Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

INTRODUCING "USINIENDESHE" BY NINI


INTRODUCING "Wamechana Mkeka" by Soggy Doggy Feat.Shiva&Map Star

BEI ZA BIDHAA MBALIMBALI KATIKA SOKO LA KIWALANI JIJINI DAR

$
0
0
 Bei za bidhaa mbalimbali katika soko  la Kiwalani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, kama zinavyoonekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG).

 Bei ya mchele katika soko la Kiwalani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo.

Nazi katika soko la Kiwalani.

BRAZIL ACCREDITS ENVOY TO EAC BLOC

$
0
0
cid:image001.png@01D4BE42.6CDFEB00EAC Secretariat
ISO 9001:2008 Certified
East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 21st February, 2019: The  Ambassador of the  Federative Republic of Brazil to the United Republic of Tanzania HE. Antonio A.M. Cesar today presented accreditation letter to the Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko to also serve as Ambassador to the East African Community.

Amb. Cesar informed the Secretary General that his government attaches great importance to regional economic groupings such as the EAC and congratulated the EAC Secretary General for the wonderful regional initiatives.

“Count on Brazil support because the goals of the Community are excellent for the prosperity of the people in the region”, asserted the Brazilian Envoy, adding that “regional integration initiatives take time but you need to continue so as to build a strong and powerful bloc”.

He hailed the EAC as one of the fastest growing RECs in the world and said Brazil and the Southern American Common Market (MERCOSUR) of which Brazil is a member had a lot to learn from the EAC.

While receiving the Brazilian Ambassador, the EAC Secretary General hailed the existing cordial relations between the EAC and Brazil. He welcomed the support from the Brazil Government geared towards enabling the Community to achieve its ambitious agenda.

The Secretary General briefed him  on the progress being registered by the Community so far that include implementation of Protocols on the Customs Union, Common Market,  East African Monetary Union and Political Federation.

Amb. Mfumukeko further disclosed that the EAC Partner States had started  drafting  Constitution for EAC Confederation which is the model for a Political Federation that had been adopted by the Heads of State Summit.

He informed the Brazilian Ambassador that the EAC has  close working relationships with other RECs in Africa which are all geared towards promoting the African Union's vision of an African Economic Community.

Present at the accreditation occasion were the EAC Deputies Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote and  Hon. Christophe Bazivamo of the Productive and Social Sector.
 The  Ambassador of the  Federative Republic of Brazil to the United Republic of Tanzania HE. Antonio A.M. Cesar  present accreditation letter to the Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko
 Amb. Liberat Mfumukeko and HE. Cesar in discussion during the accreditation ceremony

From (L-R) EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote; Brazilian Ambassador HE Cesar; Amb. Liberat Mfumukeko and EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sector. Hon Christophe Bazivamo
Amb. Liberat Mfumukeko and Brazilian Ambassador, HE Cesar displays the EAC plaque

USHINDI DHIDI YA YANGA LAZIMA. ASEMA KOCHA WA NAMUNGO FC BAKARI MALIMA JEMBE ULAYA

$
0
0
Kocha wa Timu ya Namungo FC ya  wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Bakari Malima "Jembe Ulaya"   amejigamba kuondoka na Ushindi dhidi ya timu ya yanga SC ya Jijini Dar es salaam katika Kombe la Shirikisho la Azam ASFC.
Timu ya Namungo ambayo inaongoza katika msimamo wa ligi daraja la kwanza  inatarajia kucheza na Yanga siku ya Jumapili wiki hii wakiwa katika mwendelezo wa kusaka tiketi ya kwenda robo fainali.
Bakari Malima anasema anaifaham Timu ya yanga Vizuri hivyo anauhakika wa kupata ushindi akiwa katika kiwanja cha nyumbani.
“Mimi Yanga nawafahamu nje ndani...sidhani kama watapata mteremko kama wanaotarajia. Nina uhakikia kwa kuwa gemu yenyewe tunachezea hapa nyumbani hivyo tunauwezo wa kufanya Vizuri”amesema kocha Malima.
Licha ya kujiandaaa vizuri timu hiyo ina majeruhi wanne wa kikosi cha kwanza ambapo kocha tayari ameanza kuandaa vijana wengine ili kuweza kuziba pengo la wachezaji hao.
‘’tatizo lililopo kwenye timu yangu sasa hivi kunamajeruhi kama wanne wa kikosi cha kwanza na niwachezaji tunaowategemea lakini tayari kuna vijana tunawanadaa kuchukua nafasi”
Hata hivyo Malima amewaomba mashabiki wa mikoa ya kusini kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya namungo kama moja ya Timu inayowakilisha Mikoa ya Kusini.
Tayari kikosi cha Timu ya Yanga SC kinachojumuisha wachezaji 20 kimeondoka jijini  Dares salaam Ijumaa asubuhi ya kuelekea wilaya ya Ruangwa Mkaoni Lindi tayari kucheza na timu ya Namungo.
 Namungo FC ya wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi mazoezini
Bakari Malima "Jembe Ulaya" Kocha wa Timu ya Namungo FC ya wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi 

RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA JENGO LA SKULI YA SEKONDARI YA MICHEZANI PEMBA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar amesema kuwa siasa za vyama vingi zimekuja kwa lengo la kushidana kwa Sera na sio kukashifiana. 

Rais Dk. Shein aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mkoani Pemba pamoja na kufanya Majumuisho ya ziara yake kwa Wilaya hiyo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua, iliyopo Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba ambapo viongozi kadhaa walihudhuria akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.

Katika hotuba yake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Dk. Shein alisema kuwa siasa za vyama vingi havikuja kwa lengo baya la kukashifana na badala yake vina lengo zuri la kushindana kwa Sera ili iwe kivutio kwa wanachama na sio ugomvi.

Hivyo, Rais Dk. Shein aliwasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kuishi kwa mapenzi na kufahamiana sambamba na kushirikiana pamoja kwao wote ni ndugu.

Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwataka viongozi wa CCM kutembelea Matawi, Wadi, Majimbo na Wilaya zao sambamba kuwatembelea wananchi na wanachama wa chama chao ili kuwasikiliza changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.

Pia, Rais Dk. Shein aliwataka viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo kuimarisha miradi ya ili chama hicho kiweze kupata mapato ya kuweza kukiimarisha na kuapata mafanikio makubwa zaidi.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa tayari utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 imeshatekelezwa kwa kiasi kikubwa na ahadi nyingi zilizoahidiwa zimeshatekelezwa sambamba na zile ambazo haziko katika Ilani.

Alisisitiza kuwa viongozi wote waliomo Serikalini ni vyema wakatambua kuwa wanatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha CCM, hivyo, wanakila sababu kufanya kazi zao kwa bidii na yule ambaye hatoweza anapaswa kukaa pembeni.

Aliongeza kwua huo ni utaratibu wa Serikali zote duniani kwa chama kinachoongoza Serikali  ni lazima viongozi wote watekeleze Ilani ya Chama hicho kwani ndicho kilicho madarakani na ndicho kinachoongoza nchi.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa huo ndio utaratibu wa kimataifa na demokrasia ya nchi hivyo viongozi wote waliomadarakani katika Serikali anayoiongoza hawana budi kutekeleza Ilani ya CCM kwani ndicho chama kilicho madarakani,

Alieleza kuwa ujenzi wa  barabara ya Mkanyageni- Kangani (Km 6.5) ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo imetajwa katika Ilani hiyo kwenye ukurasa wa 149.

Aidha, ujenzi wa jengo la skuli ya Sekondari Michenzani, Mkoani Pemba pia ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.

Ambapo pia, Rais Dk. Shein alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya CCM ya kujenga barabara ya Chake hadi Mkoani yenye (Km 27), ambayo hivi sasa imo katika mchakato wa michoro.

Rais Dk. Shein pia, aliusisitiza uongozi wa CCM wa Mkoa na Wilaya hiyo kuimarisha historia ya ASP kwa kulijenga jengo la Tawi la CCM lenye historia ya ASP huko Mkanyageni ambalo lilitumika na wazee waasisi kama vile marehemu mzee Mohamed Juma Pindua na yeye kuahidi kuchangia mabati kwa ajili ya ujenzi huo.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alizipongeza taarifa zilizotolewa mbele yake ikiwemo taarifa ya Serikali ya Wilaya ya Mkoani pamoja na taarifa ya Chama iliyotolewa na uongozi wa CCM Wilaya ya Mkoano.

Rais Dk. Shein pia, aliupongeza uongozi wa CCM Wilaya hiyo ya Mkoani kwa kuongeza idadi ya wanachama sambamba na ulipaji wa ada kwa wanachama wa chama hicho.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, na Mama Mwanamwema Shein, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, wakiwa katika moja ya madarasa ya Skuli hiyo ya Sekondari ya Michezani baada ya ufunguzi wake ,likiwa na meza na viti vipya vilivyoagizwa na Serikali kwa Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Michezani Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, akiwa katika ziara yake kutembelea Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
 NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Bi. Madina Mjaka, akitowa Taarifa ya Kitaalam ya ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi leo.(Picha na Ikulu)
 /WANAFUNZI wa Skuli ya Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. hayuko picha wakati wa hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Michezani leo, 21-2-2019.(Picha na Ikulu)

 WANANCHI wa Kijiji cha Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Michezani Pemba.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Michezo baada ya kumaliza kusoma Quran Surat Afaq Mwanafunzi Salim Shehe Hussein, kulia kwa Rais Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Viti na Meza Mpya vilivyoagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, tayari vimeshagawiwa kwa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba, kwa ajili ya matumizi ya Wanafunzi.(Picha na Ikulu)
 JENGO Jipya la Skuli ya Sekondari ya Michezani Kisiwani Pemba Wilaya ya Mkoani.(Picha na Ikulu)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA RUBAMBANGWE HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) mkoa wa Geita, Glagys Jeffta wanaoshuhudia ni maafisa uendelezaji biashara, Clara Lumbanga, Olivia Musanga Zoka na Phoibe Keu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani leo jioni.
Eneo lililopimwa la Rubambangwe linavyoonekana kwa picha ya Drone,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mtemi Simioni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani wakijadiliana jambo jioni ya leo baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja Chato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga.
 Mazungumzo yakiendelea baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na  na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akizungumza kutoa neno la shukurani katika uzinduzi huo kulia kwake ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni na kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani kwa mchango wake katika upimaji wa viwanja hivyo vilivyozinduliwa mauzo.


 Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
 Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni  akizunguma katika uzinduzi huo kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Philip Shoni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.

Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akizungumza katika hafla hiyo na kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani.


Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
 Wakifuatilia hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Wakiagana mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.


Halmashauri ya Wilaya ya Chato ikishirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) inautangazia umma juu ya uuzaji wa viwanja 1,035 vilivyopimwa na kuwekewa barabara katika eneo la Mlimani na Rubambangwe kata ya Muungano. Mauzo ya viwanja yanaanza wiki ijayo.

Wananchi wote mnakaribishwa kununua viwanja vyenye matumizi mbalimbali kama vile makazi, makazi na biashara, viwanja vya biashara, maeneo ya kumpumzikia, viwanja vya michezo na huduma mbalimbali za kijamii kama zahanati, Shule, Vituo vya Mafuta kwa bei ya kuanzia Tsh 1,300 kwa mita ya mraba.

Viwanja vipo mita chache kutoka katikati ya mji wa Chato. Vipo mkabala na barabara kuu iendayo Bukoba. Pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Viwanja vilivyopimwa na kupangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo:
1. Ujazo wa juu (High density)
2. Ujazo wa kati (Medium density)
 3. Ujazo wa chini (Low density) 

VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI

1. Makazi –Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,300/=
2. Makazi na biashara- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,700/=
3. Biashara (Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa)- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
4. Huduma za jamii (Zahanati, shule ya awali, sekondari) Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
5. Ibada/kuabudu- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=

UTARATIBU WA KUNUNUA KIWANJA

Chukua fomu ya maombi kutoka o­fisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato au Ofi­si ya NHC iliyo karibu nawe.
Lipia angalau asilimia 30 ya thamani ya kiwanja unachonunua na kiasi kinachobaki kilipwe ndani ya siku 90.
Malipo yote yafanyike kwenye akaunti ya benki ifuatayo: Jina la Akaunti : MRADI WA VIWANJA CHATO Nambari ya akaunti : 327 100 116 07 Benki: NMB Tawi la Chato
Rejesha fomu ya maombi uliyojaza kwa usahihi ukiambatanisha pamoja na vielelezo vinavyohitajika ikiwemo nakala ya malipo (deposit slip) kutoka benki.
Utapatiwa barua ya uthibitisho (Offer Letter) mara tu ombi lako litakapokubaliwa, pamoja na masharti ya kukamilisha malipo ya kiwanja unachochagua.
Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za Idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Au KAMBARAGE House, 1 Mtaa wa Ufukoni, Dar es Salaam, Tanzania. Kwa Mawasiliano piga namba  +255 282 228 007/ +255 754 444 333.

PHILIP SHONI
KWA NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
21/02/2019

KIJANA MWENYE ULEMAVU ATOA OMBI KWA RAIS MAGUFULI,WASANII BONGO MOVIE WAMTEMBELEA

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

KIJANA Khamis Salum mwenye ulemavu wa miguu awapongeza wasanii wa Bongomovie kwa kumtembelea na kumpatia baadhi ya mahitaji nyumbani kwake Yombo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Salum amesema ni faraja kubwa ameipata na hakutegemea kama wasanii wangeweza kumkumbuka na kumpelekea baadhi ya mahitaji kama vile mchele,magodoro pamoja na fedha.

Hata hivyo ameomba apatiwe msaada wa kitabibu kutokana na maumivu makali anayoyapata siku hadi siku na kumsababishia kushindwa kutimiza ndoto zake kama kijana .

"Naamini nitaweza kusimama tena naomba Rais wetu wa wanyonge Dk.John  Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  wasikie kilio changu kwani nateseka sana, ukizingatia mimi kiumri bado mdogo nahitaji kusoma na kutimiza malengo yangu," amesema Salum.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nitete Frola Rauo amesema Salum anahitaji kupendwa,kuthaminiwa na kutunzwa na watu wote kwani ni kijana mdogo sana na anahitaji msaada wa hali na mali.

