Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

wanafunzi walioshinda shindano la kuandika insha wazawadiwa

$
0
0
Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee zawadi ya redio (music sytem) Winfrida Leonard kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA – Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
Faiza Ussi kutoka shule ya Sekondari ya Sunni Madressa ya mjini Zanzibar alifurahia zawadi ya laptop aliyopewa hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
Meneja wa shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama Ali Mindria (kulia) akipokea kombe la ushindi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee kutoka kwa Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA). Wanafunzi wane kutoka shule hiyo waliingia kumi bora kwa kushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa kati ya wanafunzi 32 walioshiriki shindano hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo shule ya WAMA-Nakayama aliibuka mshindi wa jumla.
Washindi kumi walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za kimarekani. Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>