Unapomuongelea MAKEKE si jina geni kwenye Tasnia ya mitindo nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mwaka jana alikuja na collection ya aina yake iliyoitwa TABID - The African Beauty in The darkness, ( uzuri wa Afrika gizani) collection hio imefanya vizuri sana 2016/2017 kwani imeoneshwa kwenye Majukwaa mbalimbali makubwa ya mitindo. Na mwaka huu mwanamitindo huyu asiyeishiwa MAKEKE amekuja na kitu kipya kabisa, kinachoitwa OTOSIM2017 - ON THE OTHER SIDE OF MAKEKE, akiwa na maana ya ladha/ubunifu wa aina Nyingine. Kwa Mara ya kwanza OTOSIM imeoneshwa kwenye jukwaa kubwa la ZANZIBAR SWAHILI FESTIVAL mwezi uliopita na kufanya maajabu makubwa jukwaani. Kwa watu waliokuwepo pale walijionea utamu wa show hiyo ya Ki - MAKEKE. Msanii huyu wa mitindo ameahidi mambo mengi matamu zaidi kwa mwaka huu 2017. Tuendelee kusubiri.
↧