Rauo amesema kupitia shirika la Nitetee ambalo lipo kwa ajili ya kusaidia watu waliweza kufanya mikakati ya kuhakikisha wanamtoa Salum pale Kariakoo na kumtafutia sehemu ya kuishi ambayo ni yombo kwa sasa

"Tulimpeleka  hospital kwa ajili ya vipimo mbalimbali na kugundua tatizo lake la miguu kuvimba linazidi kukua siku hadi siku tofauti na hapo awali," amesema Rauo

Hata hivyo kiongozi wa Msafara huo ambae ni Msanii wa Bongomovie Steven Mengere a.k.a Stive Nyerere amesema Salum ni watoto kama watoto wengine wanahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee kwa sasa kutokana na maradhi yanayomsumbua ya miguu kuwa mikubwa na kumlazimu kukaa ndani na kuwa tegemezi kwa kila kitu.

"Sisi wasanii tujitathimini na kulichukua jukumu la kumsaidia mtoto huyo kwa sasa na kuwahamasisha jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla kuhakikisha Khamis anasimama," amesema Steve Nyerere.

Pia ameeleza kuwa mahitaji madogo waliyompatia hayataishia hapo bali watarudi kujipanga upya na kuhakikisha wanampatia vitu vingine ikiwemo kumlipia chumba,fedha pamoja na vingine.
Kijana mwenye tatizo la miguu kujaa Khamis salum akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii baada ya kumtembelea anapoishi kwa sasa yombo jijini Dar es salaam.
Msanii wa Bongomovie Steven Nyerere akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii waliofika kumtembelea mtoto Khamis salum  na  kuwasilisha mahitaji yake  salum  jijini Dar es salaam


VODACOM YAZINDUA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Momba, Bw. Juma Ilando akizungumza baada ya uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania mjini Tunduma ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuwafikia wateja wake. Kulia kwake ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya nyanda za juu Kusini, Bw. MacFadyne Minja (mwenye shati nyeusi) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tunduma.
 Wanamuziki  wakiburudisha katika uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania mjini Tunduma, ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuwasogezea wateja wake huduma.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Bw. Juma Ilando akikata keki baada ya kuzindua duka la Vodacom Tanzania wilayani hapo ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuwafikia wateja wake. Kulia kwake ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya nyanda za juu Kusini, Bw. MacFadyne Minja (mwenye shati nyeusi) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tunduma. 


RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE WATOA POLE KWA FAMILIA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DKT. HAMIS KIGWANGALA ALIYEFIWA NA MTOTO WAKE. JIJINI DAR ES SALAAM LEO FEBRUARI 22, 2019

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo, Victoria Jijini Dar es salaam nyumbani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pole na Dkt. Bayoum Kigwangala ( Mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangala),  pamoja na Bi Hawa Mushi na Bi. Bagaile Bakari nyumbani kwa Waziri huyo Victoria Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Watoto Hk Junior ,Sheila na Hawa ambao ni watoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala alipoambata na mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole kwa Familia ya Waziri huyo nyumbani kwake Victoria Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Dua maalum na mkewe Mama Janeth Magufuli ,Dkt. Bayoum Kigwangala (Mke wa Dkt. Kigwangala), Hk Junior , Sheila, Hawa (Watoto wa Waziri Kigwangwala) pamoja na Bi Hawa Mushi na Bi. Bagaile Bakari nyumbani kwa Waziri huyo Victoria Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Mtoto wake aitwaye Zul Hamis Kigwangala Kilichotokea Februari 21,2019 katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Muhimbili)  Jijini Dar es Salaam

MAWAZIRI SABA WATEMBELEA MANYARA

$
0
0
MAWAZIRI saba wametembelea Kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa eneo hilo na hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero. Pia mawaziri hao wamesikiliza mgogoro wa ardhi wa kijiji cha Irkushbor cha wilayani Kiteto na hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero. 

Mwenyekiti wa mawaziri hao, William Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema wametumwa na Rais John Magufuli kusikiliza mgogoro huo. 

Waziri Lukuvi alisema baada ya kupokea mapendekezo ya namna ya kumaliza mgogoro huo kutoka pande zote watafikisha suala hilo kwa Rais Magufuli ili atoe maamuzi. 

Alisema wamepokea maoni kutoka kwa wananchi wa vijiji hivyo, viongozi wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya, wabunge, hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero. 

"Baada ya kupokea mapendekezo haya kwa njia ya maandishi na maoni ya mdomo tumeandika na tutayapeleka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri na kisha aliyetutuma atayatolea maamuzi," alisema Lukuvi. 

Mawaziri saba waliofika Simanjiro ni Lukuvi, Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima. 

Akizungumza mbele ya Mawaziri hao saba, Mnyeti alisema amekagua nyaraka zote zilizopo kwenye mkoa huo lakini hajakuta sehemu inatamkwa kuwa pori la akiba la Mkungunero lipo Manyara. 

Mnyeti alisema baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro na Irkushbor wilayani Kiteto wanafukuzwa mara kwa mara na wakanyang'anywa mifugo yao zaidi ya 600. 

Mbunge wa jimbo la Simanjiro, James Ole Millya alisema wananchi hao wamenyanyasika vya kutosha kwani kila wakati wanafukuzwa na kuambiwa wapo hifadhini. 

Ole Millya alisema ni wakati sahihi wa kuweka mpaka ili ijulikane mwisho wa wafugaji hao na hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero, kuliko mpaka wao kusogezwa kila wakati. 

"Kwa sababu mmekuja na helkopta mnaweza kupita juu na kuona mifugo yetu ng'ombe na mbuzi zinachungwa pamoja na wanyamapori wakiwemo tembo, pumbamilia, swala na nyumbu sisi wamasai ni wahifadhi wazuri," alisema Ole Millya. 

Diwani wa kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga (Mardad) alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuwajali na kuwatetea wafugaji na wakulima nchini. 

Mardad alisema hivi sasa wafugaji na wakulima wa eneo hilo wanalishia mifugo yao na kulima sehemu ambazo walikuwa wanazitumia miaka iliyopita kabla ya kuondolewa kwa kudaiwa wapo sehemu ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara baada ya kufika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza mbele ya Mawaziri saba waliofika kusikiliza mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa Vijiji vya Kimotorok Wilayani Simanjiro na Irkushbor Wilayani Kiteto na hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akizungumza huku amefunga shuka ya kimasai juu ya manyanyaso waliopata wananchi wa Kijiji cha Kimotorok kutokana na mgogoro wa ardhi na hifadhi.

MABULA AKUTANA NA JENERALI MUSUGURI

$
0
0
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Msuguri, nyumbani kwake katika Kitongoji cha Kitanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.

Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amekutana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Msuguri, nyumbani kwake katika Kitongoji cha Kitanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Jenerali Msuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya mwaka 1980 hadi 1988 wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Serikali ya Awamu ya Pili ya Mhe. Ali Hassan Mwinyi.

Jenerali Msuguri alikuwa mstari wa mbele katika kupigana vita dhidi ya Nduli Idd Amin ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilivyopigana kuukomboa Mkoa wa Kagera wakati Iddi Amin alipovamia Novemba 1978.

Jenerali Msuguri ndio mwanzilishi wa eneo maarufu lililopo jiji Dar es salaam lijulikanalo kama Mbezi kwa Musuguri, ambapo aliishi wakati akiwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania.

Dkt. Mabula amekutana na Jenerali Msuguri wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara ambapo katika maongezi yao Jenerali Msuguri alimgusia kuhusiana na uvamizi unaosemekana umefanywa na wakazi wanaozunguka eneo lake lililopo Kimara Temboni, jijini Dar es salaam lenye Hati namba 231.

Katika eneo hilo lenye ekari 17 Jenerali Msuguri amemueleza Dkt. Mabula kwamba inasemekana tayari ekari 3 zimeishavamiwa na baadhi ya wakazi ambao wanalima na baadhi wamejenga makazi yao huku wakigoma kutoka kwa kutumia nguvu.

Miongoni mwa watoto wa Jenerali Msuguri Bi. Felista Musuguri alimueleza Dkt. Mabula kwamba walifanya jitihada za kuwaondoa watu wanaosemekana ni wavamizi lakini walikimbizwa na mapanga hivyo wanaogopa isije ikatokea machafuko.

Kwa sasa Jenerali Msuguri yupo nyumbani kwake katika Kitongoji cha Kitanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara jirani kabisa na Kijiji cha Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo.

Akiwa Wilaya ya Butiama Dkt. Mabula alifika katika Kijiji cha Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo na kuzuru Kabuli la marehemu Julius Nyerere, Mkoa wa Mara.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Musuguri (katikati) akimuonesha wanafamilia wake Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi na wanafamilia wengine.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Musuguri (nguo nyeupe katikati) akiwa na wanafamilia wake, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi na wanafamilia wengine.
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akisali katika kabuli la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo Mkoa wa Mara wakati alipofika kuzuru Kabuli hilo.
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwasha mshumaa katika kabuli la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo Mkoa wa Mara wakati alipofika kuzuru Kabuli hilo.
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwa Nyumbani kwa Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo Mkoa wa Mara, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.

