HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TU ZINASEMA MFANYABIASHARA MMOJA MAARUFU NCHINI SAID MOHAMED AMEMWAGIWA KITU KINACHODHANIWA NI TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA MAENEO YA MSASANI JIRANI NA KITUO CHA POLISI CHA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.
MFANYABIASHARA HUYO ANAEMILIKI MADUKA YA HOME SHOPPING CENTRE INASEMEKANA AMEPATWA NA SHAMBULIO HILO MARA BAADA YA MUDA WA KUFUTURU.
AIDHA, WANAHABARI WETU WAMESHUHUDIA MAGARI KADHAA YA POLISI YAKIWA KWENYE MAEGESHO YA DUKA MOJA KUBWA LILILOPO MAENEO KARIBU NA OYSTERBAY POLICE, AMBAKO HAKUNA ALIYETAKA KUSEMA CHOCHOTE, JAPO HABARI ZINASEMA HAPO NDIPO TUKIO LILIPOTOKEA.
JUHUDI ZA KUMSAKA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KINONDONI AMA KAMANDA WA KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM AFANDE SULEIMAN KOVA ZINAENDELEA. NASI TUTAWAJULISHA KILA TUTAPOPATA HABARI ZAIDI.