Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba wa pili kushoto akitoa Maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha cha maandalizi ya mwisho cha kupitia Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla ya kuiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara mjini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu aliyenyanyua mkono akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kuhusu bajeti ya Jeshi la Polisi nchini mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo mjini Dodoma.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akipokea taarifa mbalimbali zilizotolewa na watendaji wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa wizara mjini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa wa pili kulia akitoa ufafanuzi mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye wa tatu kulia akitoa ufafanuzi kuhusu Jeshi lake mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa Kikao cha maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kusomwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI