Na Shamimu Nyaki.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba Wataalamu wa lugha ya Kichina hapa nchini kutafsiri Filamu za Kiswahili kwa lugha ya kichina ili zipate soko nchini China.
Prof. Elisante Ole Gabriel ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua Maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo amesema kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa watanzania katika filamu za kichina ni kutumia lugha ya Kiswahili.
“Njia rahisi ya kufikisha ujumbe kwa watu wote ni kutumia lugha mtambuka katika tamthiliya zetu hii itasaidia sana kukuza uhusiano wetu na Jamhuri ya Watu wa China”,Alisema Prof.Ole Gabriel.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi vya Luninga Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy ameelza kuwa ushirikiano wa shirika hilo na Kampuni ya Star Times ambayo ndio waandaji wa Tamthiliya hiyo umeleta mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa watazamaji wanaopenda tamthiliya za kichina zenye tafsiri ya lugha ya Kiswahili zinazooneshwa katika luninga hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na hadhira (haipo katika picha) katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi vya Luninga Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy akizungumza na hadhira (haipo katika picha) akitoa maelezo mafupi kuhusu Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali ya China katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimataifa nchini China, Bi. Ma Li akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.