Ilikuwa saa 11.00 jioni, siku kama ya leo tarehe 27 February, 2006 ulipotutoka. Wakati bado tulikuhitaji sana, tulidhani ni ndoto tu.Japo sote tuliamini kuwa siku moja ungeamka ukiwa mzima.Mama,japo leo ni miaka saba tangu ututoke,bado tunahisi tuko ndotoni na tumeshindwa kabisa kukubaliana na ukweli kwamba haupo nasi. Mara kwa mara nakuona ndotoni, lakini ninapoamka nagundua ni ndoto tu,na hiyo inazidisha uchungu na majonzi.
Japo siku zote tangu ututoke tumekuwa na wakati mgumu sana ,siku hii ya leo tunapoadhimisha miaka saba ya kifo chako ni ngumu zaidi kwetu.Inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.
Kazi ya Mungu haina makosa.Tukijiuliza sana kwanini alikuchukua wakati bado tunakuhitaji sana tutakuwa tunakufuru.Tunajaribu kujifariji kwa kuamini kuwa alikuchukua kwa vile alikupenda zaidi yetu.Na tunajitahidi pia kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani na unaangaziwa mwanga wa milele ukistarehe kwa amani.Japo haupo nasi kimwili lakini siku zote tupo nawe kiroho
Unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa Bupe, Lilian na Shirima, Fred na Furaha bila kuwasahau wajukuu zako Irene-Kanyampa, Aziz-Elian, Rose, Junior-Ereneus na Katarina.
Pumziko la Milele Akupe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Akuangazie Ustarehe Kwa Amani, AMEN