Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth
  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akitambulisha ujumbe alioambatanao kabla ya mazungumzo mafupi na na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisini kwake kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18, 2019. Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.

   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipotembelea Ofisini kwake leo Novemba 18, 2019.

   Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisi kwake leo kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18, 2019. 

  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akizungumza na wafungwa na mahabusu wa Gereza Mbulu(hawapo pichani) leo Novemba 18, 2019 alipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo(Picha zote na Jeshi la Magereza).

   Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Mbulu, SP. Danson Mpinga alipowasili Gereza Mbulu leo kwa ziara ya kikazi. Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.


  0 0


  *AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WATATU

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini kuhusu utendaji kazi wake huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa wakala huo.

  “TBA tunaihitaji lakini watu wake wana shida. Hatuwezi kuwaacha, TBA wasipewe miradi kwa sababu hawawajibiki na wanadhani kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ndio wataachwa wafanye mambo ya hovyo.”

  Waziri Mkuu amewasimamisha kazi wakurugenzi hao leo (Jumatatu, Novemba 18, 2019) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

  Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Arch.Humphrey Killo, Kaimu Meneja wa Miradi, Abdallah Awadh na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushauri Arch. Hamis Kileo.

  Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika miradi mbalimbali waliyopewa na Serikali ukiwemo ujenzi wa jengo la NEC ambalo ujenzi wake ulianza Julai, 2017 na ulitakiwa ukamilike Juni 2018 kwa gharama ya sh. bilioni 13. Hata hivyo mradi huo bado haujakamilika na ujenzi wake umesimama.

  Akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya NEC Waziri Mkuu alihoji sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi alisema jengo hilo limeshindwa kukamilika kwa sababu wakati walipokuwa wanaanza kazi walibaini kuwa kuna vitu vilisahaulika wakati wa uandaaji wa Bill of Quantities(BOQ). TBA ndio waandaaji wa ramani ya jengo hilo na ndio wajenzi.

  “Bajeti ya awali ilikuwa sh. bilioni 10 wakati wa uandaaji wa michoro ya ujenzi gharama ziliongezeka na kufikia sh. bilioni 13 ambazo ndizo tulikubaliana katika mkataba. Wakati tunaendelea na kazi tuligundua kuna vitu vimesahaulika kwenye BOQ jambo lililoongeza bajeti ya ujenzi na kufikia sh. bilioni 32.” Amesema Arch. Killo.

  Waziri Mkuu akahoji tena “kutoka sh. bilioni 13 hadi kufikia sh. bilioni 32 je unaona inakuja vizuri hiyo” sh. bilioni 10 hadi sh. bilioni 13 tena hadi sh. bilioni 32 inazungumzikaje hii na je mwenye jengo mlikubaliana naye? Awali mwenye mahitaji alisema ana sh. bilioni 10 sasa imefikaje 32 je mlimshauri muhusika kuhusu ongezeko hili?

  Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi Arch. Killo alipotakiwa kueleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi huo amesema waligundua tofauti wakati wakiwa kwenye eneo la ujenzi kwamba kuna kazi zilitakiwa zifanyike lakini katika mkataba hazipo na hawakuwasiliana na muhusika.

  Miongoni mwa vitu vilivyosahaulika katika BOQ ya mradi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa ghorofa ya nne katika jengo moja wanalolijenga katika mradi huo ambalo ni la ghorofa nane, pia hapakuwa na paa la jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya NEC.

  Waziri Mkuu amesema miradi mingi inayojengwa na TBA katika maeneo mbalimbali imeshindwa kukamilika kwa wakati, hivyo amemwagiza Waziri wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama asitishe mkataba huo wa ujenzi na atafutwe mkandarasi mwingine aje amalizie.

  “Jengo la TAMISEMI lililopo katika mji wa Serikali limejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.7, nyie wataalamu gani na kwa nini tuendelee kuwaacha ndani ya taasisi? TBA hamfanyi kazi vizuri wakuu wa mikoa na wilaya wanalalamika majengo hayakamiliki ni Serikali gani itakayowavumilia, mmeshindwa kutambua majukumu yenu.”

  Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.  
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu), wakati alipoenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), uliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, ambao haujakamilika kwa wakati, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi (TBA), Humphrey Killo (kulia), wakati alipoenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, Novemba 18, 2019, baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mwakilishi wa Meneja Mradi, kutoka Chuo Kikuu Ardhi, Godwin Maro (kulia), wakati alipoenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, Novemba 18, 2019, baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Jaji Semistocles Kaijage. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 


  0 0


  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

  UPANDE wa mashtaka katika kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mfanyabiashara Khamis Luwonga 'Meshack' (38), anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuwa upelelezi wa kesi hiyo kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

  Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Novemba 18, mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

  Amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, na kwamba upelelezi umekamilika na  jarada lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyingine ili waweze kufatilia suala hilo.

  Hakimu Ally amearisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu. Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

  Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mkewe Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa hutuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya (kulia) Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico (kushoto) Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Hassan Khamis Hafidh ,[Picha na Ikulu.] 18/11/2019.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa hutuba yake katika viwanja vya Fumba Mji mpya mkoa wa Mjini Magharibi. [Picha na Ikulu.] 18/11/2019.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Tanzania Nd,Josphat Rweyemamu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Wajasiriamali baada ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya Mkoa wa Mjini Magharibi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico wakiangalia Gazeti la Zanzibarleo alipotembelea madanda ya maonesho ya wajasiriamali baada ya kuyafungua rasmi Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya Mkoa wa Mjini Magharibi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico wakifuatana na viongozi wengine wakati alipotembelea madanda ya maonesho ya wajasiriamali baada ya kuyafungua rasmi Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya Mkoa wa Mjini Magharibi 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico mara alipowasili katika viwanja vya Fumba Mji mpya katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.] 18/11/2019.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico mara alipowasili katika viwanja vya Fumba Mji mpya katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo (wa pili kulia) Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Hassan Khamis Hafidh ,[Picha na Ikulu.] 18/11/2019.

  0 0

  .Mh Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(kulia) pamoja na Mkuu wa
  Wilaya Ya Kilosa Mh Adamu Mgoyi (mwenye shati ya draft )na baadhi ya
  wananchi wa kijiji hicho wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa rea katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza katika kijiji cha mabana kata ya mbigiri wilaya ya kilosa mkoani morogoro hapo jana .
  Mh Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu pamoja na Mkuu Wa Wilaya ya
  Kilosa Mh Adamu Mgoyi na baadhi ya wananchi wa kijiji cha mabana kata ya mbigiri wakizungumza na wananchi kabla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa rea katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza wilayani kilosa mkoani morogoro 
  Mkuu Wa Wilaya Ya Kilosa Mh Adam Mgoi (Aliesimama) Akizungumza Na
  Wananchi Wa Kata Ya Mvuha Ndani Ya Wilaya Hiyo Baada Ya Ugeni Wa Naibu Waziri wa Nishati Mh Subira Mgalu Kutembelea Wilaya Hiyo.
  Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Makwambe Kata Ya Mvumi Wilayani
  Kilosa Wakimskiliza Naibu Waziri Wa Nishati Bi Subira Mgalu Alipotembelea Kijiji Hicho.

  *********************************

  NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.

  Wakandarasi Wa Mradi Wa Rea Katika Awamu Ya Tatu Mzunguko Wa Kwanza Wametakiwa Kutekeleza Majukumu Yao Kikamilifu Ili Kufanikisha Adhma Ya Serikali Ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo Katika Maeneo Yao Ikiwa Uunganishwaji Wa Umeme Huo Katika Vijiji Utaleta Manufaa Makubwa Ikiwemo Uuanzishwaji Wa Viwanda Vidogo Vidogo Kuelekea Uchumi Wa Kati.

  Kauli Hiyo Imetolewa Na Naibu Waziri Wa Nishati Bi Subira Mgalu
  Alipotembelea Katika Kijiji Cha Mabana Kata Ya Mbigiri Wilayani Kilosa
  Mkoani Morogoro Kwa Ajili Ya Uzinduzi wa Uwashaji Wa Umeme, Na kuongea na wananchi wa kijiji Makwambe Kata Ya Mvumi Wanaotarajiwa Kupatiwa Umeme Kupitia Mradi Huo.

  Mh.Mgalu Amesema Kumekuwa Na Malamiko Mengi Kutoka Kwa Wananchi
  Hasa Kuhusu Michoro Inayoidhinishwa Na Bodi Katika Uwekaji Wa Nguzo Za Umeme Hivyo Limekwisha Tatuliwa Tatizo Hilo Na Kama Wizara Wametoa Maelekezo Ya Namna Ya Michoro Hiyo Kama Ilivyoidhinishwa Na Bodi Ya Wakala Wa Vijijini Rea.

  Kwa Upande Wake Kaimu Meneja Tanesco Bw.Martin Schilima Na Mkuu Wa
  Wilaya Ya Kilosa Mh Adam Mgoi Wameishukuru Serikali Kupitia Naibu Waziri Mh Subira Mgalu Kwa Hatua Na Jitihada Zinazofanyika Katika Kuwafikia Wananchi Kwa Kuwaunganishia Umeme Na Kuahidi Kushirikiano Nao Pamoja Na Wananchi Kwa Kila Hatua Ili Kuwafikia Kwa Wakati.

  Nao Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Mabana Kata Ya Mbigiri Wametoa
  Shukrani Zao Kwa Kuwashiwa Umeme Katika Kijiji Hicho Na Kuahidi Kufanya Makubwa Katika Kuwaletea Maendeleo Hasa Uanzishwaji Wa Viwanda Vidogo Vidogo Kama Kusindika Nyanya.

  Mradi Huu Upo Katika Awamu Ya Tatu Mzunguko Wa Kwanza Ambapo Kuna
  Vijiji Mia Moja Na Sitini Na Tano Katika Mkoa Wa Morogoro Ambapo Katika
  Wilaya Ya Kilosa Kuna Vijiji 24 Na Mpaka Sasa Vijiji Kumi Vimeshawashwa
  Umeme Na Vijiji Vilivyosalia Kumi Na 4 Vinakwenda Kuwashwa Umeme Kabla Ya Mwezi Desember Mwaka Huu.

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiongozana na madiwani 11 wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamekutana na wanawake na mabinti wanaoishi katika kata ya Mwakitolyo ili kuzungumza nao namna ya kukomesha vitendo vya baadhi ya mabinti wenye umri kuanzia miaka 12 na wanawake watu wazima wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘Chemsha chemsha’.

  Hatua ya mbunge na madiwani hao kukutana na wanawake na mabinti wa Mwakitolyo leo Jumatatu Novemba 18,2019 inatokana na azimio la kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichofanyika Mwezi Agosti mwaka huu ambapo Mhe. Azza aliomba aongozane na madiwani wanawake kwa ajili ya kwenda kuzungumza na mabinti na akina mama ili kukomesha biashara ya ngono katika kata hiyo.

  Akizungumza katika kikao cha ndani na wanawake hao wakiwemo wanaomiliki gesti na nyumba za kupanga kilichofanyika katika kijiji cha Nyaligongo,Mhe. Azza amesema biashara ya ngono inadhalilisha utu wa mwanamke lakini pia kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya zinaa hivyo inapaswa kupingwa na kila mtu.

  “Ndugu zangu biashara ya ngono ni biashara ya kujidhalilisha naomba wanawake na mabinti wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo. Tutafute kazi za kufanya ambazo siyo za kujidhalilisha,kazi yeyote ukiipenda na ukaifanya kwa moyo mmoja ni lazima utafikia malengo yako”,amesema Azza.

  “Acheni biashara hii. Wanawake tutambue heshima tuliyopewa na mwenyezi Mungu,mama ndiyo anayejua kila kitu katika nyumba,mama ndiye aliyebeba majukumu makubwa katika familia,kwa hiyo tunatakiwa tuibebe heshima tuliyonayo badala ya kujidhalilisha”,alisema mbunge huyo.

  Mhe. Azza ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni ‘gesti’ na wanaopangisha vyumba kutoruhusu watu wanaofanya biashara ya kuuza miili.

  Aidha amewashauri kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili ili waweze kupata mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na kwamba hata kama wana biashara zingine basi wajishughulishe pia na kilimo ili wawe na uhakika wa chakula katika familia zao.

  “Nitumie fursa hii kumpongeza mtendaji wa kata ya Mwakitolyo na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kwenda kuwatafuta wanawake na mabinti waliokuwa wanafanya biashara na kuwapa elimu ya kuondokana na biashara hiyo na kuwapatia vyerehani ili waweze kufanya biashara ambayo ni halali,jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa biashara hiyo”,ameongeza Azza. Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake akiwasili katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 18,2019. Picha zote na Said Nassor - Malunde 1 blog 
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake akiwasili katika kata ya Mwakitolyo.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake katika kata ya Mwakitolyo 
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipokelewa katika kata ya Mwakitolyo. Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na wanawake wa kata ya Mwakitolyo.

  Wanawake wa Mwakitolyo wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na wanawake wa kata ya Mwakitolyo.
  Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja akisoma taarifa ya kata ikiwemo biashara ya Chemsha chemsa
  Mbunge wa Azza Hilal na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakisikiliza taarifa ya kata ya Mwakitolyo.
  Diwani wa kata ya Mwakitolyo Limbe Augustine Limbe akizungumza katika kikao hicho.
  Akina mama wakiwa kwenye kikao hicho.
  Diwani wa viti maalumu Chausiku Hassan akizungumza katika kikao hicho. 
  Wanakikundi wakisoma risala mbele ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad 
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akimkabidhi Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja Eploni 50 kwa ajili ya Mama Lishe katika kata ya Mwakitolyo.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na baadhi ya mama lishe baada ya kuwakabidhi Eploni nyekundu zitakazowasaidia kwenye kazi yao.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na baadhi ya mama lishe waliohudhuria kikao cha ndani cha mbunge,madiwani wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja na Mama lishe pamoja viongozi wa halmashauri na kata.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wachimbaji wadogo wanawake kata ya Mwakitolyo.Chama hicho kimemuomba Mbunge kuwa Mlezi wa chama hicho.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja viongozi wa kikundi cha hiari ya Moyo kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo kinachojihusisha na kuweka na kukopa.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja viongozi wa kikundi cha hiari ya Moyo kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha na kikundi cha wanawake na maendeleo kilichoanzishwa kwa lengo la kuwafanya akina mama kuachana na biashara ya kuuza miili yao.Dhamira ya kikundi hicho ni kushusha Punda 200 'ndoo za mawe ya dhahabu' ili kusafisha senga 'mchanga wa dhahabu" 
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na akina mama wa Mwakitolyo.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na akina mama wa Mwakitolyo. 

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga January Lugangika amesema kwamba wilaya hiyo wanahitaji nakala 3000 ya kitabu kilichoandikiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamini Mkapa kutokana na kwamba uwepo wa maeneo mengi ya kuuzia vitabu hivyo.

  Kitabu hicho ambacho kimeandikiwa na Rais Mstaafu huyo ni cha “My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu)” ambacho kilizinduliwa Jumanne iliyopita na Rais Dkt John Magufuli.

