Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

JAFO AMUAGIZA MKANDARASI KUBOMOA SAKAFU ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amemuagiza mkandarasi anayekarabati shule kongwe ya sekondari ya Malangali iliyopo wilayani Mufindi mkoani Iringa kubomoa Sakafu iliyowekwa kwenye madarasani kutokana na kuwa chini ya kiwango.

Hali hiyo imetokea leo wakati Waziri Jafo alipokuwa mkoani Iringa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefika katika shule hiyo na kukagua moja ya darasa ambalo tayari lilikuwa limekamilika na kubaini kuwa sakafu yake imewekwa chini ya kiwango baada ya kugonga gonga kwa viatu na kutokea nyufa. Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemuagiza Mkandarasi huyo kubomoa sakafu hiyo na kuanza kazi upya.

Jafo ameoneshwa kukerwa na hali hiyo na kuagiza msimamizi wa kazi hiyo ambaye ni Wakala wa Majengo nchini(TBA) kuhakikisha sakafu hiyo inavunjwa na kujengwa upya katika ubora unaotakiwa.Shule ya Malangali ni miongoni mwa shule kongwe 89 ambazo serikali imeamua kuzikarabati upya ili zirudi katika ubora wake.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kwa usimamizi mzuri wa ukarabati kituo cha afya Malangali ambapo majengo yake yamejengwa kwa ubora wa hali ya juu. 

Aidha, Jafo ameitembelea hospitali ya Frelimo iliyopo Manispaa ya Iringa na kujionea changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara bungeni na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ritta Kabati.

Kutokana na changamoto hizo, Jafo amesema hospitali hiyo inapaswa kupewa kipaumbele kwa upande wa majengo ya Wodi pamoja na jengo la uchunguzi ili iweze kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa vyumba vya madarasa katika sekondari kongwe ya Malangali ambapo ameagiza sakafu kufumuliwa kutokana na kutokuwa na ubora.
Viongozi wakifanya Ukaguzi wa miundombinu inayojengwa katika kituo cha afya Malangali
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo na Mbunge wa Viti Maalum Ritta kabati walipo watembelea akina mama waliojifungua katika hospitali ya Frelimo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza, Mbunge Ritta Kabati pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Frelimo


WANACHAMA WA YANGA KWA KAULI MOJA WAKUBALI MABADILIKO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Wanachama wa Yanga kwa kauli moja wamfikia hatua ya makubaliano kwenda katika mfumo wa mabadiliko ambao utaruhusu timu hiyo kuwa Kampuni.

Yanga iliyofanya mkutano wake leo Jijini Dar Es Salaam, ulianza kwa hotuba ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na kuwaasa wanachama wa Yanga wafanye maamuzi sahihi ili kuweza kuiweka timu yao katika dira nzuri.

Dkt Mwakyembe amesema kuwa Yanga ni alama ya ukumbusho barani Afrika kama klabu iliyoweza kusaidia upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika na bara la Afrika.

"Yanga imechaguliwa kuwa alama ya ukumbusho barani Afrika kama moja ya vilabu vilivyobeba alama ya uhuru wa Tanganyika na uhuru wa bara la Afrika, Yanga ni klabu kubwa na yenye historia yake ndania ya nchi hii , "amesema Dkt Mwakyembe.

Dkt Mwakyembe amesema uwekezaji katika klabu za mpira ni jambo lisilokwepeka na hata serikali inaunga mkono suala hilo kulingana na mahitaji yanayohitajika ili kuwa na soka la ushindani.Pia amesema wanachama waacheni kuichukulia mzaha mzaha tu na kufikia inafungwa mpaka na timu ndogo ila maamuzi yao ndiyo yatakayoamua mustakabali wa timu ya Yanga.

Pia katika mkutano huo wanachama waliweza kupinga barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wao Yusuf Manji na kusema kuwa bado wanamtambua kama mwenyekiti mpaka sasa hivi.Wanachama hao wamesema kuwa hawawezi kukubaliana na baria hiyo na wamemuomba arejee katika nafasi yake ya Uenyekiti wa klabu yao ambapo wka kipindi cha mwaka mmoja imekua imekaimiwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga.

Ikumbukwe kuwa Mwaka 2017, Manji aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake katika klabu ya Yanga ila ndani ya mwaka mzima Yanga haikuwahi kuweka mkutano wa wanachama ili kuweza kuijadili barua hiyo.Baada ya kupinga suala la kujiuzulu Manji anarejea Yanga akiwa mwenyekiti huku akisaidiwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga.

TAARIFA KWA UMMA.

USAID YAPONGEZA MCHANGO WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF KATIKA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI.

$
0
0
Na. Estom Sanga-TASAF 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa -USAID, Andy Karas amefanya ziara katika mkoa wa Kagera na kukagua shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF na kuridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

Akiwa katika kijiji cha Mishenyi kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba Vijijini ,Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID alitembelea Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambako alijionea namna Walengwa hao walivyoboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora kwa kutumia ruzuku itolewayo na TASAF .

Aidha Karas alipata ushuhuda wa Walengwa namna wanavyotumia ruzuku hiyo katika kuboresha huduma za elimu na afya kwa kaya zao huku pia wakitilia mkazo suala la uanzishwaji wa miradi midogo midogo ya uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato chao.

“huu ni mwelekeo sahihi na unaopaswa kuungwa mkono na wapenda maendeleo kama USAID kwani unatekelezwa kwa misingi endelevu” alisisitiza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID alikagua miradi na bidhaa mbalimbali inayotekelezwa na Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mishenyi kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao. Miongoni mwa bidhaa hizo ni mbuzi, kuku,vikapu, mayai,vikapu na Mikungu ya ndizi.

Nao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho cha Mishenyi waliipongeza serikali kwa kubuni Mpango huo kupitia TASAF ambao wamesema umesaidia kurejesha utu wao kwani hapo awali waliishi katika hali ya ufukara na sasa wanaona nuru ikiwarejea kwa kuanza kumiliki mali na kumudu kuendesha maisha yao kaya zao.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF,Amadeus Kamagenge,aliwahakikishia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kote kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii imeweka mkakati madhubuti wa kuwashirikisha walengwa katika kupunguza umaskini huku mkazo ukiwa ni kwa wao kufanya kazi za uzalishaji mali.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID  Andy Karas (wanne kulia )katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa miradi wa TASAF Amadeus Kamagenge (wa pili kulia )nje ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kutumia fedha za Mpango huo  katika kijiji cha Mishenye kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera. 

 Mkurugenzi  Mkazi wa USAID  Andy Karas  na Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Amadeus Kamagenge wakiangalia bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mishenye kata ya Butelankuzi halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.

 Mkurugenzi  Mkazi wa USAID  Andy Karas (aliyeshika daftari) akiangalia bidhaa zilizotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF  katika kijiji cha Mishenyi  kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato na kupambana na umaskini..

 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa ,USAID, Andy Karas akikagua moja ya mabanda ya kufugia mbuzi lililoanzishwa na mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, katika kijiji cha Mishenyi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Hapa ni mwendo wa zawadi tu, Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Mishenye kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wakimpatia zawadi mgeni wao Mkurugenzi Mkazi wa USAID baada ya kuzungumza nao na kuwatia moyo wa kufanya kazi ili waweze kuondokana na umaskini.

MANISPAA YA ILALA MABINGWA WA JUMLA UMITASHUMTA

$
0
0
Na Heri Shaaban 

MANISPAA ya Ilala wameibuka mabingwa wa jumla katika michezo yote ya mashindano ya umoja wa Shule za Msingi Umitashumta Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya pili Wilaya ya Kinondoni na nafasi ya tatu Temeke. 

Akizungumza  Dar es salaam jana, Ofisa Michezo mkoa wa Dar es Salaam Hadoph Ally amesema wameunda kikosi cha mkoa chenye wachezaji 120 ambao watakwenda Mwanza kushiriki ngazi ya Taifa.

"Mashindano ya umitashumta ngazi ya mkoa yalishirikisha timu za wilaya tano Ilala, Temeke, Ubungo, Kinondoni na Kigamboni  ambapo bingwa amepatikana katika mashindano hayo na tumeunda wachezaji 120 ambao wanasafiri kwenda kushiriki ngazi ya Taifa wakiambatana na viongozi wao 20 jumla  140,"amesema.

Kwa upande wake Ofisa Elimu Ilala  Elizabeth Thomas amepongeza ushindi wa jumla katika wilaya yake.Amesema Ilala ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo imekuwa ikifanya vizuri Mashindano hayo na mwaka huu timu kutoka kutoka Dar es Salaam itarejea na vikombe vyote ngazi ya Taifa.

Amesema kamati ya Ilala iliwaanda vizuri wachezaji wao ndio siri ya mafanikio ya ushindi mnono .Amesema mazingira ya timu ya Ilala yalikuwa mazuri ndio yamewafanya  Kufanya washinde.
OFISA ELIMU MSINGI MANISPAA ya ILALA Elizabeth Thomas (kushoto) akikabidhiwa kombe LA ushindi wa jumla mkoa Dar es Salaam ambapo ILALA wameibuka mabingwa na OFISA ELIMU Taaluma mkoa wa Dar es Salaam Janeth Nsunza Jana, katika ufungaji WA mashindano ya Umoja  wa Shule za Msingi(UMITASHUMTA)wengine Mratibu wa Umitashumta ILALA Hamis Ngoda (PICHA NA HERI SHAABAN)

KIFO CHA SAM WA UKWELI NI PIGO KUBWA KWANGU- RIDHIWANI KIKWETE

$
0
0
Na Shushu Joel, Chalinze 
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze  mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na msiba wa msanii wa Bongo fleva Sam wa Ukweli aliyefariki dunia siku za karibuni.

Akizungumza mara baada ya mzishi ya msanii huyo yaliyofanyika wilayani Bagamoyo Ridhiwani alisema kifo cha Sam wa Ukweli kwake ni pigo kubwa  kwani alikuwa akimtumia katika mikutano yake kama mwamasishaji wa watu kujitokeza kwa wingi kupitia nyimbo zake.

"Nimesononeshwa na msiba huu , nimpoteza mtu muhimu sana lakini sina jinsi, kilichobaki ni kumuombea dua tu ili apumzike kwa amani huko aendako,"amesema Ridhiwani.
Aidha amewataka wasanii na watanzania kuonesha umoja,upendo na mshikamano kama ndugu wa baba na mama mmoja ili kusaidiana.

Kwa upande wa moja ya wazee maarufu katika jimbo la Chalinze Abudalla Mzimba amewashukuru wote waliojitokeza katika mazishi ya kijana na msanii aliyekuwa mfano wa kuigwa katika CCM.

Amefafanua muda mwingi alikuwa akifanya kazi ya kuwahamasisha watu kusogea kwenye mikutano ili kusikiliza kile kilichokusudiwa kusemwa na viongozi wetu wa kisiasa.

Pia ameongeza kuwa kifo cha msanii huyo ni fundisho kwa vijana waliobaki kwa kutokusema ukweli magonjwa yanayowasumbua bila kwenda kutafuta tiba katika sehemu husika .

Mazishi ya Sam wa Ukweli yamehudhuliwa pia na Rais msataafu Dk. Jakaya kikwete.
 Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na wasanii wa bongo fleva katika dua ya kumuombea msanii wa bongo fleva alifariki jana na kuzikwa wilayani Bagamoyo.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazishi ya msanii sam wa ukweli.
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Kikwete kwenye mazishi ya msanii Sam wa ukweli wilayani Bagamoyo.
Rais msaatafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza waombolezaji katika msiba wa msanii wa bongo fleva Sam wa ukweli.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAKAMISHNA WA MAGEREZA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza kikao kazi cha Makamishna na Manaibu Kamishna wa Magereza Ofsini kwake leo Jumatatu 11, 2018 jijini Dar es Salaam. Jumla ya Maafisa 9 wa ngazi ya juu ya Jeshi la Magereza wamepandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kujaza nafasi mbalimbali zilizokuwa wazi ndani ya Jeshi hilo.
 Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa kwanza kulia) akiwa na Makamishna wapya wa Jeshi hilo wakifuatilia kwa makini kikao kazi kilichoongozwa chini ya Uenyekiti wa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani), leo Jumatatu 11, 2018, Jijini Da es Salaam.
Manaibu Kamishna wapya wa Magereza waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Mhe. Rais Magufuli wakifuatilia kikao kazi kilichoongozwa chini ya Uenyekiti wa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini.
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

RAIS DK.SHEIN AFUTARISHA MKOA KASKAZINI UNGUJA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuika na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Swala ya Magharibi jana iliyoswalishwa na Sheikh Shaibu Kadir Khamis,kabla ya futari aliyowaandalia Wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini "A".
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali katika Futari aliyoiandaa kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkokotoni,Wilaya ya Kaskazini "A".
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na Viongozi Wanawake katika Futari iliyoaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja  kwa ajili ya Wananchi wa Mkoa huo jana,(kulia) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Sira ubwa Mamboya na Mwakilishi wa nafasi za Wanawake Mhe,Panya.
  Baadhi ya Akinamama wa Shehia mbali mbali za Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwa katika Futari iliyoaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkokotoni,Wilaya ya kaskazini"A" Unguyja jana.
 Baadhi ya Wananchi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwa katika Futari iliyoaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkokotoni,Wilaya ya kaskazini"A" Unguyja jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed wakiitikia dua iliyoombwa baada ya futari aliyowaandalia \wananchi wa Mkoa huo jana  katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkokotoni,Wilaya ya kaskazini"A" Unguyja jana (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kher(kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Bw.Iddi Ali Ameir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiagana na Viongozi na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika futari  aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja jana katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini'A" Unguja.(Picha na Ikulu)

MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib azikwa Bagamoyo

$
0
0
 MWENYEKITI wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib (67) amezikwa jana jumapili kwenye makaburi ya Mwanakerenge mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 Katika mazishi hayo yaliyowakusanya wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari familia ya marehemu iliwaomba waombolezaji waendeleze mshikamano aliouacha marehemu Taalib.

Kaimu Mwenyekiti wa SHIWATA, Deo Kway alisema wataendeleza juhudi za marehemu kuwaunganisha wasanii na wanamichezo kujikomboa kiuchumi.
Kway alisema wakati wa uhai wake marehemu Taalib aliwaunganisha wasanii mbalimbali na kuunda SHIWATA ambayo imefanikiwa kujenga kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga na kumiliki shamba la ekari 500 kwenye kijiji cha Ngarambe mkoa wa Pwani.
 Marehemu Taalib alianza kuugua ugonjwa wa moyo kutoka mwaka jana na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha JK na baadaye kuruhusiwa na kuendelea kupata matibabu kila wiki.

Marehemu Taalib atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na juhudi zake za kuunganisha wasanii wa fani zote pamoja na kuwahimiza kuweka maslahi yao mbele ambapo alihamasisha ujenzi wa nyumba kwenye kijiji maalumu cha wasanii mkoa wa Pwani.
 Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib jana jumapili kwenye makaburi ya Mwanakerenge mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib jana jumapili kwenye makaburi ya Mwanakerenge mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib katika mojawapo ya mikutano ta chama chake enzi za uhai wake.

Waziri Kalemani aitaka Tanesco kukamilisha ukarabati wa miundombinu kabla ya Juni 30

$
0
0
Na Greyson Mwase, Kagera
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha linakamilisha kazi  ya ukarabati wa miundombinu yote ya umeme nchi nzima kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Dkt. Kalemani ameyasema  hayo leo tarehe 10 Juni, 2018 alipokuwa akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwenye ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) na ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji cha Rusumo  kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 80 baada ya kukamilika Februari, 2020.
Alisema kuwa, kwa sasa nchi ina nishati ya  umeme wa uhakika mbali na  kuwepo kwa changamoto ya kukatika kwa umeme inayotokana na uchakavu wa miundombinu ya kusafirisha umeme.
“ Tulikubaliana na uongozi wa TANESCO kuhakikisha kazi ya ukarabati wa miundombinu ya umeme nchi nzima, inakamilika ndani ya miezi mitatu yaani hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili wananchi waanze kupata nishati ya umeme wa uhakika,” alisema Waziri Kalemani.
Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani alimtaka mkandarasi anayefanya kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika mkoa wa Kagera kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu, kampuni ya Nakuroi Investment Company Limited kuongeza kasi ya usambazaji katika mkoa wa Kagera ili mradi uweze kukamilika kwa wakati na wananchi kupata umeme wa uhakika.
Aidha, alizitaka taasisi za umma kama vile mashule, vituo vya afya na halmashauri kutenga fedha kwa ajili utandazaji wa nyaya za mifumo ya  umeme (wiring) katika majengo yao ili waweze kuunganishiwa umeme mapema wakati wa utekelezaji wa mradi.
Wakati huohuo, Dkt. Kalemani aliitaka Serikali ya Mkoa  na Wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda ili iwe rahisi kuwekewa miundombinu ya umeme wakati wa utekelezaji wa miradi.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji umeme katika kijiji cha Kyerwa kilichopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali Mstaafu Shabani Lissu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akibonyeza kitufe kuashiria uwashaji umeme katika kijiji cha Kyerwa kilichopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kyerwa kilichopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
 Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na mkandarasi kutoka kampuni ya Nakuroi Investment Company Limited wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani)
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Katanda kilichopo wilayani Karagwe wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuwapunguzia gharama za ujenzi wa Mtaro wa Maji ya Mvua Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko waliojitolea kuanzisha Mradi huo kwa lengo la kujiepusha na Mafuriko yanayosababishwa na mkusanyiko wa maji mengi yanayoleta maafa wakati wa mvua za Masika.

Kauli hiyo imetolewa na Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Wananchi wa Bubujiko mara baada ya ziara fupi ya kukagua hatua za ujenzi wa Mtaro huo uliosimamiwa na Wananchi wenyewe na kuungwa mkono na Uongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na washirika wa maendeleo.

Balozi Seif Ali Iddi alisema  kitendo cha Wananchi wa Bubujiko kujenga Mtaro huo kimekuja mara baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein kutoa kauli ya Serikali ya ujenzi wa Mtaro huo ambacho kinapaswa kupongezwa.

Alisema Serikali Kuu itaangalia namna ya kusaidia hatua iliyobaki ya kukamilika kwa ujenzi wa Mtaro huo uliobakia Mita 65 zinazotarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Milioni 30,000,000/- ambapo hadi kukamilika kwake unatarajiwa kufikia Milioni 50,000,000/-.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Umoja na Mshikamano waliyouonyesha Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko ndio chanzo cha mafanikio hayo yanayopaswa kuigwa na Wananchi wa Vijiji vyengine hapa Nchini.

“ Nafarajika kuona Mtaa wa Bubujiko kwa sasa utabakia katika Historia ya kuepuka na Mafuriko yaliyokuwa yakileta simanzi na hasara kubwa kwa Wakaazi wake”. Alisema Balozi Seif.
 Mhandisiwa Ujenzi wa Mtaro wa Kijiji cha Bubujiko Bwana Bwana Mohamed Abdullah kutoka Wizara ya Kilimo, Mali Asili, Uvuvi na Mifugo Pemba akimuonyesha Ramani ya Mtaro huo Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa mbele ya Karo inayoingiza maji hayo.
 Balozi Seif akiwapongeza Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko kwa hatua waliyochukuwa ya ujenzi wa Mtaro utakaonusuru na majanga ya mafuriko ya mavua.
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko wakisikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao kwenye Mtaa wa Kijiji hicho kiliopo pembezoni mwa Mji wa Wete.
 Mkaazi Muathirika nambari moja wa majanga yaliyokuwa yakitokea kwenye Kijiji hicho wakati wa Mvua za Masika Maalim Omar Hamad kwa niaba ya Wananchi wenzake akiishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada inazochukuwa za kuwahudumia Wananchi wake.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA JINSIA NA MAHAKAMA AFRIKA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) tayari kufungua Mkutano wa Kimataifa unaohusu masuala ya Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, wengine pichani kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma,Waziri wa Sheria Dkt. Palamagamba Kabudi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

NEWS ALERT: MZEE JUMA MBIZO AINGIA STUDIO KUACHIA KIBAO CHA BONGO FLEVA NA MWANAE H-MBIZO

$
0
0
Inaweza kukuwia vigumu kuamini, lakini ndiyo hivyo tena, akiwa anatimiza umri wa miaka 68, miaka 39 ya kuwepo kwenye fani za michezo na burudani, Mzee Juma Mbizo ameamua kuingia studio kwa mara kwanza na kufanya ‘kolabo’ na mwanae H-Mbizo.
Naam Mzee Mbizo amejitosa katika studio za Fire Music chini ya producer More Fire na kurekodi wimbo wa pamoja na H-Mbizo aliyepata kutamba na wimbo wa “Mchumba”.
H-Mbizo ambaye pia ni mwandishi mzuri wa nyimbo akiwa amewaandikia wasanii wengi akiwemo Snura kupitia wimbo “Majanga”, ameuambia mtandao huu kuwa kibao hicho alichoimba na baba yake kitaachiwa hewani mwezi huu.
Licha ya ukongwe wake kwenye game na utalaam wa kuandaa matamasha makubwa ya burudani, lakini Mzee Mbizo hakuwahi kuingia studio na kurekodi wimbo wowote ule na hii ndio hali itayofanya kazi hii alishoshirikishwa na mwanae iteke masikio ya mashabiki wengi wa muziki.

Mwakyembe aipa mamlaka BMT kusimamia mchezo wa kuogelea

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja baina ya serikali na viongozi wa zamani wa Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) na kuamuru BMT kusimamia shughuli za mchezo huo wakati mchakato wa kuandaa uchaguzi mkuu ukiandaliwa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Suzan Mlawi na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT. Alex Nkeyenge.

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipa mamlaka Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) kusimamia shughuli za mchezo wa kuogelea wakati mchakato wa kuandaa uchaguzi mkuu wa chama hichon (TSA) ukiandaliwa.

Waziri Mwakyembe alisema hayo juzi katika kikao kilicho wakutanisha viongozi wa zamani walioenguliwa madarakani na wanachama wa chama hicho na Kamati ya Muda iliyomaliza muda wake wa miezi mitatu.

Alisema kuwa TSA  imekuwa na mvutano wa uongozi kwa muda sasa na kuhatarisha maendeleo ya mchezo huo ambao umeifanya Tanzania kutambulika zaidi kwa nchi za Kanda ya Tatu (Cana zone three) ikiwa ni mabingwa mara mbili mfululizo.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkeyenge akizungumza.

Mwakyembe alisema kuwa mbali ya BMT kusimamia mchezo huo kwa sasa, viongozi wa zamani chini ya mwenyekiti Alex Moshi na Katibu Mkuu, Ramadhani Namkoveka wanatakiwa kuwasilisha ripoti ya utendaji wao ikiwa pamoja na taarifa za fedha (mapatona matumizi) kwa Msajili wa Klabu na Vyama Vya Michezo.

Alifafanua kuwa TSA ilitakiwa kufanya hivyo mwaka jana, lakini kutokana na hali ilivyokuwa, zoezi hilo lilisogezwa mbele mpaka Februari 28 mwaka huu, jambo ambalo halikufanyika.

“Nawaagiza kuwasilisha taarifa za utendaji wenu haraka iwezekanavyo kwa Msajili, kinyume hayo, sheria itachukua mkondo wake, serikali ya Awamu ya Tano  haina mchezo mchezo kwa viongozi ambao hawawajibiki na tutafanya haya kwa kila chama cha michezo,” alisema Mwakyembe.
Wanachama wa TSA wakifuatilia mkutano.

Alisema kuwa  hata viongozi ambao walijihudhuru nafasi zao, wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao mpaka pale walipoamua kuachana na uongozi.

“Naipongeza Kamati ya Muda kwa kukamilisha kazi zao kwa muda wa miezi mitatu kama walivyopewa na BMT na kwa sasa suala la Katiba litajadiliwa na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Msajili na viongozi wa zamani na Kamati hiyo siku ya Jumatano (June 13),” alisema.

Kamati ya Muda iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Imani Dominick na Katibu wake, Inviolata Itatiro iliyomaliza muda wake Juni 9 mwaka huu. Wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa, Alex Mwaipasi, Amina Mfaume na Anna Shanalingigwa.
Mwenyekiti wa zamani wa TSA, Alex Moshi akizungumza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa TSA, Imani Dominick akizungumza.

DSTV WANAKWAMBIA HIVIII.... mambo ni Motoooo!

$
0
0
Zikiwa zimesalia siku 3 tu kuelekea katika mashindano ya FIFA Kombe La Dunia 2018 nchini Urussi. DStv watakuwezesha wewe mteja wao kufurahia mechi zote 64 za michuano ya FIFA Kombe la Dunia 2018 LIVE zikiwa kwenye picha ang’avu HD kupitia chaneli zake mpaka 6 maalum zilizoandaliwa kwa ajili ya mchuano hii. Wateja wote wa DStv watafurahia mashindano haya kuanzia kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu!

DStv pia imekuandalia matangazo ya moja kwa moja ya FIFA Kombe la Dunia 2018 kwa Lugha ya Kiswahili utakaoletwa kwenu na timu yetu mahiri ya wachambuzi Nguli wa soka kutoka hapa nchini akiwamo Oscar Oscar, Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Ibrahim Maestro, Edoku Mwembe, bila kumsahau Ephraim Kibonde watakaokuletea matangazo haya LIVE kutoka Russia.

Kwa kuongezea, DStv imekuleta ofa maalum kwa wateja wake wapya, Sasa wataweza kujiunga na DStv kwa shilingi 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure kitakachokuwezesha kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia LIVE mechi zote 64 kupitia chaneli za supersport .

Mbali na ofa hiyo na kutangazwa kwa michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili, DStv inataka kuhakikisha kuwa wateja wanaweza kutazama DStv popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, laptop na tablet.

Download App yetu ya “DStv Now”, unaweza kutumia hadi vifaa vitano tofauti ambavyo vyote huunganishwa na dikoda yako hivyo kuwawezesha wanafamilia kutazama vipindi tofauti wakiwa sehemu yoyote kwa kutumia vifaa vyao.

Kujiunga wasiliana nao kwa namba 0659 070707
Wanasema “Kama Sio DStv Potezea”!!

Mwongozo wa ukuaji bora wa miji wazidi kunolewa

$
0
0
Na Mwandishi wetu,
WATAFITI waliokuwa wakifanyia utafiti mada kuhusu ukuaji bora wa miji nchini Tanzania, wamekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha katika mkutano mkubwa wa wadau chini ya mwavuli wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) siku ya Ijumaa tarehe 8 Juni 2018.
Katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida, ilielezwa kuwa Tanzania Urbanisation Laboratory (TULab)  ilikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuonesha njia bora ya ukuaji wa miji nchini Tanzania kwa kuzingatia uchumi wa viwanda katika tafiti zake tatu.
TULab ilibuniwa mwaka jana kufuatia uchambuzi wa hoja ya Better Urban Growth in Tanzania ambayo ilijengwa katika kuhakikisha kunakuwepo na uelewa na kuuchochea mazungumzo ya kisera juu ya mabadiliko muhimu yanayotarajiwa katika kuelekea nchi yenye majiji makubwa yanayoshindana.
Mkutano wa mwishoni wa wiki uliitishwa kwa ajili ya kuona kilichojiri katika tafiti tatu kabla ya utafiti mwingine wa nne kufanyika, baadae mwaka huu.
Utafiti huo umelenga kutoa majibu kwa maswali yanayohusu maendeleo ya miji nchini Tanzania ambapo wadau wanatakiwa kuona.
Dkt.  Kida alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kukubali kuwa mwenyekiti wa jukwaa hilo lenye umuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Septemba mwaka jana kulianzishwa tafiti tatu ambazo zilichangiwa vyema na wajumbe na sasa mkutano huo ulikuwa unatoa taarifa za mwisho kuhusu nini wamekibaini katika tafiti hizo tatu.
Utafiti wa kwanza ulilenga kuelewa ugharimiaji wa miundombinu na huduma katika majiji makubwa 6 nchini Tanzania. Utafiti wa pili ulichunguza uhusiano kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na namna uhusiano huo unavyo athiri ugharamiaji wa miundombinu na utoaji wa huduma katika miji, na utafiti wa tatu ulilenga kuibua taarifa na takwimu ambazo zilikuwa hazijabainika hasa katika masuala ya maji.
pekee au watu binafsi pekee bali zinatakiwa kufanywa kwa ushirikiano.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa mabaara kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji yaliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dr. Idda Swai akiwsailisha utafiti juu ya uhusiano kati ya Serikali kuu na serikali za mitaa na athari zake katika kutoa huduma kwa wananchi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Mussa Martine akiwasilisha mada kuhusu huduma za tafiti za kifedha kwenye miji wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mtafiti Mshiriki kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dr Nathalie Jean-Baptiste akiwasilisha mada kuhusu utafiti uliofanywa wa maisha ya kila siku ya wananchi kwenye miji ya Tanzania wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini, akielezea mipangilio ya programu hiyo kuelekea mabadiliko ya miji iliyopangwa wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete wakijadiliana jambo wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RIDHIWANI APATA FUTARI NA VITUO VITANO VYA WATOTO YATIMA NYUMBANI KWAO MSOGA

$
0
0
 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza baada ya kumaliza Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu.
 Mmoja ya Wadau kutoka Tasisi ya K Innovates Nasra Kaseja akizungumzia umuhimu wa kuwasaidia watoto yatima wakati wa Iftar iliyoandaliwa na  Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu kata ya Msoga.
 Mshereshaji Masoud Kipanya akizungumza juu ya utaratibu na umuhimu wa kufutirisha makundi ya watu maalum katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.  
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa ana swali kabla ya Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watoto yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipakuwa chakula wakati wa  Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu.
 Wadau wa Tasisi ya Ko Innoavate Pink Ijab wakiwa katika picha ya kabla ya Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Msoga
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete katikati  akiwa na Wadau waliotoa Vifaa kwa ajili ya Watoto Yatima wakati wa  Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Msoga
Baadi ya wadau waliofika  katika  Iftar   iliyofanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu.

TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limepewa muda wa miezi mitatu kuhakikisha maeneo yote ambayo reli inakatiza barabara kuwe na vizuizi  badala ya kutegemea alama peke yake.
Uamuzi huo unakuja ikiwa ni siku chache zimepita  tangu kutokea kwa ajali ya basi kugonga treni mkoani Kigoma na kusababisha watu 10 kufariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati anazindua bodi mpya ya wakurugenzi ya TRC.
Hivyo wakati anazungumza na wajumbe hao na watumishi wa TRC amesema ipo haja ya kuweka vizuizi kwenye maeneo ambayo reli inakatiza barabara.

Amesema katika suala la usalama wa raia wa nchi hii gharama isiwe kigezo cha kutowekwa vizuizi hivyo huku akitoa maagizo ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa vizuizi viwe vimewekwa.
"Hakikisheni kunakuwa na vuzuizi kwenye maeneo ambayo reli inakatiza barabara, ile ajali ya Kigoma kama kungekuwa na kizuizi huenda isingetokea.

"Kuwa na alama peke yake haitoshi kwani wapo wengine macho yao hayaoni mbali, hivyo kukiwa na kizuizi hakuna anayeweza kupita,"amefafanua Waziri Mbarawa.

Amesema vizuizi hivyo vinaweza kuwa vya nguzo ambapo kutakuwa na mtu maalum atatakiwa kukaa na hata akilipwa Sh.300,000 kwa mwezi si mbaya na wala si gharama mbele ya uhai wa mtanzania, hivyo vizuizi hivyo vianze kuwekwa mara moja.

ZIARA YA ULEGA JIMBO LA MKURANGA YAPAMBA MOTO, SEKTA YA ELIMU YAPEWA KIPAUMBELE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Mkuranga na Naibu Waziri Ufugaji na Uvuvi Abdallah Ulega ameendelea na ziara yake katika jimbo la Mkuranga katika kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo Ulega amesisitiza umoja na mshikamano  katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo kwa mustakabali wa kizazi kijacho na amesema anatambua changamoto ambazo bado zinazikabili jimbo lao na ataendelea kupambana nazo.

