Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117117

jk awataka uhamiaji kuacha uzembe

$
0
0
Na Angela Sebastian, Bukoba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema udhaifu na uzembe unaoendelea kufanywa na watendaji wa Idara ya Uhamiaji umesababisha nchi kuwa na lindi kubwa la wahamiaji haramu kutoka katika nchi zinazotuzunguka.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kwa uchungu leo Ikulu ndogo mjini Bukoba wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani hapa na kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kwasasa Tanzania ina wahamiaji haramu zaidi ya 52,000 huku mkoa wa Kagera ukiwa na wahamiji haramu zaidi ya 36,000 ambapo ameongeza kuwa hilo ni tataizo kubwa lililosabaishwa na udhaifu wa watendaji wa idara ya uhamiaji na litaigharimu nchi yetu.

“ Tanzania sio shamba la bibi kila mtu anaingia na kutoka na mifugo yake eti kwasababu kuna sehemu nzuri ya malisho alafu watendaji wa vijiji na wenyeviti wanawapa vibari wahamiajia hao na kuwahonga viongozi hao wa vijiji ng’ombe sana sana hawazidi wawili na nyie uhamiaji mnaona na kuyafumbia macho mnatenda dhambi kubwa asambayo inapeleka nchi yetu katika hali mbaya kwa kipindi cha miaka 50 ijayo”alisema Rais Kikwete kwa uchungu.

“Hili sijalisema kwa mara ya kwanza,niliisha lisema hata mwaka 2008 nilipokuja Kagera na kuhutubia wilayani Muleba lakini bado mmenyamaza,kuna mtu anaitwa Katongole anaishi kule mpakani Mutukula ndiye anayeingiza wahamiaji hapa nchini ameishajua bei zenu anawahonga anaingiza watu wake,mtu anayetoa rushwa anajulikana ushahidi upo wanaohongwa wanajulikana PCCB mnafanya nini mmenyamaza tu basi kazi imewashinda”aliongeza Rais

Alisema hili suala la watendaji na wenyeviti wa vijiji kuwapa vibali watu hao,uhamiaji wanalijua na wameliacha kwa muda mrefu na kama wangelitilia maanani pale mnapobaini kuwa viongozi hao wametoa vibali feki mnawakamata na kuwachukulia hatua,nchi isingefikia hatua hii ya kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji kiasi hiki.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya ulegevu na udhaifu wenu inawafanya watu wajiulize maswali mengi juu ya utendaji wenu wa kazi na kuwaona kama nyie ndio sehemu ya tatizo; kila siku sisi misako tu mpaka lini?kwanini tusisimamie zoezi hili kwa umakini pale mtu anapoingia tu na kumbaini tunamrudisha mara moja na sio kusubiri wawe wengi ndio mfanye misako,itafikia siku mtataka kuwarudisha watagoma na kukuelezeni kuwa ni kwao na wanahaki ya kuishi hapa jambo ambalo litazua mtafaruku mkubwa kati ya wazawa na hao wahamiajia haramu na mwisho wake ni mapambano.

Alisema hatuchukii wageni ila mtu anayetaka kuishi Tanzania afuate utaratibu,apeleke maombi uhamiaji na watayafanyia kazi na pale mtu akikataliwa kupewa uraia asihoji kwasabu sio kila mtu atapewa uraia kuna wengine ni majambazi,wauza madawa ya kulevya na makosa mengine hatuwezi kuwapa uraia”mwaka 1982 Hayati mwalimu Julias Nyerere alitoa uraia wa fursa kwa wahamiaji 30,000 wakapata uraia na mimi kwa kipindi cha uongozi wangu nimetoa Fursa hiyo ambapo watu 160,000 wameomba na kupewa uraia kwaiyo ambaye hakuomba huyo hataki kuwa raia wa Tanzania wasakwe na kurudishwa kwao pia kumbuka hao ni binadamu wasiswagwe kama mifugo kama mtu ana mali yake auze na kuondoka msiwadhulumu.

Aidha Rais amewaasa Watanzania kuacha kutumiwa na watu wenye nia mbaya ya kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu kwa kupitia njia ya udini na siasa kwani matokeo yake ni kugawanyika na kupoteza malengo yao.

Pia ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Bukoba kumpa jibu haraka kuhusu wananchi 800 wa mgogoro wa viwanja wanapewa lini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117117

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>