ZANTELI YAENDELEA KUMWAGA ZAWADI KUPITIA PROMSHENI YAO YA 'TUMIA EZYPESA USHINDE'

$
0
0
Meneja wa mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa, amesema kuwa promosheni hii itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu na hadi kufikia sasa zimefanyika droo mbili ambazo zimewezesha wateja 60 kujishindia simu za SmartPhone pia kutakuwepo na droo ya mwezi ambayo itawezesha wateja kujishindia fedha taslimu kati ya shilingi 200,000/-mpaka shilingi 1,000,000/-na wateja wapya wanapatiwa motisha. Meneja wa Zantel kitengo cha Bidhaa EZYPESA Leonard Kameta (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya na washindi waliopokea zawadi zao za simu za kisasa za mkononi (SmartPhones). Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zantel, Sakyi Opuku akimkabidhi zawadi ya simu mmoja wa washindi wa promosheni ya tumia EzyPesa ushinde, Rehema Ali Rashid wa Mombasa Unguja, hafla iliyofanyika katika ofisi za Zantel Vuga mjini Unguja. Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zantel, Sakyi Opuku akimkabidhi zawadi ya simu mmoja wa washindi mshindi wa shindano la tumia Ezypesa ushinde kutoka Zanzibar katika hafla iliyofanyika Zanzibar.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Zantel Tanzania, Rukia Mtingwa akimkabidhi mmoja ya washindi zawadi ya simu ya kisasa ya mkononi (SmartPhones). Pembeni kushoto anayeshuhudia ni Meneja wa Zantel kitengo cha Bidhaa EZYPESA Leonard Kimeta. Meneja wa Zantel kitengo cha Bidhaa EZYPESA (kulia) Leonard Kimeta akimkabidhi zawadi  mmoja ya washindi zawadi ya simu ya kisasa ya mkononi (SmartPhones). Pembeni kulia anayeshuhudua ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Zantel Tanzania, Rukia Mtingwa.

BREAKING NYUZZZZZ.....KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUCHOMA KITUO CHA POLISI BUNJU A JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu kifungo cha maisha watuhumiwa nane (8) kati ya 18 waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma za kuchoma moto kituo cha polisi Bunju A jijini Dar es Salaam.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS YALETA NEEMA MANONGA

$
0
0
*Gulamali akabidhi gari la kubebea wagonjwa tarafa ya Simbo, ahaidi kusimamia sekta ya afya, elimu na miundombinu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora na kutembelea Wilaya zote saba (7) za  Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora .

Katika  wilaya Igunga Makamu wa Rais alipokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa iliyowasilishwa na mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, na kukagua maendeleo ya ujenzi wa tanki kubwa la maji ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mradi wa maji wa shilingi bilioni 600 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 58.

Pia Makamu wa Rais alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Simbo ambapo alipanda mti wa kumbukumbu na kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Simbo katika jimbo la Manonga  Makamu wa Rais amesema kuwa, Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha maji ya kutosha yanapatikana ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa uhuru na ufanisi zaidi. Pia amempongeza Mbunge wa jimbo hilo Seif Gulamali kwa juhudi zake za kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu hasa za afya, elimu pamoja na miundombinu.

Kuhusiana na suala la afya Wilayani humo imeelezwa kuwa, Wilaya hiyo ina Vituo 66 vya afya kati ya hivyo 55 vinamilikiwa na Serikali, huku vituo vingi zaidi vikizidi kujenga na kufanyiwa ukarabati.

Makamu wa Rais amehimiza Elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya umuhimu wa bima ya afya ambapo Serikali inaandaa na mpango wa bima kwa wote na kuwataka wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na kuhakikisha vitambulisho vya wajasiriamali vinatolewa kwa waliokidhi sifa na vigezo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Manonga Seif Gulamali amekabidhi gari ya kubebea wagonjwa katika tarafa ya Simbo ikiwa ni moja ya utekelezaji ahadi yake ya kuhakikisha huduma za afya, elimu na maji ni muhimu na lazima jimboni humo.

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka jana Gulamali alitembelea kituo hicho cha Simbo  pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati na kuahidi kuboresha zaidi sekta ya afya hasa kwa kujenga nyumba za wauguzi, maabara, vyumba vya kuhifadhia maiti na vyumba vya upasuaji katika hospitali jimboni humo.

Na amewata wananchi wa Manonga kutumia fursa zinazotolewa na Serikali hasa katika elimu pamoja na fursa iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa wajasiriamali kwa kutoa vitambulisho vitakavyowasaidia kufanya biashara zao bila bughudhi

Katika ziara yake Mkoani Tabora Makamu wa Rais aliambatana na Waziri wa Madini Doto Biteko, Naibu Waziri Maji  Juma Aweso, Naibu Waziri Ujenzi  Elias Kwandikwa na Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cha jimbo la Manonga kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Seif Gulamali wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano Simbo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Gari la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa kwa wananchi ya tarafa ya Simbo na Mbunge wa Jimbo la Manonga, Kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Seif Gulamali na kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara. 


WAZIRI MKUU ASHUHUDIA MWAFUNZI ASIYE NA MIKONO AKIANDIKA KWA KUTUMIA VIDOLE VYA MGUU

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia  wakati mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive, Joseph Mtei ambaye hana mikono, alipokuwa akiandika kwa kutumia  vidole vya mguu   baada ya Waziri Mkuu kuzindua Shule hiyo, Februari 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwa kutumia vidole vya mguu na  Joseph Mtei ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika  Shule ya Sekondari ya ST.  Pamchius  Inclusive ya wilayani Hai,  Februari 22, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mgwira na wa pili kushoto  ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Shule ya Sekondari ya  St. Pamachiwa  Inclusive wilayani Hai, Februari 22, 2019. Kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Isaac Amani na wa pili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AFISA TAWALA WA WILAYA YA KISARAWE APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA RUSHWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani imemfikisha Mahakamani John Mwendamaka, Afisa Tawala Wilaya ya Kisarawe kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi milioni mbili (TZS 2,000,000/=) kinyume ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

John Mwendamaka alifunguliwa kesi ya Jinai Namba 22 ya mwaka 2019 akiwa Afisa Tawala katika ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kisarawe Devotha Kisoka, Mwendesha Mashtaka kutoka TAKUKURU, Naftali Mnzava ameieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa ya kiasi cha shilingi milioni mbili (TZS2,000,000/=) kutoka kwa mtoa taarifa ili aweze kumsaidia mdogo wake kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, jambo ambalo ni kosa kisheria kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

Mnzava ameieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alipokea rushwa ya kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mbili (TZS 2,000,000/=) kutoka kwa mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

Mshtakiwa amekana makosa yote mawili na dhamana ilikuwa wazi, hivyo mshatakiwa amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hii itakuja kwa ajili ya hoja za awali tarehe 05/03/2019.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Bi Suzana Raymond amewaasa wananchi wote kufuata taratibu kanuni na Sheria za nchi ili kuweza kwenda na kasi ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Mh Dr.John Pombe Magufuli. 

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CCM WILAYA YA MKOANI PEMBA AKIWA KATIKA ZIARA YAKE

$
0
0


  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. akiwahutubia Viongozi wa CCM na wa Serikali wa Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Wilaya hiyo.(Picha na Ikulu)
WAZEE wac Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mkoani Pemba wakifuatilia hutuba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Mkoani Pemba na kuzungumza na Viongozi  wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mkoani, katika ukumbi wa Skuli ya Mohammed Juma Pindua Mkoani.(Picha na Ikulu) 
 KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mkoani Pemba Ndg. Mohammed  Ali, akiwasilisha ripoti ya Kazi za Chama za Wilaya ya Mkoani Pemba wakati wa mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wakev na Viongozi hao, uliofanyika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkoani Pemba.(Picha na Ikulu) 

 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mkoani Pemba Ndg. Ali Juma Nassor, akitowa salamu za Wanachama wa CCM Wilaya ya Mkoani wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa katika ziara yake kisiwani Pemba, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkoani.(Picha na Ikulu)
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg.Dr.Abdallah Juma Mabodi, akizungumza na Wanachama wa CCM Wilaya ya Mkoani Pemba, wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kisiwani Pemba mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkoani.(Picha na Ikulu)

 BAADHI ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani.(Picha na Ikulu)

Tanzania imeingia orodha ya 27 Duniani katika ubunifu - HDIF

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
KUTOKANA na maendeleo ya uvumbuzi nchini, Tanzania imeshika nafasi ya 27 katika orodha ya ubunifu duniani kutoka nafasi ya 123 mwaka 2013 hadi 92 mwaka huu. Sababu zilizochangia Tanzania kufikia hatua hiyo ni kuanzishwa kwa vituo vipya vya teknolojia, ongezeko la ufahamu juu ya uwezo wa ubunifu katika kutatua changamoto kubwa za kimaendeleo.

Hayo yalibainishwa leo Februari 22, 2019 jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa  Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Binadamu (HDIF), David McGinty wakati wa uzinduzi wa ripoti  inayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018'.
McGinty amesema kuwa zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, wamesaidia wavumbuzi wengi nchini ili kutekeleza mawazo yao kwa ufanisi na kuwapa mbinu mpya za kutimiza malengo. Amesema kuwa HDIF imekuwa bingwa wa kuvumbua vipaji vya baadhi ya Watanzania wenye ubunifu mkubwa na mashirika ambao wamewekeza nguvu na rasilimali nyingi kushughulikia changamoto za maendeleo nchini.

