Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117117

NAIBU WAZIRI PEREIRA SILIMA ATOA TUNZO KWA CHAMA CHA WADAU WA MAGARI TANZANIA (AAT).

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (kulia) akimkabidhi tunzo Rais wa Chama cha Wadau wa Magari (AAT), Nizar Jivani kwa ajili ya chama chake kutoa mchango mkubwa kwa kutoa mafunzo ya uendeshaji kwa madereva 2500 wa pikpiki, ambao tayari wamehitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013. Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (kulia) akiwafafanulia waandishi wa habari, jisni Chama cha Wadau wa Magari nchini (AAT), kilivyokuwa kinatoa mchango wake kwa kutoa mafunzo ya uendeshaji pikpiki kwa jina maarufu bodaboda. Madereva 2500 wa pikpiki walihitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013.      
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (wapili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wadau wa Magari (AAT) Nizar Jivani na Yusuf Ghor. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.  Naibu Waziri Pereira alitoa tunzo kwa uongozi wa AAT kwa ajili ya  kutoa mafunzo ya uendeshaji pikpiki kwa jina maarufu bodaboda. Madereva 2500 wa pikpiki walihitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013. Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117117

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>