  Akizungumza na mtandao huu DC January alimpongeza Rais huyo mstaafu kwa kuamua kuandika kitabu hicho huku akieleza kwamba kwenye wilaya hiyo kuna maeneo mengi ya kuuzia kitabu hicho ikiwemo hoteli za kitalii na kwenye makazi yake

  “Kwanza nimpongeze Rais awamu ya tatu Mstaafu Benjamini Mkapa hapa Lushoto ana makazi yake pia ni sehemu ya utalii anampongeza kwa kuandika kitambu ambacho kitakuwa ni hazina kubwa sana kwa kuwa watanzania hapa kwetu sisi tunapokea watalii wengi”Alisema

  “Kwa mwaka 2018 tulipokea watalii 1400 na mwaka huu 2019 mpaka sasa tumepokea watalii 3000 na mtalii anapokuja lushoto awe na kumbukumbu nzuri ni vuziri akanunua kitabu cha Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kwa ajili ya kumbukumbu”Alisema

  Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kumbumbuku nzuri hiyo ya kitabu mtu anaweza kuwa na kitabu anapotembelea makazi yake akikisoma anaweza kumuuliza swali lolote lile kuhusu kusudio la kuandika kitu ambacho amekiandika kwenye kitabu hicho.

  Aidha alisema pia watajitahidi kila mwana Lushoto awe na nakala moja ya kitabu kuanzia maofisini, watumishi wa umma wote na sekta binafsi ili kuhakikisha kila mkazi wa wilaya hiyo anafuatilia maisha ya kiongozi huyo

  “Lakini pia tutajitahidi kuongeza na watu wa vitabu wapate wakala mmoja na nisema sisi Lushoto tunahitaji si chini ya nakala 3000 tutaviuza kwa wakati”Alisema

  Hata hivyo aliwataka watanzania waone umuhimu wa kununua vitabu vinavyoandikwa na viongozi wastaafu hasa ambao bado wapo duniani ni rahisi kuvisoma na kumpigia kumuuliza alipoandika jambo Fulani alikuwa na maana gani ni sehemu ya utalii na kumbukumbu.

  “Lakini pia niseme tu kwamba Mkapa ni Lushoto na lushoto ni Mkapa hivyo sasa tupo tayari kusoma maisha ya kiongozi huyo kupitia kitabu chake na ndio maana tunahitaji nakala hizo “Alisema DC

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza mbele ya Viongozi wa dini katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini hapa nchini katika Mkutano uliowahusisha viongozi hao pamoja na Mkuu wa Mkoa huyu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.
  Viongozi wa Dini Mbalimbali hapa nchini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Paul Makonda katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.

  **********************************

  Viongozi wa Dini wakiwemo Maaskofu, Mashekhe, Wachungaji,Manabii, Maimamu na Wainjilisti Mkoa wa Dar es salaam leo November 18 wametoka na azimio la pamoja la kumuunga Mkono Rais Dkt. John Magufuli katika jitiada zake za kuleta maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kumaliza kero za Wananchi.

  Hatua ya Viongozi hao wa dini imekuja baada ya Kuvutiwa na taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda dhidi ya Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mkoa huo chini uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli jambo lililowakosha Viongozi wa Dini na Kuamua kuja na tamko hilo.

  Katika mkutano huo RC Makonda amewasilisha kwa Uhalisia wa Video taarifa ya miradi iliyotekelezwa na serikali katika sekta zote muhimu ikiwemo Afya, Barabara, Maji, Umeme, Elimu, Viwanda, Usafirishaji na sekta anyinginezo jambo lilikowagusa viongozi wa dini.

  Pamoja na hayo Viongozi hao wa Dini wamesema wataendelea kumuombea Rais Dkt. John Magufuli azidi kuwa na Nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jami.

  WABUNGE  watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotaka wabunge wanne wa 4 chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.

  Wabunge waliokamatwa leo Novemba 18,2019 ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa huku a Mbunge wa Kawe, Halima Mdee yeye alishakamatwa wiki iliyopita

  Heche na Msingwa wamekamatwa leo mara baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuonana na Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza kesi inayowakabili, Thomas Simba.

  Wabunge hao wameunganishwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika kituo hicho cha Osterbay huku Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akidaiwa kuwa anaumwa na amelazwa.

  Novemba 15, mwaka huu 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru wabunge hao wanne wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kutokufika mahakamani hapo bila ya kutolewa taarifa yoyote wakati kesi yao ya uchocgezi ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

  Kesi hiyo inatarajia kuendelea Novemba 19, 2019 (Kesho) kwaa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizwaji.

  Kabla ya kutoa amri hizo, Novemba 15, mwaka huu kesi  hiyo ilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, ambapo washtakiwa wengine waliwahi lakini wabunge hao wanne hadi saa 4:05 asubuhi walikuwa hawajafika mahakamani bila sababu za msingi.

  Washtakiwa waliofika mahakamani Novemba 15, 2019 ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko.

  Katika Kesi hiyo Mbowe na wenzake wanakabiliwa na  mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

  Pia, wanadaiwa kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salaam..

  Mwisho

  0 0


  0 0


            
   

  0 0


  Kuelekea siku ya Vyoo Duniani wadau mbalimbali wa Afya nchini wametakiwa kutambua changamoto zinazowakabili watu ambao wanajihusisha na uzibuaji wa mitalo mikubwa pamoja na kutapisha mashimo ya Vyoo.


  Imeelezwa kuwa katika jiji la Dar es Salaam zaidi ya asimilia 70 ya wakazi wake yapo katika maeneo ambayo si rasmi. Maeneo hayo sifa zake kunakuwa na changamoto za upatikanaji wa maji safi na Salama, upatikanaji wa huduma za usafi pamoja na huduma za utupaji wa taka maji.


  Hayo yamebainishwa na Meneja miradi mwandamizi wa Taasisi ya WATER AID Tanzania, Bw.Twaha Mubarak  alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wake na Waandishi wa habari kwenye ofisi za taasisi hiyo ya WATER AID jijini Dar es Salaam.


  Akizungumza na wanahabari Bw. Twaha amesema kuwa inakadiliwa asilimia 10 ya jiji la Dar es Salaam limeunganishwa katika mfumo wa maji taka hivyo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuibuka magonjwa mbalimbali yanayoambukiza.


  "Tukizungumzia katika asilimia hizo, asilimia 90 zilizobaki tunatumia aina nyingine za mifumo, moja kwa moja tunatakiwa kufahamu wanaofanya kazi hizo (kutapisha vyoo) ni wale ambao wanaitwa majina mengi kama vyura ama wavamiaji lulu". Amesema Bw. Twaha.

  Aidha Bw. Twaha amesema kuwa katika ripoti ambayo imeandaliwa imezungumzia changamoto hizo kwa mfanya usafi na imesheheni na kudadavua mkanganyiko wanaopitia wafanyakazi katika sekta ya usafi kwenye nchi zinazoendelea.

  Twaha amesema kuwa ripoti hiyo  imeandikwa kwa pamoja kwa shirika la kazi Umimwwnguni, Shirika la Water Aid, Benki kuu ya Dunia na Shirika la Afya Duniani, lengo hasa ni kuinua ufahamu  kuhusu Mazingira hatarishi ambayo wafanyakazi hao wanayapitia.

  Amesema Wafanyakazi hao mara nyingi hugusa kinyesi cha binadamu pasipokuwa na vifaa vya kujikinga wala vitendea kazi vilivyobora, kitu ambacho kinawaweka kwenye hatari za kupata magonjwa mbalimbali.

  Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira na Watu (UMAWA) inayofanya biashara ya usafi wa mazingira katika upakuaj wa vyoo na uchakatishaji wa maji taka, Bw.Mathias Milinga amesema kuwa biashara hiyo imekuwa kwa kiasi tangu kuanzishwa kwake kwani mpaka sasa katika maeneo mengi hasa wilayani Kigamboni upakuaji holela wa vyoo umepungua kwa kiasi kikubwa.

