Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa (kushoto) akizungumza siku ya uzinduzi wa kozi mpya kusimamia miradi mikubwa ya kimataifa iliyoanzishwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya ISAE ya Brazil. Wa pili kustoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Andrew Mbwambo, Mratibu wa Taasisi hiyo ya Brazil Bi. Rebecca Giese (kulia) na Prof. Wanderlei Marinho da Silva wa taasisis hiyo (wa pili kulia).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa (kulia) akipokea nyaraka mbalimbalikwa ajili ya kufundishia kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya ISAE ya Brazil, Bi Rebecca Giese wakati wa siku ya uzinduzi wa kozi mpya kuhusu usimamizi wa miradi mikubwa ya kimataifa jana jijini Dar es Salaam. Kozi hiyo imeanzishwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya ISAE ya Brazil.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa (kushoto) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa kozi mpya na ya kwanza ya kimataifa ya maswala ya kusimamia miradi mikubwa ya kimataifa iliyoanzishwa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya ISAE YA Brazil. katikati ni Profesa Wanderlei Marinho da Silva wa taasisis hiyo ya Brazil na kulia ni Mratibu wa Taasisi hiyo, Bi. Rebecca Giese.