Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117117

Kijitonyama Veterans Vs Golden Bush Veterans Jumamosi

$
0
0
Baada ya tambo za hapa na pale hatimaye vigogo wa soka la wazee hapa Dar es Salaam wanategemea kukutana siku ya Jumamosi katika uwanja wa bora, pale kijitonyama, jijini Dar es salaam.
Ni mechi yenye kila aina ufundi maana timu hizi mbili zinasifa tofauti kabisa. Kijitonyama ni timu maarufu sana kwenye vyombo vya habari huku Golden Bush ikiwa na sifa ya kutoa vipigo kwa timu pinzani, ni timu pekee iliyopoteza mechi chache sana toka ianzishwe. Ni kutokana na umuhimu wa game hii ya jumapili tunalazimika kuweka Camp Bamba Beach ili timu iwe sawasawa kabisa. 
Tumewatafuta kwa muda mrefu sana ndugu zetu hawa lakini tunamshukuru mmoja wa viongozi wa Kijitonyama Veterans bwana Majuto Omary amekubali game bila kusita. 
Tunaomba mashabiki mfike kwa wingi ili kuona burudani ya watu wazima walioacha mpira huku wakiwa bado kwenye kiwango cha juu kabisa. Maandalizi ya game yamekamilika na uwanja umefungwa kwa muda ili siku ya mechi pitch iwe sawasawa kabisa. 
Tumeamua kutoa habari hii mapema ili watu wa mkoani na nchi za jirani wapeta muda kujiandaa kuja kuangalia game hii siku ya tarehe 04/08/2013.

Asanteni. 
Onesmo Waziri “Ticotico” 
Msemaji wa timu na mchezaji 
mwandamizi Golden Bush FC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117117

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>