  "Wapakuaji wa kienyeji wakipata kazi mara nyingi wanakuja kwenye kituo, tumefauru kupanua huduma hiyo kwa kufanya matangazo katika vipeperushi lakini pia tunafanya kazi na halmashauri hasa kamati za afya". Amesema Bw.Milinga.
   Meneja Miradi Mwandamizi wa Taasisi ya WATER AID Tanzania, Bw.Twaha Mubarak akizungumza na wanahabari katika ofisi za taasisi hiyo  jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira na Watu (UMAWA) inayofanya biashara ya usafi wa mazingira na uchakatishaji wa maji taka, Bw.Mathias Milinga akizungumza na wanahabari katika ofisi za taasisi ya WATER AID jana  jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwasilisha hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mafunzo elekezi kwa Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu.


  Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika akitoa kwa Wahe. Majaji katika Mafunzo hayo.

  Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Mhe.Jaji  Dkt. Paul Kihwelo akizungumza wakati wa Mafunzo hayo.

   Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza katika Mafunzo hayo.

  Meza Kuu: Katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto,  ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald Ndika, wa pili kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Rose Teemba na wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi.
  Meza kuu katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wapya wanaoshiriki katika Mafunzo elekezi.


   Sehemu ya Wahe. Majaji wapya wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa akifungua rasmi mafunzo.


  Na Magreth Kinabo na Mary Gwera, Mahakama


  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa sehemu ya maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama.


  Akifungua rasmi Mafunzo elekezi ya awamu ya tano (5) kwa Wahe. Majaji 12 walioteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni, Mhe. Jaji Mkuu aliwaeleza Majaji hao kuendeleza maboresho ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa wananchi bila kuangalia maeneo waliyopo. 


  “Mahakama ya Tanzania kwa sasa ipo katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5) pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama (CCP), kwa sasa utekelezaji wake upo katika mwaka wa tatu (3) hivyo nawaalika kuwa sehemu ya muendelezo wa utekelezaji wa maboresho hayo,” alisema Mhe. Jaji Prof. Juma.

  Mafunzo hayo yanayofanyika katika Kituo cha Mafunzo na Habari za Kimahakama Kisutu yamefunguliwa rasmi na Mhe. Jaji Mkuu mapema Novemba 18 mwaka huu.

  Mbali na hilo, Mhe. Jaji Mkuu aliwataka Majaji hao pia kuzingatia dira na dhima za Mahakama ya Tanzania kwa kuwataka kutoa haki kwa wote na kwa wakati bila upendeleo.


  “Mnapotekeleza majukumu yenu msikubali kuingiliwa na mtu yeyote iwe rafiki, mwanafamilia au hata Jaji Mwandamizi juu ya mashauri yaliyopo mbele yenu kwani yapo chini ya mamlaka zenu kikatiba,” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.


  Aliendelea kwa kuwataka Majaji hao kusoma na kuzingatia Kanuni za Mwenendo kwa Maafisa wa Mahakama ‘Code of Conduct for Judicial Officers in Tanzania, 1984’ zitakazowaongoza katika utendaji kazi na vilevile kusimamia na kuviishi viapo vyao.

  Awali akimkaribisha Mhe. Jaji Mkuu kufungua rasmi Mafunzo hayo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi alimshukuru Mhe. Jaji Mkuu kwa kukubali kuruhusu kufanyika kwa mafunzo hayo yatakayoleta tija kwa Majaji hao.


  Mhe. Jaji Kiongozi alisema kwa sasa kuna jumla ya Majaji wa Mahakama Kuu 77 ambao kwa wastani kila Jaji anatakiwa kusikiliza jumla ya kesi 518 kwa mwaka  na kuongeza kuwa ingawa idadi hiyo inaonekana ni kubwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika zikiwemo za kitaaluma bila kuathiri utoaji wa haki.


  “Nina imani kwamba uelewa na uzoefu mkubwa walionao Majaji hawa wapya pamoja na mafunzo wanaoenda kupatiwa yatawawezesha kutoa mchango katika safari ya Mahakama kuelekea Mahakama mtandao ‘e-Judiciary’, kutoa haki kwa viwango vinavyotakiwa na kuwa wawajibikaji wazuri,” alieleza Mhe. Jaji Kiongozi.


  Mafunzo ya aina hii yamekuwa yakitolewa kwa Majaji wapya ambapo hupata fursa ya kujengewa uwezo na wabobezi mbalimbali wakiwemo Majaji Wakuu Wastaafu, Majaji wa Rufani na wa Mahakama Kuu waliokwisha staafu.Katika mafunzo hayo kutakuwa na wawezeshaji mbalimbali wakiwemo Majaji waliopo kazini na Wataalamu kutoka Taasisi kadhaa katika sekta ya Sheria na Utumishi wa Umma.


  0 0

  Katibu wa tawi la CCM China ndugu Yazid Iddi amekabidhi taarifa ya maoni na Mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wanachama wa tawi la CCM China yatakayochakatwa na baadae kuingizwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya 2020-2025.

  Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu Dr. Bashiru Ally akipokea taarifa hiyo amepongeza Viongozi Na Wanachama wa tawi la CCM China kwa kuwa mabalozi wazuri katika kufanya mambo mema yenye tija ya kujenga taifa bora —Novemba 18,2019 —Dodoma,Tanzania


  0 0

  Na, Editha Edward -Tabora .

  Makatibu Tawala wasaidizi wa Elimu katika maeneo mbalimbali Nchini wametakiwa Kuhakikisha Mashindano ya Kusoma, kuandika, Kuhesabu na kuchora Yanafanyika kwa ustadi mkubwa kwa kuzingatia weledi na miongozo iliyotolewa na wizara ili kuleta matokeo chanya na hatimaye kupunguza kabisa idadi ya watoto wasiojua Kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora

  Akifungua Mashindano hayo ya Kusoma, kuandika Kuhesabu na kuchora Afisa Elimu mkoa wa Tabora Suzan Nusu ambaye amemuwakilisha katibu Tawala mkoa wa Tabora Msalika Makungu ametoa wito kwa wasimamizi wa Mashindano hayo kuzingatia weledi huku akibainisha kuwa Sherikali katika utekelezaji wa dira ya Taifa kuekekea uchumi wa kati ni muhimu watanzania kuweka mkazo katika utoaji wa stadi inayozingatia ujenzi wa stadi za msingi za ufundishaji na ujifunzaji

  "Watahini wa kazi hii hakikisheni kuwa mnazingatia usawa na kuepuka upendeleo wakati wote mnapotekeleza majukumu yenu ili tuweze kupata wanafunzi mahiri watakaotuwakilisha vyema kitaifa"Amesema Nusu

  Fatuma Shabani ni miongoni wa walimu waliopata mafunzo hayo amesema yatawasaidia kuwafundisha watoto kwa ueledi na ufanisi kwani wamepata uzoefu wa kutosha na maarifa

  Aidha Mashindano hayo ya utambuzi yaliyojumuisha mikoa mitano Tabora , Simiyu, Singida Dodoma, na Shinyanga yatasaidia kuwaongezea ujuzi walimu lakini pia Ari katika utendaji wao wa kazi.
  Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nusu ambaye amemuwakilisha katibu Tawala mkoa wa Tabora akitoa wito kwenye Mashindano hayo ya kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora
  Wanafunzi wa shule ya za msingi mkoani Tabora waliohudhuria katika Mashindano hayo ya Kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora.
  Mwalimu akiwaelekeza wanafunzi waliohudhuria kwenye Mashindano hayo kwa michoro

  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga baadhi ya machapisho kutoka tume katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria.

   Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Mahiga akiongea na ujumbe waTume ya Haki za Binadamu na Utawala bora uliotembelea ofini kwake mapema Novemba 18, 2019.

   Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kulia kwake). Wengine ni Makamishna wa Tume, kutoka kulia ni Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa, Thomas Masanja, Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga (katikati) akiagana na Mwenyekiti wa tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu. Wengine pembeni waliotabasamu ni Makamu Mwenyekiti Tume, Mohamed Khamis Hamad (kulia), Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli (kushoto), nyuma yake ni Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande.
  Na Mbaraka Kambona,

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuimarisha misingi ya utawala bora nchini ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa jamii.

  Waziri Mahiga alitoa kauli hiyo Novemba 18, 2019 katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria baina yake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Mathew Mwaimu.

  Akiongea katika kikao hicho, Waziri Mahiga alieleza kuwa tume ni chombo muhimu ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia mambo mawili ambayo ni haki za binadamu na utawala bora.

  Waziri Mahiga aliendelea kusema kuwa tume katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake imekuwa ikifanya kazi kubwa katika masuala ya haki za binadamu zaidi ya utawala bora, na hivyo, kuwataka katika awamu hii ya tano wawekeze nguvu zaidi katika kuimarisha misingi ya utawala bora. 

  “Tume ni chombo muhimu katika kujenga ustawi wa jamii, hususani kujenga jamii yenye utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu nchini, lakini msisahau kujenga utawala bora”, alisema Mahiga

  “Mheshimiwa Rais anaposema serikali hii ni ya wanyonge, anataka wale watu walio kwenye mamlaka walijue hilo na wazingatie utawala bora katika kuhudumia jamii, na nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha misingi ya utawala bora inaimarika nchini”aliongeza Maiga

  Katika hatua nyingine Waziri Mahiga aliitaka tume kuieleza na kuifafanulia jamii utekelezwaji wa haki za binadamu unavyotekelezwa kwa vitendo na serikali ya awamu ya tano.

  Mahiga alisema pamoja na changamoto zinazopigiwa na kelele na wadau wa masuala ya haki za binadamu, lakini ni ukweli uliowazi kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza na inaendelea kutekeleza haki mbalimbali kwa vitendo na kuhakikisha haki hizo wananchi wanazipata.

  Alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza kwa vitendo haki ya kupata elimu kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi mpaka sekondari.

  Pia, alieleza kuhusu haki ya afya ambapo wazee wameanza kupata matibabu bure, na upatikanaji wa bima ya afya kwa wananchi.

  “Hizi jitihada zote za serikali katika kuwapatia huduma wananchi bado hazijaelezwa vya kutosha, tume tumieni nafasi yenu kuyaeleza haya kwa jamii iweze kuelewa”alisisitiza Mahiga

  Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome alimueleza Mwenyekiti wa tume kuwa masuala ya haki za binadamu yanafanywa na taasisi nyingi na hivyo kipindi hiki wawekeze nguvu zao katika kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria nchini.

  “Tume ni lazima muonekane mnachukua hatua, wekeni mkakati wa viashiria vya kubaini haraka changamoto zinazoelekea kuathiri utawala bora na kuzifanyia kazi”, alisema Mchome

  Akizungumza mapema, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alimueleza Waziri Mahiga dhamana waliyopewa wataitumia vyema katika kusaidia serikali kutimiza lengo lake la kuifikisha nchi katika uchumi wa kati.

  “Tume itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na tutatekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia taratibu, sheria na katiba ya nchi”alisema Mwaimu

  Mwenyekiti huyo wa Tume alikwenda kutembelea Wizara ya Katiba na Sheria kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri Mahiga ikiwa ndio mara yake ya kwanza tangu alipoapishwa Novemba 4, 2019.

  Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliongozana na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad, na Makamishna wengine watano ambao ni Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

  0 0

  Na Moshy Kiyungi,Tabora.

  Oktoba, 2019.


  “Kizuri hakikosi kasoro” msemo huu wa Kiswahili umejidhihirisha wazi kwa msanii Rehema Chalamila, ambaye ni mrembo mwenye sifa zote za kike, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii la Ray C.

  Aliwahi kujitumbukiza kwenye ‘janga’ la matumizi ya dawa za kulevya, lakini baadaye aliamua kujinasua kwa kuachana nayo.

  Ray C ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, aliyejaaliwa kuwa na umbo la kupendeza, sauti nyororo, sura nzuri inayopambwa na macho yenye mvuto.

  Uhodari wake wa kuzinyonga nyonga umemfanya kuwa maarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

  Rahema alizaliwa mkoani Iringa, Mei 15, 1982, amejaaliwa kuwa uwezo mkubwa wa kuimba muziki wa R&B, dansi, Afro-Jazz, Taarab hata Bongo-Bhangra.

  Kabla ya kujihusisha na muziki, aliwahi kufanya kazi ya utangazaji wa redio ya Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam.Mwaka 2003 Ray C alitoka na albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la ‘Mapenzi Yangu’.

  Msanii huyu aliendelea kujulikana zaidi baada ya kuachia vibao vingine kadhaa kama vile, Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Nawewe Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu zaidi.Juhudi zake katika muziki, hatimaye Ray C akatokea kuwa mwimbaji maarufu aliyeutingisha muziki wa Bongo Fleva kati ya miaka ya 2003 na 2009.

  Sifa zake nzuri zikatambaa kila kona, lakini akaja kuzichafua baada ya kuingia matatani, kiafya alipoanza kutumia dawa za kulevya.

  Dawa hizo zilimtesa kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012, ambapo Rais wa Tanzania wakati huo, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alimpa msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu yake.

  Alianza matibabu bila kuchelewa na mara baada ya kupona, msanii huyo Rehema Chalamila a.k.a Ray C, alikwenda kumtembelea Rais Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliompatia wakati alipokuwa mgonjwa.Katika ziara hiyo Ray C alifuatana na mama yake mzazi Margaret Mtweve na dada yake Sarah Mtweve.

  Akiwa Ikulu, alimweleza Rais Kikwete kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za washabiki wake waliokuwa wamemkosa kwa kipindi kirefu.

  Kwa apande wake, mama mzazi wa Ray C, alimshukuru Rais kwa kuokoa maisha ya bintiye.Mama huyo akatoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya matibabu ya Ray C, waache kufanya hivyo kwani yamegharamiwa na Rais Kikwete.

  Kwa mujibu wa maelezo kutoka Ikulu, Rais alimpongeza Ray C kwa kuikubali hali yake ya kiafya, pia kukubali kupata matibabu ambayo alikuwa akiendelea nayo chini ya uangalizi maalum.

  Lakini kama Waswahili wasemavyo kuwa “Sikio la kufa halisikii dawa”, katika hali ya kushangaza na kusikitisha, Ray C, alikumbwa na mikasa mingi ukiwemo wa mwaka wa 2016, ikaripotiwa kwamba amerudia tabia yake ya kutumia dawa za kulevya!

  Taarifa hizo zilipomfikia Rais Kikwete, zilimsikitisha na kumkera sana.

  Licha ya matatizo yake hayo, Ray C, alifanya kazi kwa kuachia albam za Mapenzi Yangu ya mwaka 2003, na Wewe Milele ya mwaka 2004, Sogea Sogea ya mwaka 2006 na Touch Me ya 2008.

  Ray C, alikwisha twaa Tuzo kadhaa katika kazi zake, zikiwemo za msanii bora wa kike kwa mwaka 2004.Ray C alishiriki na kufanikiwa kupata tuzo za Msanii bora Afrika ya Mashariki mwaka 2005, shindano lililoandaliwa na Channel O Music Awards.

  Mwaka 2006 kampuni ya Pearl of Africa Music Awards, ilimtunuku tuzo ya Msanii bora wa kike Tanzania.Aidha alitwaa tuzo ya msanii Bora wa kike kutoka Uganda na Tanzania na mwaka 2007.

  Ray C alinyakua tuzo ya Msanii bora wa kike Tanzania mwaka 2007 na 2008, zilizotolewa na Pearl of Africa Music Awards.

  Mwaka 2011 Tanzania Music Awards ilimpa tuzo kwa Video bora, Wimbo bora, Wimbo bora wa Afro Pop na Wimbo bora wa kushirikishwa wa 'Mama Ntilie', akishirikiana na Gelly wa Ryme & AT.

  Ray C katika baadhi ya kazi zake aliwahi kuwashirikisha wasanii wengine kama Dknob, Chid Benz, Mheshimiwa Temba, Squeezer pamoja na Nako Nako.

  Mapema Januari 02, 2018 msanii huyo wa muziki wa Bongo Fleva Rehema Chalamila (Ray C), alimuomba Rais John Pombe Joseph Magufuli kupitisha sheria kama aliyofanya Sultan Qaboos wa Oman.

  Rayc C aliaandika ombi hilo kupitia ukurasa wake wa instagram 

  “Mzee mi na shida Moja! hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji Sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili! Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman! Hakuna mahusiano ya Kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa! 

  “Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila Cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea! Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe! Utakuwa umewanyoosha kisawasawa hawa Wanaume zetu. Tutaheshimiana! 

  Msanii huyo mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, alimuanika kwenye mitandao ya kijamii mpenzi wake mpya.

  Ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na Rapa Lord Eyes, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumtambulisha mpenzi wake huyo.

  Kila la heri Rehema Chalamila aka Ray C, baadhi ya wadau wa muziki huo wanakusihi kuachana kabisa na dawa za kulevya.


  Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao ya kijamii.
  Mwandaaji wa makala hii anapatikana kwa namba: 0713331200, 0736331200, 0767331200 na 0784331200.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitambulishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela (katikati) kwa Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRD Dkt. Joseph Witts wakati alipowasili kufungua Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini lililofanyika Mkoani Mtwara.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
  David Jere, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi (CRDB) akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.

  Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kongamano lililo andaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wakandarasi ,wazabuni na wafanyabishara wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, lilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu, mjini Mtwara. Kongamano hilo lililenga kuwapatia washiriki hao elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo wanazozichukua kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

  Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, wakandarasi ni sekta muhimu sana katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hivyo wanapaswa kuboresha utendaji kazi wao kwa kuchukua mikopo toka taasisi za fedha na mabenki. Ameongeza kuwa, changamoto kubwa inayowakabili wakandarasi wengi ni ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ambapo changamoto hiyo huchangia kutomalizika kwa miradi kwa wakati.

  “Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni vilivyo, changamkieni fursa hizo ili muweze kukuza biashara zenu na kupata faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana wetu na hatimaye kulipa kodi stahiki za serikali. Ni matarajio yangu kuwa, baada ya kongamano hili tutaona utofauti mkubwa kutoka kwa wakandarasi na halmashauri, ambao wamekuwa wakipitia changamoto katika kukamilisha miradi yao, kutokana na suala la mapato na ukwasi” alisema Waziri Mkuu.

  Mheshimiwa Majaliwa pia alipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa miondombinu mbalimbali ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi.

  Alisema “Benki ya CRDB imekuwa ina fadhili miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika jitihda zake za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Tunatambua na kuthamini sana ushikiri wa Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi wa umeme wa maji katika bonde la Rufiji (Nyerere Hydro Power Project) na ule wa kusambaza nishati ya umeme vijijini yaani REA.

  Kipekee kabisa niwapongeze tena Benki ya CRDB kwa utayari wenu, ambao mmekuwa mkiuonesha katika kuisaidia Serikali, hususan katika utekelezaji wa miradii mikubwa ya kimkakati”. alisema.

  Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema kuwa,kongamano hili ni fursa pekee ya kuwakutanisha wakandarasi, wazabuni na wafanyabisahra ili kuwajengea uwezo na kuwajulisha fursa mbalimbali za kifedha zilizomo ndani ya benki ya CRDB, na namna ya kuzitumia fursa hizo ili kukuza miradi na biashara zao.

  “Tuna bidhaa nyingi mahususi kwa ajili ya kundi hili la wateja ikiwamo: Purchase Order Financing, Contract financing, and Invoice Discounting ambazo hazihitaji dhamana yoyote kutoka kwa Mkandarasi au mzabuni pindi anapotaka kukopa. Zaidi ya hilo, Benki pia hutoa mikopo kwa ajili ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, magari, mashine, Mabasi na huduma nyingine kama vile dhamana ya malipo ya awali (Advance Payment Guarantee), dhamana ya Utekelezaji wa Miradi (Performance Guarantee), Barua za Mikopo (Letters of Credit), Huduma za Bima na pia tunatoa mikopo ya muda mfupi kama mitaji ya kufanyia kazi” alisema.

  Naye mmoja wa Wakandarasi Henry Shimo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chibeshi constructions Ltd , amesema kuwa, swala zima la uwezeshwaji wa mikopo hiyo litawasaidia kwa kiasi kikubwa sana wakandarasi hao kumaliza miradi yao kwa wakati kwani changamoto kubwa ilikuwa ni mitaji kwa ajili ya kuendeleza miradi yao. Amesema kuwa, kinachotakiwa kikubwa ni uaminifu wa wakandarasi katika kujua fedha wanayopewa inahitaji kufanyiwa kazi na kurudishwa kwa wakati.

  0 0


  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, amesema CCM wanaodhani itaondoka madarakani wamechelewa bali itaendelea kuongoza nchi kutokana na misingi yake na kukubalika kwa wananchi.

  Alisema vipo vyama barani Afrika vilianguka na kuondoka madarakani sababu ya viongozi wake kushindwa kusimamia misingi lakini si kwa CCM.

  Kalli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bwiru jana kuwa, CCM itendelea kuongoza na kushika kwa miaka 100 kutokana na uimara wa misingi yake na jinsi inavyokubalika kwa wananchi.

  “Zipo nchi zinaongozwa kifalme,kidini na kisiasa.Tanzania inaongozwa kisiasa chini ya Chama Cha Mapinduzi , hivyo kitendelea kuongoza kwa muda mrefu kutokana nakutekeleza mmbo mengi ya kijamii, wenye ndoto kuwa kitaondoka madarakaniwamechelewa sana,”alisema.

  Katibu wa CCM mkoani humu alisema tangu nchi ipate Uhuru mwaka 1961 ni mengi yamefanywa katika sekta mbalimbali ukiwemo ujenzi wa shule, hospitali, vituo vyaafya na zahanati, reli,miundombinu ya barabara na maji, yote hayo si miujiza nikazi ya CCM.
  Alisema wakati nchi inapata Uhuru akina mama walijifungulia vichakani, kulikuwa na shule 22 za sekondari lakini leo kila kata ina shule ya sekondari na nyingine zaidi yamoja na akina mama wanajifungulia vituo vya afya na hospitali.

  Kallia alifafanua kuwa Mwalimu Nyerere aliweka misingi ya usimamizi wa elimu wakiwemo viongozi wengine waliofuata baada yake na sasa Rais John Magufuli anatoa elimubure huku wazazi wakibaki kuangalia mahitaji mengine ya watoto, malezi na nidhamu.

  “RaisMagufuli amenunua ndege lakini wapo wanaopinga hazina maana, si lazima tuzipande wote la hasha.Wataokazipanda watalipa nauli na serikali itaongeza shule nyingine na kutoa huduma zingine kwa wananchi,”alisema Kalli.

  Alielea kuwa elimu wanayoitafuta itawapa heshima wanafunzi haona hivyo hawana budi kujibibidisha kwenye masomo ili wapatikane wana sayansi wakumrithi Rais Magufuli, maprofesa,madaktari na watalaamu wa kada zingine lakini pia wajenge uzalendo kwa nchi yao kabla na baada ya masomo .
  Aidha,Kalli ambaye alikuwa shuleni hapo kushiriki na wanafunzi wa klabu ya Jogging kufanya mazoezi ya kujenga mwili alitumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi hao pamoja na jamii kufanya mazoezi yakuimarisha miili yao na kujenga afya ili kuepukana na maradhi.sss

  0 0

  Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana jana baada ya kufanya nao mazoezi ya kiungo pamoja. PICHA ZOTE NA BALTAZAR MASHAKA MWANZA.
  Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana akiwaongoza wanafunzi wa shule hiyo kufanya mazoezi pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli jana.
  Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, wa tatu kutoka kukaa akishikiru mazoezi ya viungo pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana jana.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana wakifanya mazoezi ya kujenga mwili pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, wa pili kutoka kila jana.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mbele) wakiwa kwenye kikao kazi na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kikao kazi hicho kilikuwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Waziri huyo ndiye mwenye dhamana ya kushughulikia masuala ya muungano.


  ……………………..

  Na James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman wamefanya kikao kazi kujadili namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma kwa umma pamoja na kuimarisha Muungano ili uendelee kuwa na tija kwa wananchi.

  Akifungua kikao kazi hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema pamoja na kujadili masuala ya kuboresha huduma pia kililenga kuimarisha muungano ili kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa taifa letu Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

  Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, katika kikao kazi hicho wameweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wa pande zote mbili za muungano ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

  Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema wao kama mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wanataka ushirikiano wa taasisi zinazoshughulikia masuala ya kiutumishi na utawala bora uendelezwe kwa vitendo kwa ajili ya manufaa ya wananchi.  Mhe. Suleiman amesisitiza kuwa, ushirikiano huu una manufaa katika kuboresha huduma zitolewazo na taasisi za umma kwa wananchi na una tija katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Taasisi za Umma nchini.  Mhe. Suleiman amewataka wajumbe wa kikao hicho, kuhakikisha misingi madhubuti ya kiutendaji iliyojengwa katika kikao kazi hicho inaimarishwa ili utekelezaji wake uwe wa vitendo na uweze kuwa chachu ya kutoa huduma bora kwa wananchi.  Masuala yaliyojadiliwa katika kikao kazi hicho kudumisha ushirikiano katika masuala ya Ajira, Serikali Mtandao, Udhibiti wa rushwa, Usimamizi wa Maadili ya Viongozi, Mafunzo kwa Watumishi wa Umma, Utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Utumishi wa Umma, Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma, Uandaaji wa Miundo na Mifumo ya Taasisi na Utawala Bora kwa ujumla.

  0 0

  Shule ya msingi vilima vitatu, ambayo amekarabati madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo na kuweka madawati na vitatu ukarabati ambao umefanywa na Taasisi ya Chemchem Association na amekabidhi umegharimu zaidi ya sh 54.2 milioni.
   Mkuu wa wilaya Babati Elizabeth Kitundu akiwa na watendaji wa taasisi ya chemchem na viongozi wa kijiji cha vilima vitatu wakiwa wanatembelea shule ya msingi Vilima vitatu.

  Mwandishi wetu,Babati. 

  Mwekezaji katika sekta ya Utalii, wilayani Babati mkoa wa Manyara,Taasisi ya chemchem association, amekabidhi shule ya msingi vilima vitatu, ambayo amekarabati madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo na kuweka madawati na vitatu ukarabati ambao umegharimu zaidi ya sh 54.2 milioni.

  Shule ya msingi vilima vitatu ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madarasa, vyoo, nyumba na walimu na madawati na kusababisha wanafunzi kusoma chini.

  Akizungumza katika hafla ya kukabidhi shule hiyo, mkuu wa wilaya babati Elizabeth Kitundu ,kukarabatiwa na kujengewa majengo mapya katika shule hiyo, ni mchango wa mwekezaji huyo katika kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha elimu.

  Kitundu ameipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika sekta ya elimu pia amewataka waendelee kushirikiana na wananchi wa Kijiji hicho ambacho kampuni hiyo, imewekeza katika utalii wa picha na hoteli.

  " Maendeleo yanakuja kwa kuletwa na elimu hivyo ninaomba muendelee kushirikiana ili kuleta maendeleo katika Kijiji hiki ili kutatua changamoto zilizopo hapa". alisema

  Alisema hata hivyo, kampuni hiyo ambayo imewekeza ndani ya hifadhi ya jamii ya Burunge, inahimiza wananchi kutunza wanyamapori na kuacha vitendo vya ujangili lakini pia kutunza na mazingira ili watalii waendelee kufika katika maeneo yao na hivyo kupatikana fedha za misaada.

  “kama tukiendelea kutoa ushirikiano kwa mwekezaji huyo, kuacha kuharibu mazingira watalii watakuja zaidi na hivyo wao wanafaidika na sisi wananchi na serikali tutaendelea kunufaika”alisema

  Afisa maendeleo ya jamii ya taasisi ya Chemchem ,Walter Pallangyo alisema pallango alisema wataendelea kushirikiana vizuri na wananchi katika kusaidiana elimu Bora pamoja na mahitaji mengine .

  Pallango aliwaomba wananchi kuendelea kutunza mazingira na uhifadhi wa wananyama kwani mazingira yanapokuwa mazuri tunapata wageni wengi maana fedha hizo zinatokana hifadhi hiyo ili wazidi kufanya maendeleo

  Afisa mtendaji wa Kijiji Husna Shabani amesema kuwa taasisi hiyo inatijitoa kwa hali na Mali katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo , ikiwa marekebisho yaliyofanyika ni vyumba vya madarasa nane ,ofisi za walimu mbili, nyumba za walimu tatu,ujenzi wa vyoo vya matundu manne pamoja na madawati Mia moja 100 vyote hivyo vikiwa na thamani ya sh 54.2 milioni.

  Husna aliendelea kusema hata hivyo taasisi hiyo imeweza kuwaletea vitabu vya kufundishia vyenye gharama ya sh 325,700 hivyo shule hiyo imekuwa na mafanikio katika taaluma Kila mwaka mwaka.

  “mwaka ,2017 walifanya mtihani 23 na walifaulu wote pia 2019 walifanya mtihani 20 na walifaulu 19 kwa wastani alama ya 150 kupitia maboresho hayo hali ya taaluma itaboreka na utoro unapungua k na matunda ya ukarabati huo umetokana na hifadhi ya jamii burunge”alisema

  Akizungumza mkuu wa shule vilima vitatu Denis Mtui alishukuru chemchem kwa kuweza kukarabati shule hiyo maana awali shule hiyo ilikuwa chakavu Sana katika sekta zote tofauti na Sasa shule hiyo inatia hamasa ya kuonekana shule Bora kimuonekano na kielimu pia.

  Mtui alisema aliahidi watatunza shule hiyo na kuendelea kukarabati inapopata shida pia anaomba wananchi kuwa naushirikiano mzuri katika kuleta maendeleo yaliyonatija katika jamii ikiwepo kuacha matukio ya kuvamia maeneo ya mwekezaji kuingiza mifugo.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo katika kikao kilichomkutanisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Wakurugenzi kutoka Sekta ya Ujenzi, jijini Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa taarifa ya miradi ya barabara iliyotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Amos Cheptoo, alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amos Cheptoo (kushoto), akisisitiza jambo katika kikao kilichomkutanisha Mtendaji huyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na wakurugenzi kutoka Sekta ya Ujenzi, jijini Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kulia), akimwonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amos Cheptoo (kushoto), miradi ya barabara iliyotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki hiyo, jijini Dodoma.
  Wakurugenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (hayupo pichani), katika kikao kilichomkutanisha Waziri huyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amos Cheptoo, alipofika ofisini kwake na kufanya mazumgumzo nae kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya barabara inayofadhiliwa na Benki hiyo, jijini Dodoma.


  …………………
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuendelea kutekeleza mkakati wake wa ufadhili wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya barabara.

  Ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati Waziri huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo kuhusiana na maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara inayofadhiliwa na benki hiyo.

  “Tunawashukuru AfDB kwakuwa miongoni mwa wadau muhimu katika kutoa ufadhili wa utekelezaji na uboreshaji wa barabara nyingi nchini, tunaomba muendelee na ufadhili kwani bado tunahitaji kuendelea kuunganisha mtandao wa barabara kati yetu na nchi jirani”, amesema Waziri Kamwelwe.

  Aidha, Waziri huyo amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka 11 iliyopita Benki hiyo imetoa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi Trilioni mbili (2) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 1,655 ambapo kati ya hizo kilometa 1,168 zimeshakamilika na kilometa 487 bado zinaendelea na ujenzi wake.

  Ametaja baadhi ya miradi ya barabara iliyofadhiliwa na Benki hiyo na ambayo imekamilika kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo ni ukarabati wa barabara ya Arusha – Namanga (km 105), barabara ya Singida – Babati – Minjingu ( km 223.5), barabara ya Iringa – Dodoma (km 260) na barabara ya Namtumbo – Tunduru (km 193).

  Ameongeza kuwa miradi mingine ya barabara inayoendelea kutekelezwa kupitia ufadhili wa Benki hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 349), barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka kwa Awamu ya II, barabara ya Tanga – Pangani – Bagamoyo (km 246), barabara za mzunguko katika jiji la Dodoma, na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Msalato jijini Dodoma.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB, Amos Cheptoo, amesema kuwa AfDB itaendelea kuunga mkono na kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara lengo ni kuifanya Afrika kuendelea kiuchumi.

  Amesema kuwa lengo la kuja kwake Tanzania ni kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki hiyo ili kuona maendeleo yake.

  0 0


  Na Ismail Ngayonga,MAELEZO
  DAR ES SALAAM


  Maji ni hitaji muhimu sana katika ukuaji wa uchumi  na hii inatokana na ukweli kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote duniani  yawe ya viwanda, kilimo na kadhalika yanategemea maji.
  Aidha Maji ni hitaji muhimu sana katika uhai wa mwanadamu na viumbe wengine na ndio maana maji hayana  mbadala na pia bila maji hakuna uhai na hivyo serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji ili kuimarisha uendeshaji na utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.
  Huduma za maji mijini hutolewa kupitia Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwenye Miji Mikuu ya Mikoa 23 pamoja na Dar es Salaam; Miji Mikuu ya Wilaya 99, Miji Midogo 14; na miradi 8 ya maji ya Kitaifa ili kufikia malengo yaliyopo ya kuboresha huduma hiyo katika Miji Mikuu ya Mikoa kutoka asilimia 86 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020
  Taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Maji inaonesha kuwa mwaka 2016, Uzalishaji wa majisafi maeneo ya mijini umeongezeka kutoka lita milioni 385 kwa siku mwezi Aprili 2015 hadi kufikia lita milioni 470 kwa siku mwezi Machi, 2016 sambamba na ongezeko la idadi ya wateja waliounganishiwa huduma ya maji kuongezeka kutoka kutoka 362,953 mwezi Aprili, 2015, hadi wateja 405,095 mwezi Machi, 2016 ambapo wateja 392,942 sawa na asilimia 97 wamefungiwa dira za maji.
  Aidha makusanyo ya maduhuli kwa mwezi yatokanayo na yatokanayo na mauzo ya maji yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 7.28 mwezi Aprili, 2015 hadi kufikia Tsh. Bilioni 8.50 mwezi Machi 2016 sawa na ongezeko la asilimia 17.
  Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika sekta ya maji nchini, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikuu ya Mikoa ili kufikia asilimia 95; na Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2020.
  Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa anasema katika mwaka 2018/2019, Serikali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini kwa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi na majitaka pamoja na kuzijengea uwezo Mamlaka za Maji Mijini.
  Akbainisha baadhi ya Miradi inayotekelezwa na Serikali katika Miji Mikuu ya Mikoa, Waziri Mbarawa anasema katika Manispaa ya Kigoma Serikali kwa kushirikiana na  na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya inatekeleza mradi wa usambazaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa gharama ya Euro milioni 16.32, ambapo hata hivyo mwaka 2018 Serikali imesitisha mkataba na mkandarasi wa mradi huo kutokana na uwezo mdogo wa mkandarasi.
  ‘’Hadi kuvunjwa kwa mkataba, utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 87 na mradi ulikuwa umeanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi, kutokana na hali hiyo, Wizara imechukua jitihada za kuhakikisha huduma iliyokuwa ikitolewa kwa wakazi wa Mji wa Kigoma inarejeshwa kwa kuajiri mkandarasi wa kuweka mitambo ya muda ya kusukuma maji’’ anasema Waziri Mbarawa.
  Kuhusu Jiji la Arusha,, Waziri Mbarawa anasema Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji majisafi na uboreshaji wa huduma ya uondoaji wa majitaka katika Jiji la Arusha kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 233.9.
  Anaongeza kuwa Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na uchimbaji wa visima virefu 56, ujenzi wa matanki 10; ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji, upanuzi na ukarabati wa mtandao wa mabomba ya majisafi, upanuzi na ukarabati wa mtandao wa majitaka, ujenzi wa mabwawa mapya 18 ya majitaka, ujenzi wa ofisi ya Mamlaka; ununuzi wa vitendea kazi na kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi.
  Akifafanua zaidi Waziri Mbarawa anasema hadi mwezi Aprili 2019, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020, ambapo kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 200 kwa siku na muda wa upatikanaji wa huduma ya majisafi utaongezeka kutoka wastani wa saa 12 za sasa kwa siku hadi saa 24.
  Waziri Mbarawa anasema katika Manispaa ya Lindi, Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya inatekeleza mradi wa majisafi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Lindi unaogharimu Euro milioni 11.7 ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017 lakini haukukamilika kutokana na uwezo mdogo wa kiutendaji wa mkandarasi.
  Anasema kuwa Serikali ilichukua hatua ya kuvunja Mkataba na Mkandarasi huyo mwezi Oktoba 2018 ambapo utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 92.3 na unatoa huduma ya maji kwa wakazi wapatao 81,343 wa Mji wa Lindi, ambapo kazi zilizobaki ni kufunga mfumo angalizi wa uzalishaji maji, ununuzi wa gari la uondoaji majitaka na kurekebisha maeneo yenye mapungufu katika mradi huo.
  Aidha Waziri Mbarawa anasema katika mpango wa muda mfupi wa kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Njombe, Serikali imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa chemchemi ya Kibena uliogharimu Tsh. bilioni 1.1, ukihusisha  ujenzi wa kidakio cha maji, ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa kilomita 2.2 na ufungaji wa pampu mbili za kusukuma maji zenye uwezo wa kuzalisha lita 72,000 kwa saa.
  Kukamilika kwa mradi huo kumeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 480,000 hadi lita 864,000 kwa siku na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika Hospitali ya Kibena, Chuo cha Uuguzi, na Ofisi za Makao Makuu ya Mkoa na hivyo kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Njombe kutoka asilimia 69 mwaka 2016 hadi asilimia 87 za sasa.
  Ili kufanikisha malengo yaliyopo, ni wajibu wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika miji mikuu ya Mikoa kuimarisha hali ya Uzalishaji wa majisafi pamoja na kupunguza kiwango cha upotevu wa maji pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma iliyo bora na endelevu kwa wananchi.