia jamii ni la kila mtu na sio serikali pekee.

Kuhusu mbio za mwaka huu za Kilimanjaro marathon Dkt. Msengi alisema, mbio hizo kufanyika katika ardhi ya Kilimanjaro ni fahari na kuongeza kuwa matarajio ya wote ni kuona kila mtu akinufaika na mbio hizo huku akiwatakia kila kheri wakimbiaji wote hasa wakimbiaji wa Tanzania.

“Nitumie Fursa hii kuwatakia kila la Kheri wakimbiaji wote wa Kilimanjaro marathon, kila la kheri watanzania wote watakaotuwakilisha keshokutwa naamini tutashinda,” alisema.

Kwa upande wake Mganga mnku wa mkoa wa Kilimanjaro (RMO), Dk. Mtumwa Mwako, akipokea magodoro na vyandarua hivyo kutoka kwa kaimu mkuu wa mkoa kwa niaba ya uongozi wa Hospitali za Kiaseni na Huruma, alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa mama na mtoto.

Nao madaktari kutoka katika hospitali hizo, Dkt. Godwin Kiwelu wa hospitali ya Huruma ya Rombo na Dk. Delfina Materu wa hospitali ya Kiaseni ya Rau, walisema kwa msaada huo mzigo wa changamoto zinazokabili hospitali hizo zimepungua huku wakisisitiza kuwa bado kuna changamoto nyngi ambazo inatakiwa jamii inatakiwa kujitokeza kusaidia kama walivyofanya TBL.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>