Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MSANII wa Sanaa za Maonyesho Amani Kipimo anataraji kufanya onesho la Igizo la Jukwaani linalokwenda kwa jina la Untoldy Story litakalo fanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi blogu muandaji wa enesho hilo Amani Kipimo amesema kuwa enesho ambalo litakuwa la bure hivyo anawaomba kila mtu aliyopo nje na ndani ya Dar es Salaam kufika katika ukumbi wa makumbusho Mei 18 mwaka huu.
Kipimo amesema kuwa eneo hilo alina kiingilio hivyo kuwaomba watu kufika kwa wingi kujionea namna ya wataalamu na manguli wa sanaa za jukwani watakavyokuwa wanatoa burudani na ujumbe kwa jamii.