"Ingawa Tanzania mazingira ya kukuza ubunifu bado yako katika hatua za awali, taasisi zinazoshughulika na ubunifu, zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uchache wa rasilimali na vipaumbele katika mashindano," amesema McGinty. Amesema ripoti hiyo inalenga kuleta kichocheo cha mabadiliko kwa kuongeza ujuzi na ufahamu kuhusu ubunifu katika jamii, pia kuongeza ufahamu wa HDIF juu ya  kuboresha matumizi, viwango, uchukuzi wa ubunifu nchini.

"Ili kuendeleza upatikanaji wa huduma za msingi na kuimarisha mazingira ya ubunifu nchini. HDIF tunaomba mashirika mengine kutafakari njia zinazoweza kutumikia kusaidia kuchochea uvumbuzi ambao utaleta kabadiliko halisi na ya kudumu," alisisitiza.

McGinty ameeleza kuwa katika miaka mitano ya utekelezaji wa mfuko huo, wamekutana na changamoto mbalimbali zilizosababisha mikakati iliyopangwa kutofanikiwa kwa ufanisi na kwamba HDIF inatarajia kubadilishana uzoefu na washirika wengine katika kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumiwa kwa ufanisi na kuchagua njia bora.

Kwa upande wake,  Naibu Kiongozi wa HDIF, Joseph Manirakiza   amesema fursa ya kuinua masuala ya ubunifu Tanzania yamesaidia kuvutia baadhi ya wafadhili wa kimataifa na wawekezaji.
Amesema HDIF inahamasisha ushirikiano kati ya wadau katika kuongeza kubadilishana taarifa ya mambo waliyojifunza ikiwemo changamoto.

"HDIF inatarajia kukamilisha kazi yake mwaka 2021 lakini kwa wakati wote miradi itaendelea kuwa kielelezo cha ubunifu nchini," amesema Manirakiza. Ameongeza kuwa  katika miradi mbalimbali ambayo waliifadhili imeleta matokeo chanya ikiwemo  mradi wa maji unaotumia mfumo wa malipo kabla uliopo Karatu mkoani Arusha.

Ameeleza kuwa mafanikio waliyoyapata yanayotakana na ushirikiano wa wadau wa masuala ya ubunifu ikiwemo Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), vyuo vikuu  na wanafunzi.
 Kiongozi wa mfuko wa Ubunifu na Maendeleo (HDIF)  David McGinty akizungumza na wanahanabri pamoja na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari wakati wa uzinduzi wa kupitia nanayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018', uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 Naibu Kiongozi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya watu (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumzia miradi waliyoitekeleza kwa miaka mitano (mwenye shati la mistari). Wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo,jijini Dar es Salaam
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya watu (HDIF), Hannah Mwandoloma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti  inanayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018', uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 Mchora Vobonzo Masoud Ally 'Kipanya' akiongoza mjadala kuhusu mchango wa waandishi wa habari katika masuala ya ubunifu baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo, jijini Dar es Salaam. Pombeni yake ni  baadhi wa wahariri kutoka vyombo vya habari. 

 Baadhi ya wadau wa habari wakichangia mada wakati wa uzinduzi wa kupitia nanayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018', uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 


Serikali imejidhatiti katika kuondoa changamoto zs kibiashara- TPSF

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema kuwa kumekuwa na ushirikiano na Sekta ya Umma katika kwenda katika soko ikiwa ni kuondoa changamoto zilizokuwa zinawakabili sekta hiyo.
Akizungumza na waandishi habari Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geofrey Simbeye amesema serikali imekuwa na utayari wa kukutana na kujadiliana na sekta binafsi kwa kuonyesha nia madhubuti ya kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini.

Amesema spidi ya serikali ya awamu tano ya Rais Dk. John Magufuli nchi itafikia soko kwa kuongeza Kampuni hadi kufikia milioni moja. Simbeye amesema kuwa mkutano waliokuwa waufanye jijini Dar es Salaam wameiahirisha kutokana na washiriki kuwa wengi na kuamua kufanya katika kanda kwa nchi nzima.

Aidha amesema miundombinu mbalimbali inayojengwa watautumia ni sekta binafsi katika kurahisisha mazingira ya kufanya biashara. Amesema sekta binafsi inazidi kuimarika kutokana na mazungumzo ya mara kwa mara na serikali ikiwa ni kuondoa vikwazo vya kibiashara  na serikali imekuwa na uwazi katika kufanya utatuzi wa vikwazo hivyo.

Simbeye amesema kufanya majukwaa katika kanda ni kuweka uwigo mpana wa kila mdau kushiriki kuliko ingefanyika sehemu moja ambayo kwa idadi ya isingetosha. "Serikali imedhamiria kushirikana na TPSF na mafanikio yameanza kuonekana na sio kukosoa kila kitu ina haki ya kupongezwa"amesema Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Geofrey Simbeye akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mwitikio wa serikali katika utatuzi wa changamoto za biashara pamoja na mkutano uliotakiwa kufanyika Dar es Salaam sasa kufanyika katika kanda zote nchini
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images