Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete akipokelewa na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule,kwenye Zahanati ya Nyamisati , iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani akiwa ni Mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea na baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete(katikati) pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani Bw.Haruna Mhina,wakipokea msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea nao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,mara baada ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo Nyamisati iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamebeba mabox yenye vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingi Mil 20 kwa ajili ya kutoa msaada katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani Rufiji vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo juzi.