Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa kuna ajali imetokea muda huu katika eneo la Rhotia Wilaya ya Karatu Mkoani Manyara, iliyohusisha Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, inayodaiwa kuwa ilipoteza mueleo na kupinduka wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu waliokuwa wakienda kufanya mitihani na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya Karatu. Inadaiwa kuwa wanafunzi zaidi ya 20 na walimu wao wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa. jitihada za kumtafunda Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara zinaendea ili kupata kauli yake juu ya ajali hii. Pichani ni baadhi ya wasamalia wakitoa msaada wa uokozi kwa wanafunzi hao.
Zoezi la uokoaji kwa wanafunzi hao likiendelea.