Leo jijini Dar es salaam kulikua na tafrija ya kutambua makampuni yaliyofanya vyema kuanzia kipindi mwaka 2012 hadi kufikia hadhi ya kupata cheti cha taasisi inayotambulika kimataifa ya Superbrands. Benki ya CRDB ikiwa ni benki pekee kutoka Tanzania ambayo imepata cheti hicho kwa miaka miwili mfululizo iliyopita, mwaka huu imeweza kuendeleza rekodi yake kwa kupata tena hadhi ya kuwa Superbrand hivyo kufanya benki hiyo kupata cheti hicho kwa mara ya tatu mfululizo.
Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrand, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrand.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay wakati wa tafrija ya kupokea cheti cha Superbrand
Baadhi ya wageni walio hudhuria tafrija hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza na waandishi wahabari juu ya sababu zilizoipaisha Benki ya CRDB hadi kutunikiwa cheti cha Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo pia mikakati ya benki hiyo katika kuboresha huduma zake ili kuendeleza rekodi yake ya kupata cheti hicho kila mwaka.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay(kulia) akipokea cheti cha Superbrand kutoka kwa mkurugenzi wa Superbrand, Jawad Jaffer