Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amenunua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC zenye thamani ya Tsh. milioni 10 pamoja na nyingine za Tsh. milioni 10 kwa ajili ya mke wake, Mary Majaliwa ili kuwahamisha watanzania kuwekeza katika uchumi unaokuwa kwa kasi.
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo Ijumaa, Mei 5, mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wakuu wa Masoko ya Hisa na Dhamana; Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amewasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao. “Hii ni fursa kwa Watanzania kumiliki kampuni. Ukinunua hisa, unashiriki kikamilifu kumiliki kampuni na pia unaboresha uchumi wako binafsi. Ninawasihi Watanzania wote tumieni fursa hii kununua hisa hizo kabla muda haujaisha ili kuboresha uchumi wetu,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kuimarisha teknolojia yake ili kuwaunganisha watanzania na kuwezesha kukuza uchumi binafsi. Vodacom Tanzania ilianza kuuza hisa za awali mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa kuuza hisa hizo itakuwa ni Mei 11, 2017.
Makundi mbalimbali ya watu wanaendelea kununua hisa za vodacom kwa ajili ya maisha ya baadae. Uuzwaji wa hisa za awali bado unaendelea hadi tarehe 11/05/2017. Waziri Mkuu kaonesha amechangamkia fursa nasi tusibaki nyuma tuwekeze katika uchumi unaokuwa kwa kasi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiongea wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa zake pamoja na mke wake Mary Majaliwa zenye thamani ya shilingi Milioni 20, wapili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Bi. Beng’i Issa , Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Rosalynn Mworia.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akielekezwa jinsi ya kujaza fomu za kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities, Bw. Gerase Kamugisha (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji, Bi.Beng’i Issa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Ian Ferrao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities, Bw. Gerase Kamugisha wakati wa hafla fupi ya kununua hisa zake na mke wake Mama Mary Majaliwa (hayupo pichani) zenye thamani ya shilingi Milioni 20.Hafla hiyo ilifanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao baada ya kununua hisa zake na za mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani) kutoka Vodacom Tanzania PLC kampni hiyo zenye thamani ya Shilingi Milioni 20.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wadau wakati wa hafla fupi ya ununuzi wa hisa Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa zenye thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na mke wake Mama Mary Majaliwa.
Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA
Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA