Bw. Samson Kamalamo anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake Mzazi Bw. Samwel Bulimbe Kamalamo kilichotokea Julai 27, 2013 jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, Mtaa wa Daima jijini Dar es Salaam.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. Maziko yanatarajiwa kufanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Julai 31, 2013. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,
Amen.