Ulega amefafanua kuwa kuhusu maeneo yenye changamoto kama  miundombinu ya barabara kukatika baada ya mvua kupita tayari fedha zimetengwa kwa  maeneo hayo na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa makandarasi.

Ulega amesisitiza kuwa ataendelea na jitihada zake na kushirikiana na wadau wa maendeleo katika  kupunguza kama si kumaliza kero ambazo bado zipo katika baadhi ya maeneo hasa katika  elimu, afya na masuala ya kijamii. 

Mkazi wa Mkuranga Yasin Ligwema ameeleza kuwa vyoo vipewe vipaumbele katika shule ili kuwaweka wanafunzi hasa watoto wa kike katika kujisitiri.

Aidha wananchi  wamempongeza Mbunge wao katika kutoa vipaumbele katika masuala ya maji, elimu na afya.

Ulega alihitimisha ziara hiyo kukabidhi zakatulfitry kwa wajumbe waliohudhuria.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega na akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mlamleni katika mkutano huo.
 Sehemu ya wanachi wa kijiji cha Mlamleni  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga  Abdallah Ulega  katika mkutano huo.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mlamleni juu ya kuendelea kushirikiana na wanachi kwa kila jambo na kutatua kero zao.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Mmoja wa wazee wa kijiji cha Mlamleni akielezea kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega.

WAZIRI PROF. MBARAWA ATOA MAAGIZO KWA BODI MPYA YA WAKURUGENZI TRC

$
0
0
*Ni baada ya RAHCO, TRL kuunganishwa, azindua bodi ya wakurugenzi TRC 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya Wakurugezi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge).

Amesisitiza ujenzi wa reli hiyo ni wa kihistoria nchini na baada ya kukamilika kwake itachukua miaka 100 kushuhudia tena ujenzi wa reli ya aina hiyo , hivyo ni fursa kwa TRC kuhakikisha wanapeleka wataalam wa kada mbalimbali kujifunza na kupata uzoefu.

Pia amesema ni wakati muafaka kwa bodi hiyo kuanza kuandaa watalaamu kabla ya kukamilika kwa ujenzi huo Novemba mwaka 2019 ikiwa ni pamoja waendeshaji wa mitambo.

Profesa Mbarawa amesema hayo leo Dar es Salaam wakati anazindua rasmi Bodi mpya ya TRC ambayo Mwenyekiti wake ni Profesa John Kondoro. 

Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo, Profesa Mbarawa amesema anatambua majukumu ambayo bodi hiyo wanayo katika kuhakikisha wanatekeleza vema majukumu waliyonayo hasa kipindi hiki ambacho ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea.
Hivyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo kwa karibu zaidi badala ya kuacha wajenzi peke yako.

Amesema siku za karibuni alifanya ziara saa sita usiku ya kwenda kuangalia ujenzi huo.Alifanya hivyo baada ya kupata taarifa hakuna usimamizi wa kutosha unaofanywa na TRC.

"Wakati naenda kwenye ile ziara kuna mtu alikuwa na taarifa hivyo akawaambia, bila hivyo nisengewakuta kule usiku.Hakikisheni mnausimamia ule mradi badala ya kukaa kando na kuacha wakandarasi peke yao,"amesema Profesa Mbarawa.

Pia amewasisitiza umuhimu wa kuanza kuandaa waendesha mitambo mapema kabla ya kukamilika kwa ujenzi.
"Haitakuwa vema mradi unakamilika halafu wanapewa watu wengine kuuendesha wakati Watanzania wapo na wakiandaliwa mapema wanaweza kuendesha mitambo kwa ufanisi mkubwa,"amesema.

Pia amesema maandalizi hayo yaende sambamba na upatikanaji wa vipuri ili isiwe kila kitu kinapoharibika kinaagizwa nje ya nchi.

Wakati huohuo ameitaka TRC kuhakikisha idadi ya mizigo na abiria inaongezeka kutokana na uwekezaji unaendelea kufanyika hasa kwa kuzingatia wamepewa vichwa vipya vya treni.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Masanja Kadogosa amemuelezea Waziri changamoto na mafanikio ya shirika hilo huku akiahidi kuwa wataendelea kutoa huduma bora na kuongeza idadi ya abiria na mizigo inayosafiri kwa treni.

Serikali imeamua kuziunganisha Shirika Hodhi la Reli(RAHCO) na Shirika la Reli Tanzania(TRL) na kupata TRC.

Kutokana na muunganiko huo wajumbe wa bodi hiyo wamehimizwa kufanya kazi kwa ushirikiano hasa kwa kuzingatia kabla ya hapo kila mmoja alikuwa na utamaduni wake wa kutekeleza majukumu yao.
 Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati  akizindua bodi ya wakurugezi wa shirika la reli Tanzania (TRC) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images