Leo Prof. Mark Mwandosya, aliyekuwa Kamisha, Katibu Mkuu, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Waziri wa Nchi(Mazingira), Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Waziri wa Nchi(Ofisi ya Rais-Kazi Maalum) amemtembelea Mhe. Stephen Masato Wasira nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam kumjulia hali na kubadilishana uzoefu. Mheshimiwa Wasira ni mmoja ya wanasiasa wa siku nyingi nchini. Amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa, Naibu Waziri, Waziri wa Wizara mbalimbali, akimalizia kama Waziri wa Nchi(Ofisi ya Rais) na hatimaye Waziri wa Kilimo.
↧