MBUNGE wa Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), leo katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, mjini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi.
Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao
Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho
Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo.
Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo
Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili.
Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja. NA theNkoromo Blog