Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

WAMASAI WAPONGEZWA KWA KUJALI ELIMU YA WATOTO WAO.

$
0
0
Picha na Habari na John Nditi, Morogoro. 

 JAMII ya Wafugaji wa Kimasai wanaishi Kijiji cha Kambala, Kata ya Hembeti, wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro wamepongezwa kwa kuitikia wito wa kuwasomesha watoto wao ikiwa ni hatua ya kuwarithisha elimu kuliko mifugo. 

 Pongezi hiyo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa The Foundation For Civil Society (FCS), John Ulanga , katika hotuba yake kwa jamii hiyo wakati wa ziara yake alipokitembelea Kijiji cha Kambala chenye asili ya wafugaji wa kimasai na kuwakuta wakiwa na mwamko wa kuwasomesha shule watoto wao.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo ambaye alifuatana na baadhi ya wawakilishi wa nchi za Ulaya zinafadhili mfuko ,aliwasifu wafugaji wa jamii hiyo kwa kuamua kuuza sehemu ya mifugo yao na kupata fedha za kuwasomesha shule watoto wao. 

 “Pamoja na kuona maendeleo ya jamii wa wafugaji wa kimasai wa kijiji hiki, wito wangu kwa wengine ambao wana ng’ombe wengi tumieni kuendeleza watoto wenu kielimu huo ni urithi pekee tofauti na mali ama ng’ombe” alisema Ulanga. 

 Wakizungumza mbele ya wajumbe hao, wafugaji wa jamii hiyo walisema kutokana na kutambua umuhimu wa elimu , wameamua kujenga hosteli ya wanafunzi wakike wa shule ya Msingi Kambala ambao wanatoka maeneo ya vitogoji vya mbali na shule . 

 Mweyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kambala, Issaya Rijiwa, alisema mbele ya ujumbe huyo, jamii hiyo imeamua kuchanga kila mmoja wao sh: 10,000 kwa ajili ya kupata fedha za ujenzi wa Hoteli hiyo na itakapokamilika utakiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200. 

 “ Tumeanza mchakati wa kukusanya fedha na kupima eneo la ujenzi ambapo awamu ya kwanza ni kukamilisha jengo la kuchukua watoto 60 na tumelenga wanafunzi wakike ambao hawamudu kutembea umbali wa kilometa zaidi ya 10” alisema Rijiwa. 

 Naye Mwenyekiti wa Society for Women and Aids in Afrika (SWAA)- Morogoro,Hellen Mbezi, alisema kuwa uamuzi wa kujenga Hosteli ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kambala ni hatua ya kuwalinda watoto na vitendo viovu hasa wanapokuwa njiani kwenda Shuleni. Alisema, wananchi wa Kata 12 za Wilaya ya Mvomero wamepatiwa elimu juu ya kuwalinda watoto na katika Kijiji cha Kambala, wananchi waliamua kuibua mradi wa ujenzi wa Hoteli ili watoto wajamii ya wafugaji hasa wakike wanaishi karibu na shule. 

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka , liupongeza mfuko wa FCS kwa kuonesha umakini katia utendaji wake wa kazi kusaidia vikundi vya wananchi vinavyoanzishwa kwa malengo ya kutoa huduma kwao. Hata hivyo alisema , kufuatia msaada wa Mfuko huo wa kusaidia kutoa fedha kwa ajili ya mchakato wa ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kambala , Serikali ya Wilaya pamoja na Halmashauri itaunga mkono jitihada hizo wakati jengo litapaofikia usawa la kutaka kupauliwa.
 Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Anthony Mtaka ( kati kati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation For Civil Society , John Ulanga , ( wapili  kushoto) wakipata nyama choma ya mbuzi  iliyoandaliwa na Jamii wa wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Kambala, Kata ya Hembeti, iliyopo wilayani humo  wakati baadhi ya wajumbe wa kutoka nchi mbalimbali za Ulaya zinazofadhili  mfuko huo walipoitembelea jamii hiyo  juzi , kijijini hapo.
 DC ANTHONY MKATA AKIONESHA CD ILIYOREKONDIWA MPANGO KAZI WA UJENZI WA HOSTELI YA WANAFUNZI WA JAMII YA WAFUGAJI WA KIMASA
 Baadhi ya wawakilishi wa nchi wafadhili wa mfuko wa FCS wakisikiliza tafsili ya hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( hayupo pichani) kijijiji Kambala
 Elizabeth Anania , mkazi wa kijiji cha Kambala akisoma risala ya wanakijiji ikielezea mpango wa ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa shule ya Msingi karibu na Shule yao
 Mkurugenzi Mtandaji wa FCS, John Ulanga ( mwenye koti jeusi) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka( kati kati) kijijini Kambala
 Katibu wa kwanza wa Ubalozi nchi ya  Netherlands hapa nchini, Orjen Kool akitafakari ulaji wa nyama choma ya mbuzi  iliyoandaliwa na Jamii wa wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Kambala, Kata ya Hembeti, wilayani Mvomero , eneo la Shule ya Msingi ya Kijiji hicho wakati ujumbe wa wa kutoka nchi mbalimbali za Ulaya zinazotoa ufadhili katika mfuko wa The Foundation For Civil Society walipowatembelea kijijini hapo,juzi  (wenye kuvaa koti) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, John Ulanga.
Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili wa jamii ya wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Kambala wakiwa nje ya viwanja vya shule ya Kambala

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles