Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiongea wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa zake pamoja na mke wake Mary Majaliwa zenye thamani ya shilingi Milioni 20, wapili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Bi.Beng’i Issa , Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akielekezwa jinsi ya kujaza fomu za kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities,Gerase Kamugisha (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji, Bi.Beng’i Issa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities ,Gerase Kamugisha wakati wa hafla fupi ya kununua hisa zake na mke wake,Mary Majaliwa(hayupo pichani) zenye thamani ya shilingi Milioni 20.Hafla hiyo ilifanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao baada ya kununua hisa zake na za mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani) kutoka Vodacom Tanzania PLC kampni hiyo zenye thamani ya Shilingi Milioni 20.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wadau wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa zenye thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na mke wake Mary Majaliwa.